NEW TRACK: SPIDER - SIO MAPENZI

12:49 PM

Noise Maker kwa DX ni kituo muhimu cha Roma akiwa Arusha, asema anapenda kufanya kazi na wasanii wa A.City.

12:31 PM

Wengi waliousikia wimbo wa Roma wa 2030 walipata hisia kuwa kulikuwa na punch kwa A.City artists Over Tanga ambapo ndo sehemu anakotokea, ama waliposikia mistari kwenye mashairi ya wimbo wake mmoja akisema 'Hip Hop ina uwanja mpana usiseme tu iko R-Chuga'. Kama wewe ni mmoja wao utakuwa unakosea hivi na inabidi umsome tena Roma.
Kupitia ukurasa wake wa facebook ROMA ameonesha kuwa mara nyingi anapokuwa Arusha hupenda kupiga collabo na wasanii wa pande hizo, na kazi zote zinapikwa pale Noise Maker na producer DX, na moja kati ya ngoma zilizopikwa hapo inaitwa 'Ukweli' akiwa na Banx na Mo Plus.Kwa hali hiyo booth ya Noise Maker ni kituo muhimu sana kwa mshindi huyo wa tuzo ya mwana Hip Hop bora.
Hivi ndivyo alivyosema Roma kupitia ukurasa wake wa facebook na kuambatanisha na picha akiwa na Mo Plus na Banx Baba la Ukoo.
"KILA NIENDAPO ARUSHA (ARACHUGA)!!! HUPENDA KUFANYA NGOMA NA MANINJA WA KULE!! DX HUSIMAMIA MIZIGO YOTE HII
with ma ninja BAAAANXXXX na MO PLUS BABA LA UKOO
NGOMA INAITWA "UKWELI"
A.city "

R.O.M.A (Rhymes Of Magic Atraction) ndivyo anavyojiita na kulitafsiri jina lake, kila akitoa wimbo mashairi yake huwa na nguvu ya ajabu kuvuta attention ya wasikilizaji wake kitu ambacho kimesababisha watu wengi kuvutika na kununua wimbo wake 2030 kwa shillingi 3000 kwa njia ya email, lakini pia baada ya kuuachia tu uliongoza kwa kupakuliwa kwenye mtandao kwa hapa Tanzania.

VIDEO: TAYGA FT RICK ROSS - DOPE

12:28 PM

New Video: Rick Ross aachia video ya wimbo wake aliyoi-direct mwenyewe "Pirates

12:22 PM


Big boss wa Maybach Music Group Rick Ross ameachia video ya wimbo wake 'Pirates', uliopo kwenye album yake ambayo ilikuwa nominated kwenye tuzo za Grammy "God Forgives, I Dont".

Rick Ross mwenyewe ameshiriki katika kuiongoza video hiyo kama co-director akishirikiana na muongozaji maarufu wa video Dre Film ambae ni mshika kamera wa Maybach Music Group. Video imefanyika Miami, Florida ikiwa na story nzuri.

Iangalie hapa:
                 

Justin Bieber hajapenda mama yake kufanya project ya filamu ya kupinga utoaji mimba.

12:10 PM

Siku chache baada ya mama mzazi wa mkali wa pop na R&B Justin Bieber kutangaza kuwa anatengeneza filamu fupi ya kupinga utoaji mimba (anti-arbotion), inasemekana kuwa Justin Bieber hajapenda project hiyo mpya ya mama yake.


Kwa mujibu wa Chicago Sun Times, mwimbaji huyo mwenye umri mdogo hajapenda project hiyo kwa sababu imebeba mambo ya kisiasa.
Mtu wa karibu wa Biebs aliliambia Chicago Sun Times kuwa Justin hapendi mambo ya kisiasa kama utoaji mimba ambao kwa upande wa Marekani ni issue nzito sana iliyojaa siasa. Chanzo hicho kilisema kuwa Biebs ameegemea zaidi katika kuwaburudisha fans wake na havutiwi kabisa na agenda za kisiasa. Amesema amechoshwa na kukutana na vichwa vya habari ambavyo ni vinahabari mbaya zinazomhusu yeye.

Mama yake Bieber Pattie Mallette alitangaza hivi karibuni kuja na project mpya ya filamu inayoitwa "Crescendo" inayopinga utoaji mimba, akiwa na lengo la kuwahamasisha vijana kufahamu kwamba kuna sehemu ya kwenda ambapo watu watawatunza na sehemu ya kuishi kama watapata ujauzito na wakaona hawana sehemu ya kuegemea.


Crescendo inatarajiwa kuoneshwa kwa mara ya kwanza february 28,na waandaaji wa filamu hiyo wamepanga kukusanya pesa kiasi cha $10 million kwa ajili ya vituo vya kuwahudumia wajawazito.

NEW TRACK: FAN KISS _ LADIES SWAGZ

11:33 AM
 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates