TOP 10 YA WASANII WA BONGO FLAVA WALIOINGIZA HELA NYINGI 2013 4-Ommy Dimpoz

7:52 AM
Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa yupo kwenye ziara ya muziki nchini Marekani ameingiza fedha zake nyingi kupitia show alizofanya. Ziara zake za Ulaya na Marekani pekee zimemuingizia dola 50,000 ambazo ni sawa shilingi milioni 81. Tangu aachie wimbo wake mpya Tupogo,tayari Ommy ameshaingiza shilingi milioni 50.Kwenye show yake ya hivi karibuni ya Tupogo Night iliyofanyika Club Billicanas,Ommy alipeleka nyumbani shilingi milioni 10 baada ya kukata gharama zote.Watu 1,770 walihudhuria show hiyo. Show yake ya Burundi ya mwanzoni mwa mwezi uliopita ilimuingizia staa huyo shilingi milioni 30. Ommy hutoza si chini ya shilingi milioni 7 kwa show na kwa mwezi,amekuwa na uhakika wa kufanya show tatu ama nne za ndani bila kusahau show za Kili Music Tour. Hivi karibuni kwenye segment ya Tell it All ya Bongo5,Ommy alifunguka kuwa makampuni mengi yamekuwa yakimfuata kumpa endorsements lakini msimamo wake wa kutaka kulipwa fedha ya uhakika imemfanya azikatae nyingi lakini yupo mbioni kupata deal kubwa. Mpaka sasa Ommy anajenga nyumba mbili kwa mpigo zenye thamani ya shilingi milioni 250 hadi zilipofikia. Tayari ana viwanja vingine viwili anavyotaka kuangusha mijengo mingine.Hivi karibuni pia atakuja na clothing line yake ya PKP.

TOP 10 YA WASANII WA BONGO FLAVA WALIOINGIZA HELA NYINGI 2013 1-diamond platnumz

7:43 AM
Hakuna ubishi kuwa,mwaka 2013 Diamond Platnumz ndiye msanii aliyeingiza fedha nyingi zaidi.Pesa nyingi ya Diamond imetokana na malipo ya show zake za ndani na nje ya nchi.Kwa uhakika,mwaka huu pekee,Diamond amefanikiwa kuingiza takriban shilingi bilioni 1. Kwa show za ndani peke yake,Diamond hutoza si chini ya shilingi milioni 10 ama 15 na kila wiki hufanya show zaidi ya 2.Hivyo tangu mwaka uanze,Diamond amekuwa akiingiza shilingi milioni 40 kila wiki.Tour za nje alizofanya mwaka huu ni pamoja na zile za Uingereza ambako alifanya show kwenye miji mitatu,show ya Burundi na Congo,show mbili za Kenya (Nairobi na Mombasa),show ya nchini Comoro ambako alilipwa si chini ya dola 30,000 na show ya Malaysia wiki iliyopita. Kwa upande wa show za hapa nyumbani ambazo ni nyingi mno zisizo na idadi,ukiachana na zile za kawaida,Diamond aliingiza shilingi milioni 40 kwenye show 4 za Kili Music Tour ambapo kila show alilipwa shilingi milioni 10.Ndiye msanii aliyelipwa fedha nyingi zaidi kwenye ziara hiyo. Pia amefanya show kadhaa za Fiesta 2013,show za promotion za Tigo na makampuni mengine Tamasha la Matumaini,show ya Tulizana Tuko Wangapi ya Leaders Club,show yake na Nay wa Mitego (Dar Live na Maisha Club). Mwezi February 16 mwaka huu, Diamond alifanya show jijini Arusha ambayo kiingilio chake kilikuwa ni shilingi 150,000 ndani ya Club Safari na ukumbi kufurika. Miezi kadhaa iliyopita pia hitmaker huyo wa ‘Number 1’ ameshaalikiwa kwenye show corporate kuburudisha wafanyakazi wa benki na taasisi zingine pamoja na watu binafsi na zote hizo zimemuingizia fedha nyingi. Pamoja na show,Diamond amekuwa akiingiza fedha nyingi zaidi kwenye malipo ya ringtones ambapo kila baada ya miezi mitatu amekuwa akiingiza si chini ya shilingi milioni 20.Kwa mujibu wa Push Mobile,akaunti ya Diamond kwenye kampuni hiyo ndio inayoingiza fedha nyingi kuliko msanii mwingine yeyote wa Bongo Flava. Mkataba exclusive alioingia na kampuni ya simu ya Vodacom kuuza wimbo wake mpya My Number One kama muito wa simu, umezidi kumpandisha juu na ikidaiwa kuwa mkataba huo ni wa mamilioni ya shilingi. Ikumbukwe pia,Diamond ni balozi wa Cocacola. Mkataba huo ambao haijajulikana umemuingizia shilingi ngapi,lakini ni fedha inayoweza kuwa si chini ya shilingi milioni 100. Diamond ni miongoni mwa wasanii wengine 23 wa Afrika akiwemo Lady Jaydee kwenye mradi mkubwa wa Cocacola wa Coke Studio africa.

TOP 10 YA WASANII WA BONGO FLAVA WALIOINGIZA HELA NYINGI 2013

7:24 AM
#2-Lady Jay Dee Huwezi amini,vuguvugu la Anaconda limemsaidia Jaydee si tu kukusanya mashabiki wengi zaidi,bali pia limempa fedha nyingi mno.Zaidi ya tiketi 3,500 zilinunuliwa kwenye show yake ya mwezi June ya Miaka 13 ya Muziki na kuingiza takribani shilingi milioni 100.Haikuishia hapo,albam yake Nothing But The Truth ilinunuliwa kwa kiasi kikubwa na kumfanya kuwa msanii pekee wa Bongo Flava anayeendelea kufurahia mauzo ya albam zake. Hits zake mbili,Joto Hasira na Yahaya kutoka kwenye albam yake hiyo,zimebadilisha maisha yake na kumfanya kuwa mwanamuziki mwenye show nyingi zaidi pia.Lady Jaydee ametumbuiza kwenye karibu show zote za Kili Music Tour ambako ameingiza shilingi milioni 25. Mwaka huu pia Lady Jaydee amefanya show nyingi kubwa ikiwemo ile ya uzinduzi wa filamu ya Lulu,Foolish Age,show yake kwenye Miss Tanzania 2013,Family Day Show ya Arusha iliyofanyika Eid Pili,Anaconda Show iliyofanyika Triple A na nyingine iliyofanyika Snow View Hotel. Akiwa Arusha pia,Lady Jaydee aliuza kopi za albam yake kama njugu pamoja na tiketi za Anaconda zilizouzwa kwa shilingi 15,000 kila moja. June mwaka huu pia,Lady Jaydee alitumbuiza kwenye semina ya kuwezesha wanawake kuondokana na njaa na umaskini,iliyofanyika chini ya mfuko wa fursa sawa kwa wote chini ya mama Anna Mkapa. Biashara yake ya Nyumbani Lounge,imeendelea kufanya vizuri pia kwa kupata wateja wengi wanaoenda kupata chakula,vinywaji na burudani kutoka kwa bendi yake ya Machozi. Bado anaingiza fedha kupitia udhamini wa Airtel kwenye show yake ya TV ya Diary of Lady Jaydee. Msanii huyo ambaye jina lake ni Judith Wambura pia miongoni mwa wasanii 24 wa bara la Afrika waliochukuliwa kwenye mradi wa Coke Studio Africa wa kampuni ya Cocacola unaoendelea jijini Nairobi Kenya.

SIFA 15 ZINAZOFANYA MWANAMKE KUMPENDA MWANAMME

3:37 AM
Pengine watu wengi wamekuwa wakitafuta ni jinsi gani wanaweza kupendwa na wasichana au wanawake. Niwazi kabisa kila mwanamke anachaguo lake kwa mwanaume ampendae.Huenda ukawa unavigezo kibao lakini akapenda mweyevigezo vichache. Vifuatavyo ni vigezo 15 ambavyo wasichana wengi hupenda kutoka kwa mwanaume. 1. Kujiamini 2. Mcheshi 3. Mwenye utashi 4. Anayetoa msaada unapohitajika 5. Anaetunza siri 6. Mwenye kujithamini 7. Mwenye malengo / makini 8. Mwenye mawazo mapana 9. Muwazi na mkweli 10. Anayeridhika 11. Aliyeshupavu na jasiri 12. Mwenye huruma 13. Anaesamehe 14. Hadhi na heshima 15. Hisia ya uadilifu.

HAPPY BIRTHDAY COOL KAKA MAFIAN RAPPER

2:59 AM

PICTURES HIVI NDIVYO JENGO LA WESTGATE LILIVYOPOROMOKA

2:51 AM
Westgate
Kupomomoka kwa jengo la ghorofa tatu ndani ya Westgate Mall baada ya mlipuko uliosababisha vifo vya magaidi wa 5 na na wengine 11 kushikiliwa na Polisi siku ya Jumamtatu Sept 23, 2013 kama unavyoonekana katika picha magari yaliyokua yameegeshwa juu ya paa la magesho ya magari yakiwa yameanguka chini kwa mlipuko huo.

BONYEZA HAPA KUPATA ALBUM YA RAMA DEE-THE BEST OF RAMA DEE (2000-2013)

2:48 AM
Biography
Born 3rd July 1983, Rama Dee started his career in 2001 with the hit Tomorrow. Since then he has built a successful career and released 2 albums, Kutoka Moyoni and Chini ya Uvungu wa Moyo Wangu.
He won KILI MUSIC AWARDS in category of  BEST RnB SONG OF THE YEAR 2013,song namely KUWA NA SUBIRA.
Genre;Rn'B
Hometown;Dar es-saalam
Record Label; Independent
General Manager; Self Managed
Influences; John Legend, Anthony Hamilton, R Kelly

VIDEO YA MAELEZO JINSI ALL SHABAAB WALIVYO JIPANGA KABLA YA UVAMIZI WESTGAT

2:33 AM

Na Heshimu Kazi Za Kendrick Lamar Ila Kanye West Ndio Mpinzani Wangu Mkubwa, Asema Rapa Huyu Wa Young Money

2:06 AM
Rapper Drake hivi karibuni ameka chini na kuongelea mambo tofauti kuhusu mziki wake na kusema tayari ana mpango mkubwa wakufanya kazi na kundi lenye heshima kwenye Hiphop game duniani Wu-Tang Clan. Kwenye mahojiano kuhusu ujio wa cd yake mpya ya Nothing Was The Same Drake amesema wimbo wake wa Wu Tanf Forever umepokelewa vizuri sana na ninafasi yake kufanya kazi na wakongwe hao
 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates