GHAKA FT MR. WAIZ - DJ (Officiall Video)

11:15 AM

ATHARI ZA KUFANYA MAPENZI MARA KWA MARA

10:45 AM

Wapenzi wengi hasa wale ambao uhusiano wao ni mchanga hupenda sana kufanya mapenzi kila wanapokutana au wanapohisi wamehemkwa na miili yako.

Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nying

i, lakini linapokuja suala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo huleta madhara kwa watu wanaoendekeza sana ngono.


Kuna watu ambao hawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku wengine wakikosa uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu.


Mtu anaweza kuwa na mke na kujikuta kila siku anatumia ‘chakula cha usiku’ kwa sababu tu hakuna wa kumkataza na kwamba ana haki ya kufanya hivyo kwa sababu amelipa mahari.


Hilo linaweza kuwa jambo jema kwa upande mwingine, lakini uchunguzi unaonyesha kuwa watu wengi kati ya watu wanaolalamika kupoteza hisia za kimapenzi hutoka katika kundi la watu wapenda ngono.


Pamoja na tatizo hilo, yapo madhara mengine mengi ambayo mtu asiyekuwa na kiasi katika tendo la ndoa anaweza kukabiliana nayo, hivyo ni vema tukajifunza ili tusiwe watu wa kuendekeza miili kiasi cha kulazimika kufanya mapenzi kila tunapokutana hata kwenye nguzo ya umeme na chini ya miti kwa vile tu miili imetaka kufurahika.

KUPOTEZA HAMU YA TENDO

Watu wenye pupa za kufanya mapenzi hupoteza haraka hisia za kimapenzi kwa wapenzi wao kutokana na sababu za kisaikolojia zinazoweza kujitokeza wakati wa ufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa mara.


Sababu hizo zinaweza kuwa ni pamoja na zile za kumzoea mwenza kiasi cha kukosa msisimko hata anapomuona akiwa mtupu.



Aidha kukinai haraka staili za kimapenzi kunatajwa kujitokeza kutokana na kukutana mara kwa mara kwa aina zile zile za mapenzi na pengine sehemu moja, kitanda kimoja na chumba kile kile, jambo ambalo linaweza kumfanya mhusika asione jipya kutoka kwa mwenza wake na hivyo kupoteza hamu naye na kuhisi kama hawezi tena kushiriki tendo la ndoa kikamilifu.

Photo: ATHARI ZA KUFANYA MAPENZI MARA KWA MARA Wapenzi wengi hasa wale ambao uhusiano wao ni mchanga hupenda sana kufanya mapenzi kila wanapokutana au wanapohisi wamehemkwa na miili yako. Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini linapokuja suala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo huleta madhara kwa watu wanaoendekeza sana ngono. Kuna watu ambao hawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku wengine wakikosa uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu. Mtu anaweza kuwa na mke na kujikuta kila siku anatumia ‘chakula cha usiku’ kwa sababu tu hakuna wa kumkataza na kwamba ana haki ya kufanya hivyo kwa sababu amelipa mahari. Hilo linaweza kuwa jambo jema kwa upande mwingine, lakini uchunguzi unaonyesha kuwa watu wengi kati ya watu wanaolalamika kupoteza hisia za kimapenzi hutoka katika kundi la watu wapenda ngono. Pamoja na tatizo hilo, yapo madhara mengine mengi ambayo mtu asiyekuwa na kiasi katika tendo la ndoa anaweza kukabiliana nayo, hivyo ni vema tukajifunza ili tusiwe watu wa kuendekeza miili kiasi cha kulazimika kufanya mapenzi kila tunapokutana hata kwenye nguzo ya umeme na chini ya miti kwa vile tu miili imetaka kufurahika. KUPOTEZA HAMU YA TENDO Watu wenye pupa za kufanya mapenzi hupoteza haraka hisia za kimapenzi kwa wapenzi wao kutokana na sababu za kisaikolojia zinazoweza kujitokeza wakati wa ufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa mara. Sababu hizo zinaweza kuwa ni pamoja na zile za kumzoea mwenza kiasi cha kukosa msisimko hata anapomuona akiwa mtupu. Aidha kukinai haraka staili za kimapenzi kunatajwa kujitokeza kutokana na kukutana mara kwa mara kwa aina zile zile za mapenzi na pengine sehemu moja, kitanda kimoja na chumba kile kile, jambo ambalo linaweza kumfanya mhusika asione jipya kutoka kwa mwenza wake na hivyo kupoteza hamu naye na kuhisi kama hawezi tena kushiriki tendo la ndoa kikamilifu.

FANYA HAYA UNAPO MPENDA MTU MWENYE MPENZI WAKE

10:36 AM

Tumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ametuwezesha kuonana tena wiki hii tukiwa wazima. Lakini pia tumshukuru kwa kutuletea kitu kinachoitwa mapenzi.


Mapenzi yamekuwa yakichukua nafasi kubwa sana katika maisha yetu ya kila siku na yamekuwa yakichangia kwa kiasi kikubwa furaha kwa kila mtu.


Kama huamini, angalia wale waliotokea kupenda na wao wakapendwa, utabaini nyuso zao zimetawaliwa na furaha isiyo na kifani. Lakini mapenzi hayo hayo yamekuwa ni chanzo cha vilio kwa baadhi ya watu.


Mpenzi msomaji wangu, kupenda hakuna macho! Moyo ukishapenda hausikii la kuambiwa. Katika hili ndiyo maana unaweza kumuona mwanaume kazimika kwa demu ambaye hawaendani kabisa lakini moyo wake ndiyo umeshapenda.


Ilishawahi kutokea msichana akampenda kijana mmoja ambaye ni fukara kupita maelezo. Yeye akawa ndiyo anamhudumia kwa kila kitu. Akamfanyia mpango wa ajira na mwisho wake wakafunga ndoa.


Sasa hivi wanaishi maisha ya furaha na amani. Wamegeuka mfano wa kuigwa kwa jinsi wanavyopendana lakini huko nyuma msichana huyo alikuwa akichekwa kwa kutoa penzi kwa mwanaume asiye na mbele wala nyuma.


Hayo ndiyo mapenzi jamani! Lakini pia katika kufurukuta kumtafuta mpenzi wa kuwa naye maishani, mwanaume anaweza kujikuta unaangukia kwa demu ambaye tayari ana mpenzi wake.


Moyo wako unakuambia yeye ndiye mtu sahihi katika maisha yako lakini tayari ana mtu wake, unafanyaje?


Utapambana kuhakikisha unapata kile ambacho moyo wako umekipenda au utakubaliana na ukweli kwamba huwezi kuwa naye kwa kuwa ana mtu wake? Inapofikia hatua hiyo unaweza kujikuta upo njia panda hasa pale ambapo huyo mwenye mtu wake naye anaonesha kuwa na chembechembe za mapenzi kwako.

Kuna mambo kadhaa ya kukusaidia kukabiliana na hali hii.


Chunguza

Tumia muda wako mwingi kuchunguza juu ya uhusiano wake. Uhusiano wao umesimama na wanaonekana ni watu wenye ‘future’? Nasema hivyo kwa sababu, yawezekana uhusiano wa huyo uliyetokea kumpenda ni wa kuzuga tu na huenda wewe ndiye mwenye ‘future’ naye. Ndiyo maana nikasema chunguza uhusiano wake kwanza.


Usitafute uadui

Baada ya kuchunguza, ukibaini kwamba uhusiano wao hauko ‘siriasi’, vuta subira, lolote linaweza kutokea na likaufurahisha moyo wako. Lakini kama utaona ni watu walio siriasi na wanaelekea kuoana, usitafute uadui bure, kaa pembeni.


Una nafasi kwake?

Sawa umetokea kumpenda msichana aliye na mtu wake, umeshawahi kujiuliza kama una nafasi ndani ya moyo wake? Anaonesha dalili fulani za kukupenda kama unavyompenda na ni mtu anayeonesha kukumisi anapokuwa mbali na wewe? Utakapobaini una nafasi kwake, uamuzi wa kumpotezea hautakuwa na nafasi.


Ni rahisi kubadili uamuzi wake?

Unadhani huyo uliyetokea kumpenda anaweza kubadili maamuzi ya kumuacha huyo aliyenaye kama kweli hawana ‘future’? Utagundua hilo kwa kuongea naye na kumsikia kama anaweza kufanya maamuzi hayo ili awe na wewe.


Pingana na moyo wako

Ifike wakati upingane na moyo wako. Unajua moyo wako kukuambia kuwa unataka kuwa na uhusiano na demu ambaye tayari ana mpenzi wake wakati mwingine utakuwa unakupotosha.


Kwa hiyo ukiona vipi, pingana nao. Acha kumng’ang’ania msichana mwenye mpenzi wake licha ya ukweli kwamba, huenda wewe ndiye mwenye nafasi ya kuwa mume wake na siyo huyo aliye naye.


Urafiki ni poa?

Umempenda sana na hauko tayari kumkosa katika maisha yako lakini imetokea kwamba tayari yuko na mtu na umebaini huna nafasi kwake kabisa? Usiumie, omba angalau urafiki. Siyo urafiki wa kivile sana ila angalau pale unapotaka kusikia sauti yake kwa kumsalimia tu, upate nafasi hiyo.


Usiumie, yupo mwingine

Haina haja ya kujitafutia vidonda vya tumbo bure kwa kuwa tu umebaini uliyetokea kumpenda tayari ana mtu. Chukulia ni hali ya kawaida, mademu wazuri ambao wanaishi singo wapo kibao huko mtaani, ni suala la wewe kutulia tu. Amini yupo mwingine ambaye atayafanya maisha yako yawe ya furaha.


Naomba nihitimishe kwa kusema kwamba, unapotokea kumpenda mtu fulani, pambana kuhakikisha unampata kwa sababu ukimkosa maisha yako yanaweza kuwa gizani. Ila pale utakapoona uwezekano wa kuwa naye haupo, usilazimishe ndugu yangu. Kumbuka haya ni maisha tu!

NEW TRACK: MBEYA ALL STAR

10:26 AM
 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates