KALI KUTOKA FACEBOOK USIKU HUU

2:19 PM
NISHAOMBA SANA MDAHALO NA HAO WASANII WENU MNAOWAITA HIP HOP,LAKINI NAONA KIMYA MPAKA LEO,HIVI NEY WA MITEGO AKIWA HIP HOP NA RAKIM NAE ANAKUA NANI?MNATAKA TUONGEEE ILI MTUITE WABISHI AU KAMA GENERAL ULIMWENGU ALIVYOAMBIWA SIO RAIA?NASH EMCEE SAID KUBENEA!
Like · · · a few seconds ago ·

Fedha, uzuri si kinga ya mapenzi, kuna kitu cha ziada

12:46 PM


WAKATI akili yangu ikianza kupata ufahamu, nilikuwa natatizika na kuwaza kitu gani hasa katika mapenzi kinaweza kumfanya mtu atulie ndani ya penzi lake. Niliamini kuwa na fedha ndiyo dawa ya mtu kumtuliza mpenzi wake au kwa mwanamke kuwa mzuri na mwenye sifa zote, ndiyo dawa ya kumfanya mpenzi wako atulie.
Baada ya kukua na kuingia katika dunia ya ufahamu wenye mitihani mingi ya mapenzi, nimegundua kuna utofauti mkubwa katika vitu nilivyoviwaza.
Wakati nakua, nilikutana na matukio ambayo niliona kama ngamia kupita kwenye tundu la sindano, lakini baada ya kupevuka, nilipata majibu ya maswali yaliyonisumbua kipindi kile cha utoto.
Sikuamini mke wa tajiri kufanya mapenzi na muuza mchicha, mwanaume mwenye mke mzuri kutembea na changudoa au msichana wa kazi asiyejua kuvaa wala kuoga.
Baada ya kuingia katika kazi hii ya kukumbushana mambo ya mapenzi, nilipata maswali mawili ya watu wawili tofauti lakini yalikuwa na jibu moja.
Mmoja alilalamika ana mke, anamhudumia kila kitu ikiwemo familia yake lakini alichomlipa ni kutembea na mtu asiye na mbele wala nyuma. Mwingine alilalamika kuhusu mpenzi wake kutembea na mwanamke wa nyumba ya pili ambaye haufikii hata mguu wake kwa uzuri.
Kabla ya kulizungumzia hilo, nirudi kwao kuwaeleza kukosa uamini hakuangalii katembea na tajiri au mwanamke anayekushinda uzuri, kutoka nje ya uhusiano au ndoa ni kosa kwa vile penzi ni la watu walioridhiana au kuoana wakiwemo waliooa wake zaidi ya mmoja.
Leo nawajibu wote kuwa fedha au uzuri wa mtu havibebi ndoa au uhusiano. Nimekuwa muumini mzuri wa kuwaeleza penzi la kweli lipo vipi, mapenzi ni upendo wa dhati kutoka moyoni, kuwa tayari kujilinda na kujiheshimu bila kujali una fedha au ni mwanamke mzuri.
Mapenzi ni mbegu inayohitaji udongo wenye rutuba ya upendo ili mbegu hiyo imee. Siku zote mwenye mapenzi ya kweli humuangalia mtu, si kitu.
Tajiri na fedha zake asipopendwa huwa katika mateso na kukonda wakati ana kila kitu. Penzi la kweli halinunuliwi kwa gharama yoyote.
Tabia ya asili huwa sawa na moto unaowaka kwenye pamba, ukitoa moshi ujue hakuna kilicho salama. Wapo watu wasiokuwa na mapenzi ya dhati, utakuta mtu anajifanya anakupenda ukiwa naye lakini mkiachana hana habari na wewe, hata kama mnakaa nyumba moja na kulala kitanda kimoja.
Mtu anapoamua kutoka nje ya ndoa wakati ndani ana mke mzuri au mume wa ukweli anayempa kila kitu, kuna mawili:
Mosi:
Huenda mwanamke aliyenaye alimtamani kutokana na sura na umbile lake na hakumpenda kwa dhati. Matokeo yake baada ya kumchoka, mwanamke huonekana hafai na hukaa naye kimazoea.
Upande wa mwanamke, naye huenda amekwenda kwa mwanaume kutokana na kujua ana fedha lakini anakuwa hana mapenzi naye. Hapo lazima atatafuta penzi la nje ili afurahishe nafsi yake, kwa hiyo watu hawa kutoka nje sishangai.
Pili:
Tabia ya kutoridhika na mpenzi mmoja, watu wa aina hii huwa hawajisikii kula kitu cha aina moja kwa muda mrefu, lazima atatafuta mtu wa kumfanya abadili mboga.
Vitu hivi vyote huwa vinawachanganya watu, hasa wale wanaoamini kuwa mwanaume anapokuwa na fedha au mwanamke anapokuwa mzuri, ni kila kitu katika mapenzi.
Mapenzi ni bahati, hasa kumpata uliyemkusudia, basi muombe Mungu utakayemchagua naye awe kweli amekukubali, hata ukiwa mbali kila mmoja amlindie mwenzake heshima, kwa kutanguliza uaminifu mbele.

RAMA DEE APONDA SHOW YA RICK ROSS

12:30 PM


PICTURES ZA MAANDAMANO YA MBAGALA LEO

12:26 PM





















Baada ya kushutumiwa ku-copy nyimbo, Timbulo sasa apiga collabo na X-maleya wa Cameroon.

12:03 PM
Redsan

Msanii wa nchini Kenya Swabri Mohammed maarufu kama Redsan amesema alikataa deal la kupiga picha za utupu kwa sababu hiyo sio tabia yake.
Katika interview aliyofanya na mtangazaji wa radio moja nchini Kenya aitwae Adelle ambae alikuwa anamuuliza kuhusu maisha yake, mtangazaji huyo alimuuliza Redsan kama alishawahi kupiga picha akiwa naked, na jibu la Redsan liliambatana na taarifa ambayo iliwashtua mashabiki wengi.
“Nakutaka” hit maker alisema hajawahi kupiga picha akiwa mtupu na hatafanya hivyo, kaisha akaongeza kuwa “actually hivi karibuni jarida la Fitness walipropose nipige picha nikiwa bila nguo, lakini nikawaambia hiyo sio style yangu.”
Watu maarufu wengi hasa waimbaji na wasanii wa kuigiza wamekuwa wakipiga picha zinazoonesha wakiwa nusu uchi ama hata wako naked, kutokana na kuwa siku za karibuni Kenya kumekuwepo na baadhi ya majarida yanayotoa mpunga mrefu kwa ajili ya matangazo ya picha za aina hiyo. Tunaweza kusema kwa kulingana na maadili ya kiafrika basi Redsan ni mfano wa kuigwa.
Mwanzoni mwa mwaka huu media zilimuandama sana Redsan baada ya kufungwa minyororo ya mapenzi na msichana aliyemaliza chuo Kikuu cha Nairobi Viverz a.k.a Lilo ambae alituhumiwa kumpiga limbwata , ‘juju’ ama Kamote kama inavyojulikana huko Kenya ili amuibe kutoka kwa girlfriend wake aliyejulikana kwa jina la Delilah.
Rumors zilizozagaa kwenye mitaa ya Nairobi zilisema mwanadada Lilo alizuga anaujauzito ili kumkoleza zaidi Redsan, na Redsan akachukua jukumu lote na inasemekana walifunga ndoa ya kwa usiri  maeneo ya Pangani.

Baada ya kushutumiwa ku-copy nyimbo, Timbulo sasa apiga collabo na X-maleya wa Cameroon.

12:02 PM
Msanii wa bongo flevah nchini Tanzania maarufu kama Timbulo amesema anategemea kutoa wimbo wake mpya siku chache zijazo ambao amewashirikisha kundi la X-maleya kutoka nchini Cameroon.

Miezi kadhaa iliyopita Timbulo aliandamwa na maswali mengi yaliyoambatana na maneno ya kumshutumu kuwa ali copy na kupaste nyimbo zake mbili zilizopita "Domo Langu" na "Waleo Wakesho" kutoka katika nyimbo za kundi hilo.

Kwa mujibu wa maelezo ya Timbulo alidai kuwa haku copy bila idhini ya wenye nyimbo kama inavyodhaniwa na wengi, bali alipewa ruhusa na X-Maleya wenyewe na vithibitisho vyote anavyo.

Timbulo ameendelea kusema kutokana na kwamba anawa feel sana X-maleya na wao wanam feel, sasa ameamua kuwashirikisha kabisa katika wimbo wake mpya aliouita "Lastic ya Upendo" inayotegemewa kutoka hivi karibuni na tayari wameshamtumia demo yenye sauti zao na ya Timbulo na kinachosubiriwa sasa ni mixing imalizike.

Kupitia ukurasa wake wa facebook Timbulo leo ameandika: " Habar njema ni kwamba wimbo mpya tayar upo mkonon, waitwa Lastic ya upendo nimefanya na x-maleya, a group music from cameroun, ambao nimewah kutajwa kuiba nyimbo kutoka kwao,,,!".

Leotainment ilimuuliza Timbulo juu ya mpango wa video ya wimbo huu aliyowashirikisha wasanii kutoka nje ya Tanzania, na hiki ndicho alichojibu: 

" Wao X-maleya walitupa option tatu za kufanya video, option ya kwanza ni wao watutumie clips za parts zao walizoimba katika wimbo huu watakazo shot huko kwao. Option ya pili ni sisi tusafiri kwenda Cameroon kushot huko, na option ya tatu ni wao waje Tanzania tushot hapa. Sasa mpango mzima utafahamika mara baada ya audio ya wimbo huu kuwa released wiki ijayo kama mixing na mastering itakuwa imekamilika, lakini uamuzi wa kufanya video utatoka katika hizo option tatu".

Kazi hii ya "Lastic ya upendo"  imetengenezwa katika studio ya Combination Sound chini ya producer Man water, lakini mixing inafanyika hapa Tanzania na Cameroon kisha watachagua ile itakayokuwa nzuri zaidi kwa ajili ya official release.

PEEN LAWYER WA ANTI-VIRUS AMEFUNGUKA KUHUSU TUKIO LA DIAMOND KUVUA NA KUBAKI NA BOXER KWENYE STAGE YA FIESTA.

11:59 AM
SIKU CHACHE BAADA YA KUMVAA CYRILL KUHUSU SLOGAN YA FIESTA 2012  "BAAASS"" SASA PEENLAWYER WA ANT-VIRUS NA UWAZI MIXTAPE AMEFUNGUKA KUHUSU  TUKIO LA DIAMOND KUVUA NA KUBAKI NA  BOXER KWENYE STAGE YA FIESTA....

MSIKILIZE HAPA...

The Game anataka kuanzisha upya beef na 50 Cent?Ajiita ‘-Unit killer’

11:54 AM

Rapper the Game ambae alizinguana na kundi la G-Unit na kuachana miaka mingi iliyopita amefunguka na kusema yeye ndiye muuaji wa kundi hilo linaloongozwa na 50 Cent.
Rapper huyo ambae hivi karibuni alitangaza kuwa amebatizwa na ameanza maisha mapya ya kiroho anaonekana kurudi nyuma kidogo na kuwachokoza G-Unit kundi ambalo members wake wa zamani wote waliondoka, Loyd Banks, Tony Yayo walifuata baada ya Game, lakini sasa 50 Cent amewasaini wasanii wapya ambao kiukweli hawana moto kama wale members wa zamani.
Game na 50 Cent waliingia katika mtafaruku mkubwa sana katikati ya miaka ya 2000 na Game akaanzisha kampeni inayoitwa G-U NOT. Na akasema kuwa 50 Cent aliandika wimbo wake ili aendelee kuwa juu kwenye kundi kwa kuwa alikuwa na ‘umimi’ na akaeleza kwa nini alikuwa na hasira dhidi ya 50 Cent na G-Unit. “300 Bars niliandika nikiwa na hasira sana na nilitaka G-Unit ife brand kama brand, recording label, ama group…kuna msitari niliandika ukisema you sell records but a G-G-G-Unot. Na baada ya hapo zikatoka T-Shirt na harakati zikapiga hatua hata zaidi yangu.”
Lakini mwezi march mwaka huu Game alipoulizwa kuhusu kilichotokea miaka hiyo kati yake na Boss wake 50 Cent, alisema hiyo ilikuwa ni beef ya muda mfupi, “ilidumu kwa muda wa mwaka mmoja au miwili hivi na ilinichukulia muda mwingi sana na ilinifrustrate mimi na watu wengi. Kwa hiyo nilipoanza kuandaa album ya tatu, ya pili na sasa nimeanza na hii ya nne nadhani busara kidogo ilitumika, na mimi natokea Los Angeles na sikujiingiza moja kwa moja katika huo mtego” alisema Game akimaanisha mtego wa hilo beef.
Akamaliza kusema anadhani hii inawahusisha zaidi fans wao na wakosoaji wao na kile kilichoko kati ya maadui wawili ambao walikuwa ni yeye na 50 Cent na kwamba sometimes asingeweza kucontrol hili.

Mama mtu mzima mahakamani kwa kufanya mapenzi na watoto wawili mtu na mdogo wake, mmoja miaka 15 mwingine 17... Apata ujauzito , ashindwa kujua ni wa nani kati yao!!

11:53 AM

Mama mmoja aliyeolewa na mwenye watoto watatu ambae anaishi Hull, Uingereza, amefikishwa mahakamani baada ya kugundulika kuwa alipata ujauzito baada ya kufanya mapenzi kwa wakati mmoja na mtoto wa shule, mmoja mwenye miaka 15 na kaka yake mwenye miaka 17.
Mama huyo anaejulikana kwa jina la Claire Louise Roundil(32), alimnasa mtoto wa miaka 15 kimapenzi baada ya kumuonesha picha zake zaidi ya mia moja akiwa mtupu, picha zilizoonesha zaidi sehemu za matiti.
Baada ya kumteka akili na hizo picha mama huyo alimpeleka chocho na akampa huyo mtoto share ya mmewe. Lakini aliendelea kumbadilishia location mara kwa mara ili kumpa mzuka zaidi wa kufanya nae sex.
Ripoti ya polisi ilionesha kuwa mama huyo alikuwa pia na mahusiano ya kimapenzi na kaka yake huyo mtoto na alimpata kwa style ile ile kama alivyomnasa mdogo wake, yaani kumuonesha picha zake akiwa mtupu kisha anamteka akili na kumpeleka kajificheni kumpa burudani, na mara nyingine shughuli iliishia kwenye gari la mama huyo.
Hata hivyo uchunguzi wa polisi ulionesha kuwa baada ya mama huyo kupata ujauzito ilimbidi autoe, na alipoulizwa alisema kuwa hata aliyempa mimba hamjui kati ya hao watoto wawili kwa sababu alikuwa anafanya nao mapenzi wote.
Moja kati ya sababu za kufanya hivyo imesekana kuwa alikuwa na matatizo makubwa katika ndoa yake na matatizo ya kifedha ambavyo vyote viliichanganya sana akili yake.
Na hivyo ikaonekana kuwa “She is not the type of defendant the court needs to send to prison immediately.”  Na akapewa kile kifungo kinachoitwa kisheria “suspended sentence” baada ya kukiri tuhuma zote. Ikimaanisha aliwekwa chini ya uangalizi mkali wa mahakama kwa muda wa miezi tisa.
Na wakati wa kutoa hukumu jaji John Dowse alimwambia mahakama itaweka kumbukumbu ya haya mashtaka, na kwamba ajue kuwa anarekodi hii maisha yake yote.
Hata hivyo baba mzazi wa wavulana hao alisikika akilalamika akisema “kama ingekuwa ni mwanaume ndiye kafanya mapenzi na msichana wa miaka 15 angefungwa hata bila kutia mashaka, lakini kwa sababu ni mwanamke ndo kafanya hivi kwa wavulana kaachiwa, she took advantage of both my son, mwanangu mkubwa alipomuacha akamrukia mdogo, alikuwa amepanga yote haya. Akamaliza kwa kusema “It was disgusting what she did.”
Haya kila kubwa lina Kubwa Lake, na hili ni miongoni mwa makubwa.

Rihanna atumia jina la album yake kuwajibu walioiponda picha yake ya kwenye cover ya album hiyo.

11:51 AM

Baada ya Rihanna kureveal cover ya studio album yake ya saba yenye jina “Unapologetic” watu wengi walitoa maoni kupitia mitandao ya kijamii kama facebook na twitter.
Album cover hiyo inayomuonesha Rihanna akiwa hajavaa chochote juu (naked), picha hiyo inaambatana na maandishi mengi kwenye mwili wake ambayo hayaeleweki japo mawili matatu yanaweza kusomeka lakini bado hayatoi picha inayoeleweka haraka. Kiasi cha kufanya fans wahisi labda ni majina ya nyimbo zitakazokuwa katika album yake, likiwemo jina ‘diamond’ na Unapologetic ambalo ndilo jina la album.
Katika picha ya album cover hiyo chuchu moja ya Rihanna imefunikwa na maandishi wakati nyingine ikiwa ameifunikwa na kiwiko chake cha mkono wa kushoto.
Watu wengi walitoa maoni mbalimbali baada ya kupata details za album hiyo ambayo inategemewa kuachiwa rasmi November 19, 2012 na wengi walionesha kusifia sana cover yake hasa ile picha na baadhi ya tweet za fans zilikuwa na maneno kama ‘I love that’, unapologetic sounds good‘ I’m so proud of her the cover and the name are totally Epic, Perfect, flawless etc’, na mengine mengi ya kusifia.
Lakini kuna walioponda na kushangaa hiyo cover iliyowekwa na wengine ikaonekana kama hii ni picha inayoonesha bad girl Rihanna ambae ni unapologetic.
Rihanna alionekana kutowajali ambao wameiponda na  aliamua kutumia maneno hayo hayo yaliyo kwenye cover la album akajibu critique za wasikilizaji kwa tweet “it's okay! Refer to: album title", akimaanisha she is unapologetic.
 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates