KAMA WE NI DJ MKALI HII INA KUHUSU

12:36 PM
Kama ulikosa awamu ya kwanza sasa ni wakati wako

MAAJABU MAZISHI YA BAB'KE JOYCE KIRIA

2:05 AM
MAAJABU yameibuka kwenye mazishi ya baba mzazi wa Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa hewani na  Televisheni ya  East Africa, Joyce Kiria, Michael Francis Iwambo Kiria kufuatia kuchimbwa kwa makaburi mawili, Amani lina mkasa mzima.
 
Kondoo akichinjwa.
Tukio hilo la ajabu lilitokea kwenye msiba wa mzee huyo, Kata ya Kibosho, Kijiji cha Dakau, mkoani Kilimanjaro wakati wa maandalizi ya kuuhifadhi mwili wa merehemu huyo.

MASISTER BANDIA WAKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA

1:44 AM

Wanawake watatu wamekamatwa kwa madai ya kujaribu kusafirisha dawa za kulevya kupitia uwanja wa ndege wakiwa wamevalia kama masista.
Wasafirishaji hao walisimamishwa wakati wakiwasili kwenye kituo maarufu cha mapumziko nchini Colombia, sababu polisi walifikiri kwamba mavazi yao hayakuwa yakionekana halisia.
Maofisa waligundua kwamba kila mwanamke kati yao alikuwa na zaidi ya kilo 4 za cocaine zikiwa zimefungwa katika miguu yake.
Wakiwaongezea fedheha katika mashitaka, wasafirishaji hao walipangwa mstari mbele ya waandishi wakiwa bado wamevalia mavazi yao ya kituko kuficha ukweli.
Wanawake hao watatu, wenye umri wa miaka 20, 32 na 37, walitua kwa ndege kwenye kisiwa hicho cha San Andres kutoka Bogota siku ya Jumamosi asubuhi.
Kapteni wa Polisi Oscar Davila alisema wanawake hao walionekana kama wamechanganyikiwa, na kuongeza kwamba mfumo wa tabia zao haukuonekana kuwa sahihi.


Pale masista hao bandia waliposimamishwa na kupekuliwa, walikutwa wakiwa na shehena kubwa ya cocaine ikiwa imefungwa katika miili yao.

Wote watatu waliangua kilio na kusisitiza kwamba walitumiwa tu kusafirisha dawa hizo sababu ya matatizo yao ya kifedha, alisema Davila.

Wanawake hao walikamatwa na kuswekwa rumande kwa mashitaka ya kusafirisha dawa za kulevya.

Dawa hizo zilikadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Marekani 35,000 mtaani, kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi wa mji huo, Jorge Gomez.

"Hawakuwa wafuasi halisi wa dini, hawakuwa masista," alisema. "Kinyume cha hilo, walikuwa wakitumia mwanya huo kwa ajili ya kazi hii.
"
San Andres, iliyoko Caribbean nje ya ufukwe wa Nicaragua, ni moja ya mahali maarufu kabisa nchini Colombia kwa ajili ya wakazi na watalii.

Hatahivyo, inatumika pia kama njia kuu ya kupitishia dawa za kulevya kwa ajili ya kusafirisha cocaine kati ya Colombia bara na Amerika ya Kati

ISMAIL WA KICHEFU CHEFU ALELEZEA MIPANGO YAKE BAADA YA KUJITOA KWENYE KUNDI LA WAVANILLA

1:42 AM
 SAUTI TAMU ni project yangu mpya ambayo itaweza kuleta mabadiliko yanayoanza kutokea katika music , project hii itakuwa na member wasiozidi watano , orodha hyo MSANII ni Peke yangu (smile), WASOMI Ambao ni washauri wangu Watatu 3 ,Pamoja na manegemant yangu .. Kwa hyo naomba suport zenu wananchi ili 2weze kufikia sehemu nzuri kama walizofikia wenze2 .nawapenda sana AHSANTENI SANA.

HIVI NDIVO FACEBOOK WANAVYOPATA PESA KUPITIA KWAKO

12:12 AM
 




Kuwa na Akaunti ya Facebook ni kwa manufaa yako na manufaa ya Facebook

Facebook ambayo kwa sasa inapatikana katika lugha 70 ulimwenguni, ni mtandao wa jamii ambao unaongoza kwa kuwa na watumiaji wengi zaidi duniani. Wewe na mie kama watumiaji wa Facebook tunainufaisha kampuni hiyo ya Facebook, kwani kupitia kuitumia kwetu kunaiwezesha Facebook kuingiza mapato kwa njia ya moja kwa moja au nyingine.
Makala hii inakuchambulia namna ambavyo Facebook inaingiza "vijisenti" vyake:-
1. Kupitia Matangazo: Kwakuwa inao watumiaji wa mtandao wengi, ni rahisi kwa Facebook kushawishi watu binafsi na makampuni kutangaza bidhaa zao kupitia aina mbalimbali za matangazo yanayorushwa hewani na Facebook. Mfano , kampuni inaweza kudhamini POST yake, ili ionekane kwa watu wengi zaidi na mara nyingi. Pia kuna matangazo ya biashara ambapo unaweza kutengeneza tangazo lako la biashara na kulirusha hewani kupitia Ukurasa wako wa Facebook (Facebook Page).  Ili kutengeneza tangazo Facebook, unaweza kuenda sehemu maalum ukiwa Facebook imeandika 
CREATE AN AD.Unahitaji kuwa na Credit Card au Umejisajili na unayo akaunti ya Paypal ili kuweza kulipia huduma hii.
Mfano wa Matangazo yanayoipatia fedha facebook
 
2. Salio maalum la Facebook ( Facebook Credit)
Ni kama vile unavyonunua salio la simu yako ili utumie salio hilo kupiga simu, ila kwa Facebook, unaponunua Facebook Credit, ni kwa ajili ya kuweza kutumia credit hiyo kulipia kucheza Games, au hata kununua vitu katika baadhi ya maduka yanayouza bidhaa zao ndani ya Facebook.
Unahitaji kuwa na Credit Card au Umejisajili na unayo akaunti ya Paypal ili kuweza kununua Facebook Credit.

3. Kupitia Kuuza bidhaa mbalimbali
Facebook inayo huduma ya kuuza bidhaa mbalimbali kwa mtindo wa "Gift" ambapo wewe mtumiaji unachagua nani unataka kumnunulia bidhaa , kisha unaenda kwa profile ya huyo unayetaka kumuuzia bidhaa. Utaona sehemu imeandikwa GIVE GIFT, ukibofya hapo utakutana na aina mbalimbali za zawadi na maelekezo. Hata hivyo huduma hii ya kutoa zawadi kwa watu haipataki kwa kila nchi. Inabidi ucheki Profile ya mtu husika unayetaka kumpa zawadi kuona kama GIVE GIFT ipo katika profile yake.
 
 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates