Love Story

Julie Imperia



Aliyekuwa Rais wa Ufaransa alichukua somo la kuongeza nguvu za mapenzi ili
 aweze kumfurahisha mkewe Carla kitandani alichukua somo maalumu la
mapenzi kutoka kwa mwalimu mmoja wa kike,ili kuongeza nguvu zake za kiume.
Sarkozy al
iingia mara kadhaa kwa wiki kupata somo la mwalimu Julie Imperial aliyempa
mazoezi ya kuongeza nguvu za kiume ambapo alimpa euro 160 kwa lisaa limoja.

Akibainisha mwalimu huyo alisema"kuwa na misuli yenye nguvu kuongeza ufanisi
 katika mapenzi."
"Kufika kileleni mapema kwa wanaume kunatokana na upungufu wa nguvu
katika misuli ya maeneo ya siri"alisema Imperial

Ili kuongeza nguvu za mapenzi za rais huyo Imperial alibaki na rais huyo mwenye
 umri wa miaka 53 akimpa mazoezi mbali mbali katika masomo yake.
Katika miezi kumi iliyopita Julie Imperial,mcheza dansi na muongoza mazoezi wa
zamani amemsaidia rais Sarkozy kupunguza kilo 4 na kupungua saizi mbili za suruali
"ili kuhisi misuli yako ya maeneo ya siri fikiria kwamba unahitaji kukojoa na wewe
unajizuia kukojoa,hii ni kwa wanaume na wanawake pia".

Bi Imperial anawachaji wateja wake kati ya euro 110 na euro 180 kwa saa.
Miongoni mwa wateja wake ni wafanyabiashara wakubwa,wanasheria na watoto
 wa wafalme wa Saudi Arabia na Qatar.

Sarkozy alipelekwa na mkewe Carla kwa mtaalam huyo.
                           
                                   
                                       ATHARI ZA KUFANYA MAPENZI MARA MARA

Wapenzi wengi hasa wale ambao uhusiano wao ni mchanga hupenda sana 
kufanya mapenzi kila wanapokutana au wanapohisi
wamehemkwa na miili yako.

 Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini linapokuja suala

 la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo huleta madhara kwa watu
 wanaoendekeza sana ngono.

Kuna watu ambao hawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku wengine wakikosa 

uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu. 

 Mtu anaweza kuwa na mke na kujikuta kila siku anatumia ‘chakula cha usiku’ 

 kwa sababu tu hakuna wa kumkataza na kwamba ana haki ya kufanya hivyo kwa sababu
 amelipa mahari.

Hilo linaweza kuwa jambo jema kwa upande mwingine, lakini uchunguzi unaonyesha 

kuwa watu wengi kati ya watu wanaolalamika kupoteza hisia za kimapenzi hutoka 
katika kundi la watu wapenda ngono.

 Pamoja na tatizo hilo, yapo madhara mengine mengi ambayo mtu asiyekuwa na

 kiasi katika tendo la ndoa anaweza kukabiliana nayo, hivyo ni vema tukajifunza
 ili tusiwe watu wa kuendekeza miili kiasi cha kulazimika kufanya mapenzi kila 
tunapokutana hata kwenye nguzo ya umeme na chini ya miti kwa vile tu miili 
imetaka kufurahika.
 KUPOTEZA HAMU YA TENDO
Watu wenye pupa za kufanya mapenzi hupoteza haraka hisia za kimapenzi kwa 
 wapenzi wao kutokana na sababu za kisaikolojia zinazoweza kujitokeza wakati 
wa ufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa mara.

 Sababu hizo zinaweza kuwa ni pamoja na zile za kumzoea 
mwenza kiasi cha kukosa msisimko hata anapomuona akiwa mtupu.


 Aidha kukinai haraka staili za kimapenzi  kunatajwa kujitokeza 
kutokana na kukutana mara kwa mara kwa aina zile zile za mapenzi 
na pengine sehemu moja, kitanda kimoja na chumba kile kile,
 jambo ambalo linaweza kumfanya mhusika asione jipya kutoka 
kwa mwenza wake na hivyo kupoteza hamu naye na kuhisi kama
 hawezi tena kushiriki tendo la ndoa kikamilifu.

 KUUJAZA MWILI TAMAA KUBWA
Tabia ya kufanya mapenzi mara kwa mara huongeza uzalishaji wa homoni 
mwilini na kuufanya mwili uwe na msukumo mkubwa wa kutaka kuridhishwa
 kwa tendo la ndoa bila kukosa na hivyo kumfanya mhusika asiwe mtu mwenye 
 uwezo wa kuzuia tamaa na kukosa chaguo la nani wa kufanya naye mapenzi na 
kwa wakati gani

 Watu wanaojiendekeza katika kufanya mapenzi mara kwa mara ndiyo

 wale ambao kila wanayemtazama barabarani humtamani bila kujali 
hadhi yake. 
Hawa ndiyo wanaobaka, kusaliti ndoa zao hata kwa watumishi wa ndani
 au kufanya mapenzi na watoto wao wa kuwazaa kwa vile akili zao huwa 
zimeathirika kwa tamaa ya mapenzi. 

Unapokuwa mtu wa kufanya mapenzi mara kwa mara huwezi kuwa na uwezo 

wa kuzuia tamaa yako. Mumeo akiondoka siku mbili unatamani kuwa 
hata na houseboy ili akukate kiu ya penzi. 

 KUPOTEZA RAHA KAMILI YA TENDO
Raha ya tendo hutegemea sana hisia iliyokuzwa kutokana na mapenzi sahihi na

 kiu ya kufanya mapenzi, hivyo basi ukiwa mtu wa kufanya mapenzi kila mara 
unaweza kupoteza msisimko wa tendo na kujikuta unapata furaha ambayo 
haikutoshi kumaliza tamaa yako.

 Kama ni mapenzi utakuwa unayafanya kwa mazoea tu na msisimko 

wako utakuwa mdogo!
 KUPOTEZA NGUVU ZA MWILI
Madhara mengine yanayoweza kupatikana kwa kufanya mapenzi mara kwa mara 
ni pamoja na kupoteza nguvu nyingi za mwili. 

Kama tujuavyo tendo la ndoa hasa kwa wanaume huwafanya watumie nguvu 

nyingi, hivyo kuufanya mwili uchoke. 

Aidha lishe inapokuwa ndogo kwa wafanya mapenzi mwili hukosa nguvu za

 kutosha kuhimili misukosuko ya kimaisha.

 Sambamba na hilo mbegu za uzazi zinazotoka kwa wanaume 

wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa dhaifu.

 KUPATA MAGONJWA
Kama tulivyojifunza kuwa watu wanaofanya mapenzi mara kwa mara

 huwa na tamaa na hujikuta wanafanya mapenzi holela ambayo huweza 
kuwasababishia magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi.

Ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na msukumo wa kutosha hasa

 kwa wanawake huwafanya waishiwe msisimko na kuzifanya sehemu
 zao za siri kutotoa ut
e unaoweza kuwakinga na michubuko wakati wa kujamiiana na hivyo 
kuwasababishia michubuko itakayoweza kuleta maambukizi ya haraka ya 
magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi.

 Baada ya kungalia madhara hayo machache ni vema kwa wapenzi

 kupunguza kiwango cha kufanya mapenzi ili kuifanya miili iwe na uvumilivu 
unaoweza kumsaidia mtu kukaa kwa muda mrefu bila kumsaliti mpenzi wake
 hata kama atakuwa amesafiri mbali naye kimasomo, kikazi au kibiashara.
                                                      JINSI YA KUISHI NA MPENZI ANAE PENDA PESA

 
HAPA tunazungumza kuhusu mapenzi kama kawaida yetu. Leo nimekuja na mada ambayo naamini itawagusa wengi. Marafiki zangu, kusaidia katika mapenzi ni jambo zuri tena lenye mantiki sana.
Suala la kusaidiana si la upande mmoja. Linaweza kuwa kwa wote, kwa
mwanaume au mwanamke. Ni kati ya nguzo muhimu katika mapenzi, lakini kwa bahati mbaya kuna wale ambao wamekuwa na tabia ya kupenda sana fedha!
Unajua wenzi wanajuana kulingana na wanavyoishi, hivyo ni rahisi sana kumgundua mwenzako kama anapenda sana fedha au ni kweli ana tatizo linalohitaji msaada wako. Hii ni kasoro, lakini haimaanishi kwamba ndiyo sababu ya kuachana.
Katika mada hii ipo dawa ya namna ya kudumu katika mapenzi motomoto na mwenzi wa aina hii. Imekuwa ni kawaida kumsikia msichana akitamba mbele ya wasichana wenzake kwa kusema: “Mimi nina kibuzi changu bwana kila ninachotaka kinanipa, kinajua kisiponipa nakitosa tu, yaani nakichuna kama sina akili nzuri.”
Umewahi kukutana na maneno ya aina hii? Bila shaka jibu ni ndiyo. Si hivyo tu, wapo wanaume pia ambao ni kero kwa wapenzi wao, yaani wamegeuka wanaume kama mabinti kwa tabia zao za kutegemea kupewa kila kitu na wapenzi wao hata kama wanao uwezo wa kuvipata vitu hivyo kama watajishughulisha.
Ninachotaka kusema leo ni kwamba, mapenzi ya kweli hayana uhusiano wowote na fedha, ukiona mpenzi wako anaweka fedha mbele na ukishindwa kumpatilizia anachokitaka anakasirika, jua penzi lake lina walakini, hakupendi bali anataka kukutumia kisha kukuacha.
Katika mapenzi hatukatai suala la kusaidiana, mpenzi wako akiwa na shida fulani akaomba umsaidie, kama unao uwezo msaidie na kama huna mueleze ukweli kisha muangalie namna nyingine ya kumsaidia.
Itakuwa siyo busara kama utakuwa na tatizo lakini ukaona kwamba ukimweleza mpenzi wako ataona unamchuna. Wapenzi wanaopendana kwa dhati hawachunani bali wanasaidiana na hili ni kwa pande zote mbili.
Kinachokera ni kutoishiwa na matatizo na wakati mwingine unakuta kuchuna kwingine ni kwa mambo ya starehe. Yaani sasa hivi umemuomba mpenzi wako vocha, hajakaa vizuri umemtaka akija akuletee chipsi mayai, baadaye unataka akutoe ‘out’, bila kujali kwamba wakati huo mpenzi wako ana fedha au laah.
Katika mazingira hayo unadhani mpenzi wako atashindwa kukuchoka? Akikuacha kwa sababu hiyo utamlaumu? Kimsingi ukiwa na mpenzi mwenye tabia ya kutaka kukuomba fedha kila wakati tena katika matumizi mengine ambayo siyo ya msingi, mbinu zifuatazo ni muhimu kuzifuata. Twende tukaone.
MWELEZE UKWELI
Kama huna fedha wakati mpenzi wako anakuomba, mueleze wazi kuwa huna na kamwe usijaribu kutoa ahadi ambazo huenda ukashindwa kuzitimiza. Usiwe mtu wa kutoa ahadi za uongo, mara nitakununulia hiki na kile.
Mwanaume hatakiwi afahamike siku ana fedha au hana. Maana kuna wenzangu ambao siku za mishahara wanabadilisha hadi kutembea! Mwanamke akijua hilo naye ataongeza ‘mizinga’ ili afaidi.
JENGENI KUSAIDIANA
Jambo la muhimu ambalo wanaume wengi wanalisahau ni kutokuwafundisha wapenzi wao wajibu wa kutoa. Utakuta kila kitu ananunua yeye, hata nauli ya basi analipa, wakati mpenzi wake ana kazi yake.
Ifike wakati kwa makusudi, mwanaume ampe majukumu ya kufanya mpenzi wake, hiyo itamsaidia mwanamke kujua namna fedha zinavyokuwa hazitoshi na ataweza kubana matumizi.
ACHA UFUJALI
Kuna wanaume wengine tangu wanatongoza wanakuwa ni wafujaji wakubwa wa fedha kwa kutoa ofa na zawadi kibao. Hii inaweza kumjengea imani mpenzi wako kuwa unazo!
Unachotakiwa ni kudhibiti mapema matumizi yako hata kama fedha itakuwepo. Ifahamike kuwa kutoa hakushibishi uhitaji, kadiri unavyotoa ndivyo unavyoongeza mahitaji. Weka maisha yako katikati usijidai tajiri kumbe ni kapuku tu.
BAKI NA HILI
Katika kumalizia niseme tu kwamba, mapenzi si kukomoana, bali kusaidiana. Jenga tabia ya kumsaidia mwenzako ili siku na wewe ukiwa na tatizo akusaidie.
Kitu unachotakiwa kukiepuka ni kuwa tegemezi hadi unakuwa kero. Kumbuka kumpiga mizinga mpenzi

KWA KINA DADA ILI WAENDELE KUTUNZA NDOA ZAO


You know who your friends are when you’re going through a relationship crisis. Maybe your husband is coming up to 40 and has started acting strangely; perhaps you’ve caught him texting another woman; or, worst of all, he’s threatening to leave you and break up the family.

Whatever the circumstances, it’s only being able to phone a friend or chat with the girls over a glass of wine that stops you from going round the bend.

According to Andrew G Marshall, after almost 30 years working as a marital therapist, he has become convinced that, while men don’t have enough friends or emotional support, women can have far too many and too much.

He says, “my heart sinks when a new female client tells me her ‘friends have been wonderful’ because time and time again, while she thinks they’ve been helping her save her relationship, they’ve been fanning the flames or even throwing petrol on the fire.”

FIVE STEPS TO SAVE YOUR MARRIAGE
1.    When you’re in a hole, stop digging. Under pressure, we tend to try the same failed strategy again and again. Even though we know pushing for an answer, getting angry or going silent doesn’t work, we imagine doing it one more time (but bigger, louder or for longer) will change things. It won’t.
2.    Stop playing tit for tat. He does something horrible and you match him. Soon it’s become a race to the bottom.
3.    Just for a second, put your feelings to one side and step in your partner’s shoes. How does your relationship look now and what would you like to do differently?
4.    Make a full apology. This is different from saying sorry. First, acknowledge any behaviour that you regret; next, identify how this might have made him feel, and then apologise. Please don’t explain why you acted as you did — that’s for another day — because it can sound like an excuse and lessen the power of your apology.
5.    Be the big one. If you love your husband — and if not, why are you spending hours talking about him to your girlfriends — do you love him enough to give without any expectation (in the short term) of getting anything back?

Credits: Andrew G. Marshall is a marital therapist and author of I Love You But I’m Not In Love With You: Seven Steps To Saving Your Relationship (Bloomsbury).


                                                 LOVE STORY

                     Mara nyingi tofauti nyingi sana hutokea katika uhusiano wetu, ziko zile tofauti ndogo ndogo ambazo mara nyingine hufukiwa na kutoongelewa, lakini ziko nyingine ambazo zaweza kuanza kama cheche na baadaye kuwa moto mkubwa na kuelekea kuathiri uhusiano wetu. Tofauti hizi mara kwa mara zaweza kuwa na faida au hasara katika uhusiano wetu. Zipo tofauti ambazo baada ya kuzishughulikia, wapenzi wemekuwa
na uhusiano imara zaidi ya awali na penzi lao limekuwa bora zaidi.

Lakini zipo tofauti ambazo baada ya kutokea tu, zimeua kabisa penzi na ukaribu uliokuwepo baina ya wapendanao. Wapo ambao hata tofauti kubwa ilipotokea na penzi baina yao lilikufa na wakagawanyika. Athari zote hizi hutegemea na jinsi wapendanao hao wanavyozitazama tofauti hizi na kuzishughulikia. Wengine wetu tumeshindwa katika uhusiano wetu kwa sababu tumeziangalia tofauti zetu katika mtazamo hasi, na kwa hiyo kila tofauti kwetu tunaiona ni mbaya.

Katika makala haya nataka tusaidiane jinsi ya kuzishughulikia tofauti baina yetu, na tujue nini cha kufanya, na nini sicho cha kufanya pale wapenzi au wanandoa wanapotofautiana.
Jifunzeni kujiwekea vigezo vitakavyolinda penzi lenu pale mnapotofautiana.

Kama tayari mna vigezo hivi basi jaribuni kuvizingatia kila mnapotofautiana, kwa mfano wapenzi wengi waliolewa wamejiwekea vigezo au masharti kwamba wakati wowote wa ugomvi au kutofautiana lazima kila mmoja akumbuke kuwa kutofautiana hakumaanishi kutokupendana. Wengine wamejiwekea kigezo kwamba, hata tofauti baina yetu iwe kubwa vipi, kuachana kamwe haitakuwa upenyo au suluhisho. Kila watu hawa wanapogombana akili zao zinakumbuka vigezo walivyojiwekea wenyewe.
Jitahidini kukaa mkiwa mmeangaliana (face to face)

Mnapo kaa mkiwa miili yenu imetazamana, mnatoa nafasi kwa macho yenu pia kutazamana, na hii inawezesha kutuma ujumbe kwamba wote mkotayari kusikilizana. Mmoja anapokwepesha macho anaonyesha kutokuwa tayari kumsikiliza mwenzake na hivyo kufanya zoezi la kutafuta suluhu kuwa gumu sana. Wapendanao wengine hushikana mikono yote miwili, kama alama ya kuonyesha kujaliana ingawa wanapitia katika fotauti nzito.

Wakati mwenzako anatafuta jitihada za kukushika mikono yako, jizuie usiseme maneno magumu au kuutupa mkono wa mwenzio, au kuondoka kwa hasira pale ulipokuwa umeketi. Kama unalazimika kutaka kuwapekeyako zaidi, tumia hekima kumwonyesha mwenzako kwamba una hitaji faragha zaidi ili akuruhusu na kukuachia huru.

Mawazo yenu na akili zenu zielekee tu katika malengo maalum mliyonayo katika kutofautiana kwenu.
Mara nyingi, katika kurushiana maneno, matusi, kurushiana vitu na hata kupigana ni rahisi kutoka nje ya malengo yenu. Jiulize, Je, ni nini kilitufanya tutofautiane? Mfano: Lengo lenu lilikuwa kujaribu kutafuta muda wa kupunguza kazi za maofisini ili walau mpate muda wenu binafsi. Au labda lengo lenu ni kujaribu kuangalia uwezekano wa kuharakisha mchakato wa harusi yenu.

Kwa nini Wapenzi Hugombana:

Mara mnapohama kwenye lengo lenu la awali ni rahisi kuibua ugomvi mwingine na hivyo badala ya kuuzima moto mkajikuta mnaupalia makaa. Kila wakati mnapoendelea na tafauti zenu, mjiulize, je, hiki ndicho kilichotufanya tutofautiane?
Jaribu kuziandika au kuyaandika Masuluhisho yote yanayowezekana.
Najua ziko njia nyingi ambazo mtazichagua za kuwasaidia kupunguza au kuondoa tofauti zenu nanjia hizo zaweza kufeli. Ushauri ni kwamba, njia zote mnazoziona kuwa zinaweza kuwa na msaada ziwekeni katika mtiririko maalum.

Mara nyingi hatua hii hufanywa wakati lile fukuto la ugomvi limepoa, na kila mmoja ameshaelewa sababu ya kutofautiana kwenu. Hapa sasa mzijadili njia zote mnazoona zitakuwa suluhisho bila kujali ugumu au urahisi wa utekelezaji wa njia hizo. Maoni mliyonayo katika utatuzi pia yawekeni katika karatasi pembeni pasipo kuyafanyia tathmini yoyote.
Jaribuni kuzitathmini njia zautatuzi mlizozipendekeza katika hatua ya nne.

Baada ya kuziandika njia zote zinazoonekana kuwa suluhisho la tofauti zenu, wote kwa pamoja muanze kuzitathmini njia hizo mkiangalia madhara au matokeo ya kila mmoja.
Baada ya kuangalia madhara au matokeo mtajikuta mmezipunguza njia hizo na kuwa chache sana, labda zaweza kufikia mbili au tatu au hata moja na kwahivyo sasa mwaweza kuona ile inayoweza kufanya kazi zaidi.
Chagua njia au suluhisho lililokubaliwa na wote.
                                                                

 

 

Sababu zinazo wapelekea wavulana huachana na msichana mmoja na kwenda kwa mwingine.

awahi kujiuliza kwanini unampenda mvulana kwa muda wote lakini yeye anakuacha na kwenda kwa mwingine? Japokuwa inauma lakini kuna sababu zanazopelekea.
Hizi zinaweza kuwa ni sababu.
Mvuto.
Nivigumu kutambua lakini namana navyo enda anaweza kuwa na mvuto zaidi yako, Na kwanmna yeyote ile huwezi kumlaumu yeye kwa hilo. Wavulana tunahitaji msichana atakaye tuvutia japokuwa furaha ya mvulana mmoja inaweza kuwa maumivu kwa msichana mmoja na mvulana mwingine.

Msichana ana muamini.
Msichana akitokea kumuamini sana mpenzi wako kuliko wewe unavyo muamini basio jiandae kulia. Kama umekuwa unasubiri mpenzi wako akienda bafuni unakagua simu yake na wakati mwingine akajuwa, basi atakapoona kuna mwingine ambaye hawezi kufanay hivo yeye atakuwa radhi kwenda kwa huyo.

Ana muheshimu.
Udhaifu wa wavulana wengi nipale anapo pewa hashima na mpenzi. Kwahiyo usishangae ikawa ni sababu ya yeye kukuacha na kwenda kwa mwanamke mwingine. Nisababu amepata anaye muheshimu.

Kuwa muwazi.
Namaanisha kuwa wasichana wengi wanshindwa kuwa wawazi kwa mpenzi wake. So a guy anapopata msichana ambaye ni muwazi basi itakuwa rahisi kwa yeye kwenda kujiridhisha naye.

Kujiamini.
Guyz huwa wanapenda msichana anaye jiamini na kujikubali. Kwa muonekano wake na kwa vile anavyofanya pasipo kuiga kwa yeyote. So inaweza ikawa ni moja ya sababu ya yeye kwenda kuko.


 HIVI NDINYO NILIVYO AMBUKIZWA UKIMWI NA MWANAMKE MSAGAJI

Zuwena ( sio jina lake halisi ), ni mwanamke wa kitanzania mwenye umri wa miaka 43. Kwa sasa mwanadada huyu anaishi na virusi vya ukimwi. Mwanadada huyu anabainisha namna, alivyo pata maambukizi ya v.v.u kw kujamiiana na mwanamke mwenzake, ama kwa lugha nyingine, Zuwena anaeleza namna ambavyo mwanamke msagaji alimuambukiza v.v.u wakati wakiwa na uhusiano wa jinsi moja... Fuatilia kisa hiki cha kufundisha na kusikitisha.



Nakumbuka ilikuwa mwezi wa kumi na mbili mwaka 2007, nilipata tenda ya u MC katika sherehe ya kumuaga binti wa jirani yangu kule Buza Cape Town. Sherehe hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa Mihogoni Pub kulekule Buza.

 
Saa moja usiku nilikuwa nimeshafika ukumbini na kutoa maelekezo kwa wageni waalikwa, watu walikuwa wengi kiasi ambacho hata mama mwenye sherehe alifurahi kwa jinsi watu walivyo muitikia. Kama kawaida niliendelea na matangazo ya hapa na pale, watu walicheza na kufurahi. Muda wa chakula ulipowadia nilikaa pembeni nikiwa naangalia watu wanavyo kwenda kuchukua chakula. Ghafla alitokea mama mmoja mtu mzima kwa kumkadiria alikuwa na miaka kama 48 – 50 hivi. Alinifata pale nilipokuwa nimesimama na kuanza kutoa sifa za hapa na pale mara umependeza , mara unaongea vizuri, mara vazi ulilovaa limekupendeza, mwisho aliniomba namba ya simu akaniambia kuwa ana sherehe ya kumuaga binti yake kwa hiyo angependa niwe MC katika shughuli yake. Kwa kweli mimi nilikuwa kazini, sikukataa kumpa namba yangu.
Kesho yake alinipigia simu ya kunisalimia, kwa kuwa kiumri alinizidi nilimuamkia, ila nilichokisikia masikioni mwangu ni neno “ Ahsante baby “. Nilishituka lakini nikaona ni vitu vya kawaida , kadri siku zilivyokwenda tulizidi kufahamiana nilimwambia kuwa nina saluni yangu, alinitumia vocha na mwisho alliniambia anataka kuja kupajua ofisini kwangu, nilimuelekeza akawa anakuja kutengeneza nywele, akitoa 10,000/= nikimrudishia chenji ananiambia “ utakunywa soda “ , siku nyingine anafika ofisini kwangu ananipa hela anaondoka. Nikaanza kuwa na mawazo juu ya huyu mama lakini sikupata jibu.
Siku moja akanipigia simu akaniambia anataka kufungua saluni yake, kwa hiyo angeomba tukutane Cape Town Bar tuongee mimi na yeye. Ilikuwa siku ya Jumapili, wateja walikuwa wengi alinisubiri kama saa moja akanipigia kuniulizia nimekwama wapi?
Nikamwambia bado nina wateja , akaniambia funga saluni njoo nikulipe hela ya siku hiyo yote. Nilifika pale akaniagizia kinywaji na baada ya hapo akatoa shilinge 50,000/= .
Nilishindwa kumuelewa huyu mama akaanza kunihoji naishi na nani, nikamwambia naishi
na watoto wangu watatu, baba yao baba yao amefariki miaka miwili iliyopita .
Nikamuuliza saluni anataka kufungulia wapi? Akanijibu achana kwanza na mambo na mambo hayo tutaongea baadaye . Tuliendelea kunywa hadi saa mbili usiku nikamwambia
nawawahi watoto wangu nyumbani akaniambia nitakupeleka na gari, kusema kweli sikuelewa nia yake ni nini hivyo hata nyumbani kwangu sikutaka apajue. Nilimuaga tena kwa mara ya pili akaniruhusu , kesho yake aliniletea viroba vya unga na mchele
akavishusha saluni kwangu, akaniambia atanipigia simu , kesho yake aliniletea viroba vya unga na mchele akabishusha saluni kwangu , akaniambia atanipigia simu kesho yake kuna kitu anataka kunieleza.
Nilianza kupata hofu, ilibidi niwaeleze rafiki zangu wa karibu , ushauri walionipa waliniambia usikubali kutoka naye kwenda popote mbali ya pale Buza kwa sababu nia
yake hatueielewi. Kesho yake akafika pale bar akanipigia simu, nikaenda ila nikapanga na rafiki yangu mmoja anifuate pale . Alipokuja nilitoa hela ili nimuagizie kinywaji, Yule
mama alinizuia akatoa hela na kumuambia muhudumu alete kinywaji ila alimuomba Yule rafiki yangu akae meza nyingine. Kusema kweli alizidi kunichanganya, sikumuelewa.
Yule rafiki yangu alikunywa bia ya kwanza na ya pili na akaja kutuaga akaondoka.
Nilimtumia meseji kuwa asicheze mbali.
Baada ya kama lisaa limoja hivi alipigiwa simu, akaniaga akatoa Sh. 10,000/= akanibusu akaondoka. Yaani hapo ndio alinifanya niwe na mawazo sana, nikaenda kuwahadithia wenzangu wengine wakasema labda ni msagaji, wengine wakasema ametokea kukupenda tu au anataka kaka yake akuoe.
Kesho yake akaja na dereva mwanamke, binti mdogo mwenye umri kati ya miaka 20 au 25, akaniambia nimsindikize mjini nikamchagulie nguo za biharusi mtarajiwa. Tukaondoka
wote hadi Kariakoo, akamwambia Yule dada apaki gari pembeni ili akajisaidie, Yule binti akajitambulisha kwangu kuwa anaitwa Angel, akaniuliza huyu mama mmeanza kufahamiana toka lini, nakamwambia yapata mwezi mmoja sasa. Nikamuuliza mbona
unaniuliza hivyo akaniambia nilikuwa nakuuliza tu. Akaniuliza unajishughulisha na nini , nikamwambia nina saluni na ni mc, akaniomba namba ya simu, Yule mama alipokuja akatuuliza mlikuwa mnaongea nini? Mimi nikamjibu kuwa dereva wako ananiuliza ile saluni ni yangu au nimeajiriwa ? Tukaja mpaka mtaa wa Tandamti akamwambia apaki gari atusubiri, tukaanza kuingia madukani, badala ya kutafuta nguo ya bi harusi akawa
ananiambia mimi nichague nguo niliyo ipenda nikawa namkatalia , tukaja mpaka mtaa wa Agrrey kuna duka linauzwa nguo za kutokea usiku, tukaingia pale kuna nguo nzuri tuliikuta inauzwa 120,000/= akaniambia niichukue nikakataa, tulipotoka nje kuna
kaka alikuwa anauza viatu simple akaniambia nichague nikaona nisimkatishe tama nikachagua naye akachagua , Mara ikaingia meseji kwenye simu yangu , meseji ilikuwa inasema hivi “ Huyo mama unamtambua vizuri au haumtambui, ni msagaji mzuri pole
Aunty nakuhurumia, “ by Angel . Kwa kweli nilishtuka nikahisi nazimia , akaniambia mbona umesoma sms ukaonekana
umeshtuka . Nikamwambia kaka yangu amenitumia sms mtoto wake anaumwa sana.
Akaniambia twende nikupeleke , akili yangu ilishahama, nilimuambia tu hapana acha niende nikapande daladala niwahi hospitali. Alitoa shilingi 10,000/= akanipa kama nauli,
nilitoka speed mithili ya mshale, nilivuka mtaa wa uhuru, nusu nigongwe na gari, sikuamini macho yangu, nilifungua tena ile sms nikaisoma , ghafla akanitumia vocha ya sh. 5000/= na ujumbe uliosema “ I love you baby “Nilipofika nyumbani nikawapigia rafiki zangu simu nikawaeleza, walishtuka sana, wengine
waliniambia namsingizia . Rafiki yangu Hawa akanishauri nibadilishe laini siku hiyo hiyo na pale saluni nisikae. Nikanunua laini mpya , nikaenda kutafuta kazi ya saluni Yombo
pale kwangu nikaweka msichana. Nikamwambia mtu yoyote akiniuliza amwambie nimesafiri na simu sina. 
Na kweli huyo mama alikuwa anakuja mara kwa mara saluni
kwangu kuniulizia , lakini hakupata mafanikio yoyote. Matokeo yake niliamua kuhama nikapangisha nyumba yangu nikahamia Tandika nyumbani kwetu. 
Nilicho hofia nikwamba kwa sababu nilishakula pesa yake nyingi, angefikia kunitaka kimapenzi, matokeo yake ningemkatalia angeweza kunifanyia chochote.


JE  KITU  GANI  KILITOKEA?, ILIKUWAJE  KUWAJE  HADI  ZUWENA  AKAKUBALI  KUINGIA  KATIKA  MAHUSIANO, NA  MWANAMKE  HUYU?, NINI  KILIPELEKEA  HADI  ZUWENA  KUAMBUKIZWA  V.V.U  NA  MWANAMKE  HUYU?  Endelea  kufuatilia  mfululizo  wa  makala hii itokayo kila JUMAPILI "

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates