Taylor Swift & Justine Bieber waongoza Tuzo za MTV

12:40 PM

Jana usiku zilitolewa tuzo za MTV UEROP MUSIC AWARD jijini Frankfurt Ujerumani Justine Biber na Tayla Swift wameongoza kila mmoja kuchukua tuzo 3
Taylor alishinda
    1.Best Woman
  2.Best Look
3.Best Live
Justine Bieber.
1.Best male
2.Best Pop
           3.Best world Stage


MAKUNDI YA MICHUANO YA CECAFA

12:34 PM


  Makundi ya michuano ya CECAFA inayofanyika jijini Kampala imetoka huku Tanzania Bara ikipangwa kundi B na Zanzibar ikipangwa kundi C. Michuano hiyo itaanza November 24.
 Makundi yamepangwa hivi

SUBA MKOLE

12:28 PM

BAUCHA FT ALLY KIBA - KELELE (Oficiall Video)

12:23 PM

MWANZO MWISHO -GENTRIEZ (Officiall Video)

12:21 PM

NEW TRACK: WEUSI - NIACHE KIDOGO

12:05 PM

NEW TRACK: CHAMBER SQUAD - HOME SWEET HOME

12:02 PM

NEW TRACK- BUIBUI - BORA UNGESEMA

11:57 AM

Jarida la Bongo5 laingia mtaani.

11:53 AM

Mabibi na mabwana, toleo  jipya la mwezi November la jarida ulipendalo la Bongo5 hatimaye limeingia mtaani rasmi likiwa na mastory kibao tena very exclusive. Mfahamu vizuri Salama Jabir kama ana mpenzi ama lah! Unafahamu kuwa anataka kuja kuwa mama siku moja? Nani wa kuziba pengo la Kanumba? Jipatie nakala yako kujua wadau wa filamu wanawataja akina nani! Kuna makala nyingine kama ‘Lulu na Kajala na mwisho unaosikitisha’, Feza Kessy aingia rasmi kwenye muziki, soma ujue alivyojipanga.
Kuna makala ya Swahili Rap Inspiration iliyoandikwa na Ezden Jumanne ambapo utafamu impact ya NikkiMbishi aka Baba Malcom, One the Incredible na Stereo kwenye Hip hop ya Tanzania.
Unataka kuwafahamu wasanii wa kiume wanaokimbiza zaidi sasa hivi Tanzania? Makala ya Bongo Kings itakupa jibu. Makala ya ujio wa Rick Ross waipa heshima Tanzania na wasanii watano waliofunika zaidi kwenye Fiesta. Makala ya Kona ya Mjasiriamali isemayo: ACHA KUTAFUTA KAZI, ANZA KUTAFUTA FURSA. Unawafahamu wanasayansi wachanga wa Tanzania?
Kijana unafahamu haki na wajibu wako? Pata nakala yako uzijue. Kuna safu inaitwa Haileweki ambapo kuna kali kama, Nani aliyemtupia TID skendo ya kutaka kumuua Ali Kiba? Pamoja picha za kuvutia za matukio kama Fiesta Dar, Uzinduzi wa filamu ya Skyfall - Mlimani City na mambo mengine mengi!!
Pata nakala yako kwa shilingi elfu tatu tu.

Major Harris wa “The Deflonics” Afariki dunia akiwa na miaka 65.

11:51 AM
Anaitwa Major Harris…aliyekuwa member wa kundi la muziki wa soul kutoka Philadelphia “The Delfonics” ameripotiwa kufariki dunia huko Richmond, Virginia.
Vyombo vya habari vya karibu vimeripoti kifo hicho kutokea ijumaa Nov 09 kutokana matatizo ya moyo aliyokuwa nayo muda mrefu na kushindwa kufanya kazi kwa mapafu ambako kulipelekea kukimbizwa hospitali na baadae kufariki dunia.
Kihistoria Major Harris alianza muziki long time..mwishoni mwa miaka ya 50’s na aliwahi kuwa member wa makundi kibao tu kama Charmers, Frankie Lymon’s Teenagers na Nat Turner’s Rebeillion kabla hajamalizia muziki wake The Delfonics mwanzoni mwa 1970’s ambapo walitengeneza hits kama “La-La (Means I Love You) and “Didn’t I (Blow Your Mind This Time)”.
Wasanii kibao wa HipHop wa mid era wame-sample ngoma kibao za The Deflonics…baadhi yao ni pamoja na Grand Puba “Very Special”, Ghostface Killah “Holla” & “R.A.G.U.” na Fugees “Ready or Not”..R.I.P Major Harris.

Shettah aelezea sababu za Lady Jay dee kukataa kupiga nae collabo katika wimbo wake mpya 'Bonge la bwana'.

11:44 AM
Shettah
Siku kadhaa zilizopita msanii aliefanya vizuri na nyimbo kadhaa ikiwemo 'Nidanganye' Shettah, alitangaza juu ya wimbo wake mpya aliopanga kumshirikisha binti machozi Lady jay dee.

Kupitia Power Jams ya EA radio, Shettah ameelezea mabadiliko yaliyojitokeza juu ya wimbo huo ambao imebidi amshirikishe Linah Sanga na sio Jide kama alivyotangaza awali. Shettah amesema hapo awali alikuwa ameshawasiliana na Lady Jay dee aliyemkubalia kufanya nae wimbo huo na Shettah alimpatia title ya wimbo ili aweze kujiandaa nayo. Mabadiliko yalikuja kujitokeza baada ya Jide kuiskia mistari ya Shettah ya wimbo huo kitu ambacho kilimsababisha kukataa kuimba katika wimbo huo kama walivyokuwa wamekubaliana mwanzo. 

"mwanzo alikuwa amekubali kabisa na nikampa title ya 'Bonge la bwana' lakini alipokuja kuiskia mistari akasema hakujua kama mimi nimeimba hicho nilichoimba so ni ngumu yeye kuimba sababu hafit kwenye idea hiyo maana hata kiumri yeye ni mkubwa kwangu, ila akasema labda niibadilishe kidogo idea kitu ambacho nimeona kitafanya na mimi nibadilike kuanzia mwanzo mpaka mwisho huku ngoma tayari iko poa. So nimeamua kuifanya na Linah na Jide kasema poa nifanye na mtu mwingine halafu yeye ntakuja kufanya nae wimbo mwingine" alisema Shettah.

Shettah anategemea kuuzindua wimbo wake huo mpya wa 'Bonge la bwana' pale Maisha club tarehe 25 mwezi huu wa November, na amewataja wasanii watakao mpa support katika show hiyo kuwa ni pamoja na Feruz, Jaffarai, Pasha, One, Stereo, Young Dee, Shilole na wengine. 

Wimbo huo umerekodiwa pale G-Records na video yake inatarajiwa kufanywa na Adam Juma wa Visual Lab Next Level.
 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates