G-Nako afafanua uhusiano wa kampuni ya WEUSI na Bou Nako, azungumzia mipango yake kwa mwaka 2013, mwaka huu anaweza kuumaliza na zawadi kwa fans wake “huwezi jua”.

12:00 PM

G- Nako ambae hivi karibuni ameachia track yake kali ‘Mama Yeyo’ akiwa na mkali wa RnB Ben Paul, amefunguka kuhusu mengi ambayo fans wake na fans wa WEUSI kwa ujumla wangetaka kufahamu.
Warawara alifunguka katika interview aliyofanya hivi karibuni na Josefly mtangazaji wa radio Victoria Fm ya Musoma kuwa moja kati ya malengo yake yaliyokamilika ni pamoja na kufanya video yake ya take off, kuachia ngoma ya bado Ngware ambayo ilitoka remix yake pia, na hivi karibuni ameachia Mama yeyo.

Lakini akasema huwezi jua anaweza kuachia audio ya wimbo wake aliofanya na AY ‘Take off’ ambao kwa sasa una video tu, na ikawa kama zawadi kwa fans wake ya kufunga mwaka, “You ‘ll never know” ndicho alichosema.
G-warawara aliendelea kufunguka kuwa hayo yasingekuwa malengo yake kama alivyotaka iwe, “kubwa nachotaka ni muziki wangu ufike nje, kupata more shows nje na kuendelea kuwalisha watu wangu madini kadri inavyotakiwa,” that’s G-Nako.
Na kuhusu mipango yake ya mwakani, alisema kikubwa ni kujenga fan base yake iwe kubwa zaidi ikiwa ni pamoja na kuwaweka fans wake pamoja, na ukishajenga fan base kubwa ndo mambo mengine yanaanzia hapo, na Mnako huyo hajali itachukua muda gani kuikamilisha.
On top of that, G-Nako aliulizwa kwa nini Bou Nako ambae ni member wa Nako 2 Nako hakuingia kwenye list ya majina ya kampuni ya WEUSI, na hapo akafunguka, “unajua swala la kampuni ni swala ambalo liko tofauti kidogo na ni swala ambalo liko serious kidogo, sasa unakuta wakati ambapo mnaanzisha kampuni mnakuta labda watu wa wiwili mnaleta mawazo mezani na mnapanga labda flani afanye hivi flani afanye hivi.”
Akazama ndani kwa ufafanuzi wa kilichotokea, “kilichotokea ni kwamba wakati wazo linatokea tulikuwa watu watano na mpaka mwendelezo wake tulikuwa watano kwa hiyo tukaona kwamba hapa tuko kamili labda kinachotakiwa ni mtu ambae tunaweza kumuuzia share zetu. Lakini hata Bou Nako pia ambae yuko Nako 2 Nako, na WEUSI kama kampuni nae ni Part of it, tunapopata kazi ambazo tunaweza kufanya nae ni mtu wa karibu.”
Hapo sawa kumbe bado Bou Nako ni part of WEUSI in one way or another. Na kuhusu issue ambayo wengi wamekuwa wakihoji kuwa collaboration nyingi za members wa Nako 2 Nako na River Camp soldiers hazimhusishi Bou Nako, Warawara aliitolea ufafanuzi zaidi,
“ Bou Nako alikuwa akifanya kazi zake kama solo artist, kama G-Nako nimekuwa nikifanya kazi zangu kama solo artist, Lord Eyez hali kadhalika, kinachotokea ni kwamba mara nyingi tunavyotengeneza muziki unakuta labda niko na Joh, ama wengine ambao unakuta niko nao mara nyingi, lakini Lord eyez anafanya project zake na mimi nafanya project zangu, kwa hiyo tunafanya kitu ambacho kinatokea at the right time right moment,” alifunguka the finest wa A.R.

Kumbe Video mpya ya Diamond 'KESHO' imevuja kimakosa!! Aelezea jinsi ilivyokuwa

11:51 AM

Video mpya ya Diamond 'KESHO' ambayo imeanza kuonekana kwenye mtandao wa internet  jana usiku, ilivuja kimakosa na kusambaa kwa watu. 

Diamond kupitia kipindi cha Power Jams cha East Africa Radio leo amesema kampuni ya Ogopa Djs ya nchini Kenya ambao ndio wametengeneza video hiyo waliitupia 
walii-upload video hiyo youtube kama njia ya kumtumia Diamond na uongozi wake waitazame kwanza kama iko sawa kabla ya makabidhiano rasmi.

Akaendelea kusema baada ya Diamond kutumiwa link ya video hiyo na kuitazama aligundua baadhi ya makosa na kuwaomba Ogopa warekebishe, na baadhi ya makosa ni pamoja na titles za video zinazoonyesha producer wa wimbo ni Wasafi Entertainment na huku aliefanya wimbo huo ni Marco Chali wa Mj Records.

Diamond aliendelea kufunguka kuwa baada ya kukubaliana na Ogopa waliiondoa kwenye youtube video hiyo lakini ilikuwa too late kwani tayari watu walikuwa wameishai download na kuiweka katika akaunti zao binafsi.

Diamond alimalizia kwa kusema video rasmi ya 'Kesho' itatoka rasmi Ijumaa ya wiki hii na pia bado yeye na management yake wanajadiliana kama itoke video na audio pamoja ama video peke yake.


GRANDPA FAMILY

11:42 AM

NYOTA AWARDS 2012 NOMINATION LIST

11:41 AM
MALE ARTISTE OF THE YEAR
D.N.A
MEJJA
RABBIT
 PROFF
FEMALE ARTISTE OF THE YEAR
AVRIL
XTATIC
SIZE 8
KENDI
AMILEENA

DANCE CREW OF THE YEAR

MISCARS DANCERS
TREMAZ DANCERS
MAGICIAN DANCERS
FLEMARZ DANCERS
KIPAJI FITI DANCERS

DJ OF THE YEAR

DJ KAYTRIXX
DJ FLASH
DJ KENNEFLI
DJ HASSAN
DJ PETER ADAMS
DJ SPIN ON KENYA

MOST PROMISING ARTISTE

TL-MO
PENDO
TIERRA GEE
JAY A
AMINA
CHIFU
3D KIPAJI
TABBZ TOMBOY

BESTACTOR/ACTRESS

SHISH
ANTO
BRENDA
MISS MORGAN

BEST T.V SHOW

MSETO EAST AFRICA
IS VIPI
CLUB 1
RIDDIM UP

RADIO STATION OF THE YEAR

GHETTO RADIO
RADIO MAISHA
KISS 100
EASY FM
CITIZEN

PRESENTER OF THE YEAR

MBUSI
WILLY M MTUVA
MWENDE
SHAFFIE

BEST COLLABO OF THE YEAR

CAMP MULLA
GRANDPA FAMILY
MOG N RUFFTONE
NONINI N ANNET

BEST PRODUCTION HOUSES

GRANDPA
CALIF RECORDS
OGOPA
YOUNG WALLACE
RKAY

BEST NEWS PAPER/MAGAZINE

PULSE
THE STAR
ZUQKA
EVE



BEST SONG OF THE YEAR
1.WHY-AMILEENA
2.VIDONGE-SIZE 8
3.CHAPA-FIMBO-GRANDA FAMILY
4.CAMP MULLA

AND SPECIAL AWARD WILL BE GIVEN TO
SOCIALLY RESPONSIBLE AND BUSSINESS MINDED MALE AND ARTIST OF THE YEAR
 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates