Keko amzingua Linex?

9:43 AM
Kufuatia maswali mengi ya mashabiki wa muziki kuhusiana na kinachoendelea baada ya Msanii Linex hapo awali kutangaza kufanya kolabo na msanii mkubwa wa Uganda Keko, jambo ambalo halijafanyika, Linex ameongea na eNewz kufafanua juu ya mchongo huu.
 
Linex ameweka wazi kuwa, ratiba ya kwake pamoja na ya Keko ambazo zimekuwa na mambo mengi ndiyo kikwazo kikubwa ambacho kimefanya mchongo huu kuwa haujakamilika mpaka hivi sasa.
 
Msanii huyu ameeleza zaidi kuwa, Amekwishafanya jitihada za mara kwa mara kuwasiliana na Keko kumuuliza amefikia wapi na kukamilisha kipande chake kilichobakia ambapo kutokana na mambo mengi, Msanii huyu kutoka Uganda bado hajaweza kufanya kipande chake.
 
Linex amesema kuwa kwa sasa ameamua kutulia hadi msanii huyu wa Uganda atakapoamua kumalizia sehemu yake mwenyewe kwasababu kolabo hii inaumuhimu kwa pande zote mbili kwa kuwa yeye kama Linex ni msanii mkubwa hapa Tanzania, na Keko ni mkubwa kwa upande wa Uganda.
 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates