VIDEO - P-UNIT- MOBIMBA

8:46 AM

COMING SOON....!!!!!

8:27 AM

VIDEO - JAGUAR - KIPEPEO

8:24 AM

CHECK PICTURES ZA MAANDALIZI YA ZANZIBAR FASHION WEEK 2013

7:44 AM





BAADA YA KUJITOA KATIKA KUNDI LA PAH ONE AIKA NAH REAL NA WEESTAR WAJA NA KUNDI JIPYA

7:30 AM
Kama unakumbuka vizuri mwaka jana kundi jipya lilokuwa linakuja vizuri kwenye game ,Pah one, lilisambaratika na wengine kujitoa kwa sababu ya kutokuelewana katika kundi, kisa kikiwa ni uhusiano wa kimapenzi kati ya Nahreel na Aika ambapo yeye "Aika" alikanusha kuwa sababu ya kundi hilo kuvunjika, sasa wameamua kuja na kundi lao jipya likiwa na Nahreel, Aika na Weester, ambalo hawajasema litakuwa linaitwa nini,na tayari wako mbioni kuachia single yao ya kwanza kama kundi jipya ikiwa inajina "Hold Me Back"

LADY JAYDEE KUWAUMBUA LINAH NA BARNABA, HII NDO NJIA ATAYOTUMIA

7:23 AM
Kumekuwa na kupishana/vutanikuvute kati ya LadyJay Dee na wasanii wa THT Linah na Barnaba kuhusu wasanii hao kuwepo ama kutokuwepo kwenye show ya Jide May 31, hata hivyo Lina na Barnaba walithibitisha kuwa watakuwepo kwenye tamasha la miaka 13 ya Lady JayDee licha ya kuwa kwenye posters za show hiyo.


Leotainmenttz imeamua kufuatilia kiundani kupata maelezo ya pande mbili, kwa upande wa Barnaba na Linah wao walithibisha kupitia mtandao wa
Bongo5 kuwa hawatahudhuria kwa sababu zifuatazo:

Linah: Dada yetu alituita akatuambia ana kazi yake ya kutimiza miaka 13 kwa hiyo anahitaji wasanii ambao watamsupport kwa ajili ya kufanya show. Sisi tulifuata protocol zote kwa sababu kama wasanii tuna viongozi, tukafuata protocol zote kuweza kukubaliana nae mpaka tukafikia hatua kwenye maswala ya biashara, yaani malipo. Kwenye upande huo kidogo tukawa tumepishana kwenye masuala ya maslahi. Lakini sasa tunashangaa yeye kuanza kuweka posters na nini. Yaani tumeshafikia makubaliano kwamba kulingana na maslahi haiwezekani.

Barnaba: Hatukushindwana, lakini unafahamu kila mwanasanaa, wale wote wanaofuata utaratibu wa sanaa wanakuwa wanamanejimenti zao na wanakuwa na matakwa ya ofisi zao. Kwa hiyo swala ni dadisi na ni refu na kazi limeletwa kwenye mdahalo…hata hivyo kulikuwa na booking ya kazi nyingine zilizokuwepo. Kwa hiyo mwisho wa siku imeonekana haitawezekana kwa sababu kuna kazi nyingine zimeshabukiwa. Tofauti zetu zilikuwa pale ambapo unaenda kuzungumza na mtu wakati hauna uhakika kama atakuwepo ama hayupo. Kwa hiyo hakuna tulichoshindwana bali ofisi/management ilikuwa na kazi tayari na makubaliano yetu yalikuwa hapo kwamba hatutoweza kuwepo kutokana na makubaliano ambayo yako kwenye ofisi na ofisi.”

Barnaba alisisitiza kuwa wao hawatakuwepo na kwamba hawana kabisa ogomvi na Lady JayDee na wanaongea vizuri tu.

Kwa upande wa Lady JayDee leotainmenttz imekuwa ikifuatilia tweets zake zinazoendana na kuwepo kwa Barnaba na Linah kwenye kipindi cha Diary ya LadyJayDee kinachorushwa na EATV. Na hii  ni baada ya TID kuwepo kwenye kipindi hicho wiki iliyopita na kuzungumzia kuwepo kwake kwenye show ya Miaka 13 ya Lady JayDee Nyumbani Lounge. 

Tweet za Jide kuanzia jumapili iliyopita zilisisitiza kuwa angekuwepo TID kwenye kipindi hicho, lakini kipindi cha jumapili hii kitakuwa kitamu zaidi kwa sababu atakuwepo Linah na Barnaba. Kama ni kweli watakuwepo, je wasanii hao wataelezea kuwepo katika show ya Jide kama alivyofanya TID? Tunapata mashaka kuwa inawezekana kutokana na tweet za Jide.

Tweet zake nyingine hazitaji majina ya wasanii hao lakini zinataja siku na kuonesha kuwa labda watakana hata wakionekana kwenye TV, akitoa mfano wa style ambayo aliitumia Shaggy kumshauri mwenzake Ricardo RikRok aliyefumaniwa katika wimbo kukana na kusema hakuwa yeye “It wasn’t me”, hata kama alinaswa kwenye camera.


Hizi ni baadhi ya Tweets za LadyJadee: 
Kwa kuwa ni kitu cha kuonekana kwenye TV tusubiri tushuhudie nini kitaonekana kwenye Dairy ya Lady JayDee jumapili hii saa tatu kamili EATV.

Agness Masogange Video Queen AFUNGUKA kuhusu yote yanayozungumzwa juu yake

7:14 AM
 
Haya yalikuwa ni maongezi yake na mtandao wa teentz.
Anaweza kuwa ndiye video queen hot&sexy zaidi Bongo na ingawa ameshiriki on two videos pekee anabaki kuwa V,queen mwenye jina kubwa zaidi. Siku za karibuni amekuwa akimake headlines on social networks pia magazeti baada ya video na picha zake chafu kusambaa on
social networks,TEENTZ imefanya nae Exclusive interview na kuongea ya moyoni kuhusu yote yanayozungumzwa kumhusu.

''Me cjui hizo picha zilisambaa vipi sababu izo picha zilikuwepo kwenye camera yangu na mimi cku hiyo nilikuwa nimelewa, i was drunk sikuwa naelewa chochote na nilikuwa south Africa kwa hiyo maswala ya kuandika habari za uongo eti nimeenda south kuuza ,me sina dhiki ya kufikia kuuza mwili wangu eti nipate pesa"na ,picha niliyopiga siyo ya uchi ile hata nikikuonesha,nilikuwa nimevaa nguo kabisa ,kuna uchi nimeonesha pale?

Na mtu kuenda South ndio ameenda kujiuza?Mimi nina biashara zangu nafanya na wanaosema hivyo hawanisaidii chochote,hakuna mtanzania anayeninunulia nguo,hayupo anayenipa pesa waongee tu''
Katika hatua nyingine Agness aliyashutumu baadhi ya magazeti nchini kwa kile aklichokiita wanaandika story zisizokuwa na ukweli

"Unajua sisi wadada tuna tabia ya kuoneana wivu akiona unafanya vizuri anaanza kukusemea vitu vya ajabu pembeni,Magazeti ya Bongo nayo ,wanaandika tu vitu vya kusikia pasipokuwa na uhakika na wanachokiandika nilisoma gazeti eti Wema ana mabaka,sijui Lulu amekonda ameisha,Wema alivyo mzuri vile?Lulu mwenyewe umemwona,amekonda yule?wanaandika tu imradi wauze"

Lakini pia alizungumzia uhusiano wake na mwanadada Sintah ambae awali ilitajwa kuwa wan beef lililotokana na kuvuja kwa video chafu ya Masogange.....

"Ugonvi wetu ulishaisha ,Simchukii Sintah na sitoweza kumchukia kwanza ni mkubwa kwangu yule,me niwa 1989 tu jamani,na watu hawajui me ni mpole na sipendi kugombana na watu magazeti tu wananijengea sifa mbaya"
Kuhusu ushiriki wake katika video as video queen,Agness alifunguka kuwa hatoshiriki tena kwenye video yoyote coz mchumba wake hapendi na amemzuia.

"nimeonekana kwenye Masogange ya Belle9 na Magube gube,sitoshiriki tena kwenye video za bongo Fleva sababu mchumba wangu amenizuia na hapendi kwanza"
Na hili likawa ndio neno lake kwa watanzania
"Agnes wa saivi siyo yule wa zamani nimeshabadilika jamani,me nimchumba wa mtu,nuimeshachumbiwa n soon naolewa" .alimalizia mwanadada Agness

source.teentz.com

TILALILA UK TOUR WITH MR BLUE, SULTAN KING AND NAJ.

7:07 AM


THE BIGGEST SHOW with THE BIGGEST DJZ

6:48 AM
 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates