Angalia Trailer ya Movie inayohusu machafuko yaliyotokea Kenya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, inaitwa "Something Necessary"

5:30 AM



Miaka kadhaa imepita baada ya Kenya kukumbwa na balaa la machafuko yaliyopelekea vifo vingi vya watu, majeraha ya kudumu na watu wengi kukosa makazi yao baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 (post election violence). Wasanii wa maigizo nchini humo wameshafanya filamu inayohusu matukio yaliyotokea wakati huo na filamu inaitwa "Something Necessary".

Katika filamu hiyo wamemtumia character mmoja mwanamke aitwae Anne ambae anaonesha maisha yake yalivyokuwa baada ya machafuko yaliyoivuruga nchi hiyo mwaka 2007, Anne ni mwanamke anaehangaika kuyarudisha maisha yake aliyokuwa nayo kabla ya machafuko hayo, akijaribu kupambana kwa ajili ya afya ya mtoto wake wa kiume, alipompoteza mumewe, na shamba lake.

Lakini pia yumo character mwenye jina la Joseph, yeye ni gang member aliyehusika katika machafuko hayo, lakini wote Joseph na Anne wanajikuta wakiwa katika wakati mgumu wakitafuta jinsi ya kuzifuta kumbukumbu hizo mbaya na kuendelea na maisha yao ya kawaida.
 
 
 
 
 
Iangalie trailer yake hapa, "Something Necessary"...



Hii ni kati ya mistari ya Stamina iliyomkuna Roma kwenye 'Wazo la Leo'

5:24 AM

Mkali wa michano na ngoma zenye maisha marefu Roma Mkatoliki toka Tanga ameonesha kuwa ameusikiliza kwa makini na kuuelewa wimbo mpya wa Stamina 'Wazo la Leo' aliomshikirisha Fid Q, na kuchagua kuiandika tena kwenye ukurasa wake wa facebook mistari inayopatikana kwenye verse ya pili ya ngoma hiyo.

Roma ameandika status yenye mistari hii,

 "bora uitwe mfalme juha kwenye utawala wa kishamba
mapenzi yakikusumbua tafuta daktari wa KITANGA
#STAMINA# tisha shoro bwenzi!!!

Mistari hii ipo kwenye verse ya pili na ni mstari wa tatu na wa nne. Jinsi Stamina alivyoitaja Tanga itakuwa imemgusa Roma ambae sasa hivi yuko mitaa yake ya home Tanga, japo naamini ameguswa na mistari mingine pia au hata wimbo mzima. 

Roma ni msanii ni kati ya wasanii ambao mara kwa mara wamekuwa akitumia wall zao kuwasapoti baadhi ya wananii wa bongo anaowakubali, mwaka jana ilipodondondoka Dear God ya Kala Jeremiah alimpa shavu kwenye ukurasa wake wa facebook kuwa watu wakamwambie kuwa amemuelewa.

Anyways, ilikuwa ni maandishi ya appreciation kupitia public coz watu wangesema kama vipi angempigia hata simu amwambie mwenyewe,ila hii ilikuwa inaambatana na sapoti yake kwa Kala kupitia fans wake pia.
Hivi karibuni Roma aliachia wimbo wake mpya "2013" na uliongoza kwa kuwa downloaded kwenye mitandao mbalimbali na unaendelea kufanya vizuri.

Nas augua ghafla ashindwa kutokea kwenye show, alilazwa kwenye chumba cha dharura Hospitalini

5:18 AM

Rapper mkongwe Nasir bin Olu Dara Jones a.k.a Nas alishindwa kuhudhuria jana kwenye show yake ambayo ilikuwa inarushwa live kwenye kituo kimoja cha television kinachorusha show maarufu "Live with Kelly and Michael!"

Nas kupitia account yake ya tweeter aliwa-update fans wake kuhusu hali yake ya afya kuwa ilimbidi akimbie kwenda hospitalini muda huo na kuwaomba radhi kwa kutoonekana kwenye show.

Tweet yake ya january 11 inasomeka hivi, "Peace y'all. I'm out of the ER & doin alright. I'm on bed rest for a few. Apologies to everyone @ Live w/ Kelly & Michael. I'll make it up.."
Japokuwa 'hate me now' hit maker hakusema alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa aina gani, baadhi ya blogs za Marekani ziliandika kuwa alikuwa anasumbuliwa na Flu, na kwa mujibu wa 'The YBF' watu wa karibu wa Nas walimwambia mtangazaji msaidizi wa television show ya "Live With Kelly & Michael" kuwa Nas alikuwa na Stomach flu.

ALLEX CHATTA ATUA DYNAMIC RECORDS ZANZIBAR

5:14 AM

 Producer Allex chata toka mji kasoro bahari (morogoro) ametua kisiwa zanzibar akiwa chini ya Uongozi wa Dynamic records, akiongea na chiwileinc Allex amesema kua hii ni safari ya kikazi na amejipanga kuleta mapinduzi kwenye mziki wa zanzibar bila kujari ni haina gani ya mziki ambayo Artst watakuja nayo "nimekuja ki kazi brother muhim ni wasanii kunipa ushirikiano sababu msanii anapokua bora ni rahisi hata mimi kufanya kazi bora" alimaliza Allex 



 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates