Audio: Stereo awasikitikia wasanii wa hip hop Tanzania, adai aliuza album yake 'African Son' yenye nyimbo 19 kwa shilingi Milioni 1.5 tu

3:04 AM

Member wa zamani wa label ya M-Lab ambaye sasa hivi anafanya kazi chini ya Unit Entertainent ameonesha masikitiko yake kwa wasanii wanaofanya hip hop Tanzania kwa kudai kwamba hali ni ngumu na haiwafaidishi wengi hata kwa kiwango cha kawaida.
Mkali huyo aliyeacha alama mitaani kwa baadhi ya wasanii kuiga mitambao yake ‘Stereo flow’, amefunguka wakati akifanya mahojiano na Jabir Saleh aka Kuvichaka ama The Library/Maktaba.

NEW TRACK - NASH MC - NAANDIKA

3:01 AM

Mchenguaji anayewakilisha ngome ya Miraba Minne, Nash MC ameachia wimbo wake mpya alioupa jina la ‘Naandika’.
Wimbo umetayarishwa katika studio za Kali Nation na Jeysan Keyz. Mdundo wa wimbo huu ulikuwa wa Wasalu Muhammad Jaco aka Lupe Fiasco na mtayarishaji aliyeuandaa ni Needlz aliyeandaa midundo ya mastaa kibao akiwemo 50 Cent, The Game, Bruno Mars, Ludacris na wengine.
“Naandika kuhusu mitaa kwa hisani ya watu wa maskani, unaandika mapenzi hiyo ni kwa hisani ya radio flani. Kwa hisani ya promo mnarudi utumwani, haujui siri yeyote unaandika kwa hisani ya kusikika hewani.” Anarap Nash Mc kwenye wimbo huu.
 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates