NEY WA MITEGO NAE MATATANI BASATA

11:02 AM



 MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ney wa Mitego, yupo kwenye hatihati ya kufungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) baada ya kuachia remix ya wimbo wake wa Nasema Nao iliyojaa matusi na maneno makali dhidi ya wasanii wenzake na watu mbalimbali, Showbiz inakujuza.
Kwa mujibu wa afisa mmoja wa Basata aliyeomba hifadhi ya jina lake kwani si msemaji rasmi, katika wimbo huo ulioanza kusikika mwishoni mwa wiki iliyopita, Ney wa Mitego ametumia lugha ya matusi na maneno yasiyo ya kistaarabu, huku akiwataja kwa majina watu aliowalenga, jambo ambalo ni kinyume na sheria za baraza hilo.
 Baada ya kupata nyepesi hizo kutoka Basata, Showbiz ilimtafuta Ney wa Mitego ambaye alisema kuwa wimbo huo wa Nasema Nao Remix umevujishwa na watu asiowatambua bila idhini yake lakini akaeleza kuwa hajapokea taarifa yoyote kutoka Basata juu ya kufungiwa.

CHEKI PICHA ZA KIKOSI CHA YANGA KIKIWA KINAONDOKA KWENDA UTURUKI

10:59 AM
 
Domayo & Msuva
Nizar Khalfani akiwa uwanja wa ndege

wachezaji wakisubirai muda wa ukaguzi
David Luhendee na Said Bahanuzi 
Nadir Haroub na Baraka Kizuguto
Kocha Mkuu Ernest Brandts akiwa na mjumbe wa kamatai ya utendaji ambaye pia ni mkuu wa msafara Mohamed Nyenge
 


 Ladislaus Mbogo akiwa na Nadir Haroub Canavaro Uwanja wa Ndege JK Nyerere
 —


Meneja wa timu Hafidh Saleh
 — in Dar es Salam.
Viongozi wa Yanga wakiwa uwanja wa ndege

FUNGA MWAKA....2012 NI BONGE LA SHOW

10:47 AM
FUNGA MWAKA 2012 NI BONGE LA SHOW TANZANIA wakal kibao kwenye jukwaa ROMA,SUMA LEE,STAMINA,MOMBA,YAKUZA MOBB,JUMA NATURE,BARNABA,MAKOMANDO,ALONAME,CHIBWA,ROBBY,DULLAYO,FAN KISS.KIINGILIO 7000TU.CHAKULA VINYWAJI POOL TABLE,MPIRA WA MIGUU MCHANGANI,BURUDANI KIBAO

NEW TRACK; BEBEE FT SHAREEZY SULTAN KING & LANGA, TUNAWEZA

6:42 AM

New Track; Joh Makini ft. Dunga - Sijutii

6:33 AM

Producer Baucha awashauri producers kwenda shule, amepanga kuingia mikoani kuibua vipaji 2013..asema Baucha rec. ndiyo inachaji bei ndogo kuliko......!!

6:17 AM

Producer mkongwe ambae alitisha miaka flani na ngoma alizofanya kama 'Fid Q.com' na 'Usiulize' anayejulikana kama Baucha wa Baucha Records ameelezea vitu ambavyo vimebadilika hivi sasa katika game hasa kwa upande wa utayarishaji wa muziki ukilinganisha na enzi zile walipokuwa wao ndo wana-run the game.

katika interview aliyofanya hivi karibuni na josefly wa radio victoria fm ya Musoma, Baucha alifunguka kuwa kati ya vitu ambavyo anaona havikuwa sawa na hadi sasa haviko sawa katika tasnia ya utayarishaji ni kwamba baadhi ya watu walikuwa wanaingia tu kwenye tasnia hii bila hata kupata elimu hasa ambayo itawasaidia kufanya kazi kwa kiwango kinachostahili. Lakini pia Serikali haikuwa na sapoti na kuutambua muziki kama biashara, ila ilikuwa inajulikana kama sehemu ya burudani tu,
Alipoulizwa sababu maoni yake kwa watayarishaji wa muziki ambao wanajifunza kwa kutumia utundu wao tu lakini hawakusomea maswala ya utayarishaji wa muziki.
"Nawashauri kwamba tuingie sana kwa sababu tasnia ya sanaa sasa hivi lazima na elimu iwemo, lazima tuwe na elimu, sasa kwa wale ambao hawakusoma labda sasa hizi waingie kwenye kusoma ili tuweze kuitoa sanaa zaidi kutoka kwenye nchi hii kuipeleka kuipeleka kimataifa zaidi, hilo ndilo swala la msingi sana," alifunguka Baucha.
Baucha ambae alikuwa kimya lakini hivi karibuni amerudi kwa kishindo na ngoma yake kali akiwa na Ali Kiba "Kelele" amesema sasa amerudi rasmi kwenye game na yupo0 kivyote kuanzia utayarishaji wa muziki, na uimbaji, na kwamba anampango wa kuzunguka mikoani ili kuibua vipaji ambapo atarekodi kazi za wasanii ambao anaona wanafaa.
Kwa sasa Baucha yuko Paris Ufaransa kuangalia kwa lengo la kuangalia vifaa vya studio, kisha ataelekea Sweden kwa ajili ya show ya mkesha wa mwaka mpya, pia ataelekea pia Berlin Ujeruman ambako atakutana na Snaa lee ambae zamani aliitwa Snop Lee, na Baucha amepanga kufanya nae wimbo.

kwa mujibu wa Baucha mwenyewe kupitia ukurasa wake wa facebook amesema anatarajia kurudi Tanzania January 8 kwa ajili ya kuendelea na kazi zenye ubora zaidi ndani ya studio yake (Baucha Records).

All the best Baucha tunatarajia mengi mazuri na makubwa kwa wadau wa muziki kama wewe kwa ajili ya kuinua mziki wetu wa Tanzania zaidi.

NEW TRACK: TOSH FT. ALONEYM - USIENDE MBALI

6:16 AM
 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates