2POINT AFUNGUKA KUHUSU MAHUSIANO YAKE NA SHILOLE

2:09 PM

Presenter anae fanya vizuri kisiwa zanzibar toka Hits fm Radio, 2POINT amefunguka kuhusu mahusiano yake na mwana dada toka bongo movie SHILOLE  msikilize 2POINT akiongea na chiwileinc


NONINI FT ANNETTE - POLE POLE (Officiall Video)

1:59 PM

Nick Minaj ambwatukia Mariah Carey, amtishia “I’m gonna knock you out”

1:55 PM
Nick Minaj

Wiki chache baada ya Mariah Carey kukanusha tetesi kuwa alikuwa na beef na Young Money Queen Nick Minaj ambae ni jaji mwenzake kwenye American Idol sasa mambo yamekuwa tofauti baada ya video yenye picha tofauti kabisa na kile kilichoelezwa na Carey kusambaa kwenye mitandao.
Video hiyo inaonesha Nick Minaj akiwa kakasirika na anampa makavu live Mariah Carey, tukio hili limetokea wakati wanaendelea na kazi yao ya kujaji washiriki mbalimbali na safari hii walikuwa Charlotte, North Carolina.
Mtu mmoja ambae alishuhudia live tukio hilo amesema kuwa Nick Minaj alionekana kupandisha mzuka na kufikia hatua ya kumtishia the R&B diva Mariah Carey na kusema “I’m gonna knock you out”.
Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa Nick Minaj aliongea kwa sauti ya juu sana na kumtolea matusi makali Mariah Carey akisema “I told them, I’m not f***kin’ putting her f**kin’ highness there.”  Lakini hii sehemu haikushikwa na lensi ya camera hiyo iliyokuwa inachukua matukio ya American Idol.
Inasemekana kuwa hii varangati ilitokea baada ya kutofoutiana sana katika maamuzi kwa washiriki walio-perform siku hiyo. Wakati hayo yanatokea, Nick Minaj na Mariah Carey walikuwa wamekaa kwenye meza ya majaji, na jaji mwenzao Keith akiwa amekaa katikati yao na Randy Jackson akiwa amekaa mwishoni upande wa Mariah Carey.
Kutokana na hali hiyo watayarishaji wa American Idol iliwalazimu kusimamisha performance ya siku hiyo ili majaji hawa wacool down kwanza. Hali hii inaonekana kuwatishia waandaji wa American Idol na wana wasiwasi kama Nick Minaj na Mariah Carey watadumu kwa muda mrefu wakiwa wanafanya kazi yao pamoja kama majaji wa American Idol.

Mariah Carey
Katikati ya mwezi September iliripotiwa kuwa Nick Minaj na Mariah Carey hawana maelewano mazuri, na mtu mmoja ambae ni mfatiliaji wa mambo ya muziki Marekani alisema hata Mariah Carey alipopigiwa simu kuambiwa kuwa Nick Minaj ndo atakuwa jaji mwenzake kati ya wale wanne alikata simu.
Lakini September 17 ambapo MTV ilienda New York pale ambapo American Idol ilikuwa imeanza na ikafanyika kwa siku mbili, ili kujionea nini kilikuwa kinaendelea kati ya Mariah Carey na Nick Minaj, na walipouliza kuhusu kutoelewana, wote walikuwa wanatabasamu kama vile walisikia utani hivi, na Mariah Carey akaonesha kushangazwa na taarifa hizi jinsi zilivyosambaa kwa haraka ndani ya muda mfupi sana, na akamaliza kwa kusema "It's fun, it's music, it's singing, it's laughter," na Nick Minaj akawa anatikisa kichwa kuonesha anasapoti alichokuwa anasema Mariah Carey.

Wajuzi wa mambo walisema time will tell sasa kila kitu kinaanza kuonekana hadharani, chanzo kabisa cha kutoelewana kwa wawili hawa bado hakijajulikana kwa sababu kama Mariah Carey alikata simu pale tu aliposikia jaji mwenzake atakuwa Nick Minaj, basi chanzo sio kutoelewana katika maamuzi ya ujaji wao, there must be a long term factor.

Britney Spears, Taylor swift wamsogelea Oprah katika list ya wanawake wanaolipwa zaidi, Rihanna nafasi ya nne, Beyonce afichwa.

1:53 PM
Oprah Winfrey

List ya wanawake wanaojihusisha na entertainment wanaolipwa mpunga mrefu zaidi duniani kwa ajili ya kazi zao kwa mwaka iliyotolewa na Forbes inaonesha kuwa Oprah Winfrey anayeendesha talk show anashikilia nafasi ya kwanza, ambapo kati ya may 2011 na may 2012 amepokea $ 165 million. Na imegundulika kuwa bado kuna mshahara mwingine hajapata, kwa hiyo hautajumuishwa kwenye pato la mwaka ujao, 2013 ili isiwe nafasi ya kumuongezea ushindi tena mwaka ujao kumbe kuna pato la mwaka huu bado analisubiria.

Britney Spears
Katika list hiyo nafasi ya pili imekamatwa na judge wa X Factor mwanadada Britney Spears, ambae yeye ameingiza mpunga wa ukweli kiasi cha $58 million ndani ya mwaka mmoja. Kwa mujibu wa Forbes Spears alimake mkwanja mrefu sana kupitia album yake na hasa kupitia tour ya album hiyo aliyoibatiza “Femme Fatale tour”, na  alijazilishia kwa mkataba mnono wa kuendesha X Factor ambao ni $15 alizozisign.
Taylor Swift
Nafasi ya tatu imekamatwa na mwanadada Taylor Swift ambae ana historia ya aina yake na MTV VMAs, alipovamiwa jukwaani na Kanye West, na hili tukio liliwafanya watu wengi zaidi kutega masikio kwa huyu mwanadada mwenye umri wa miaka 22 hivi. Yeye amemfata kwa karibu sana Briteney Spears kwa kuingiza $57 millioni kwa mwaka kama pato halisi. Huyu ni mwanadada mwenye umri mdogo zaidi kwenye hii list na tour yake ya Speak Now ilichangia kwa kiasi kikubwa sana pato lake lakini pia ngoma kibao kali alizoachia ikiwemo ile safe &sound. Na mwezi huu anatarajia kuachia album yake inayoitwa Red. Kumbuka wimbo wake wa kwanza ulikaa kwenye nafasi za juu sana za Billboard’s Hot 100 chart kwa muda wa wiki tatu.

Rihanna
Nafasi ya nne imekamatwa na the R&B Queen Rihanna, lakini hapa amefungana na mwanadada Ellen DeGeneres wote wakiwa wameingiza kiasi cha $53 million.

Nafasi ya tano imekatwa na Lady Gaga na  jaji wa zamani wa American pop Idol Jeniffer Lopez, wakali hawa wamefungana pia na wameingiza mpunga kiasi cha $52 million kwa kipindi cha mwaka mmoja. Gaga album yake iliyoambatana na tour ya Born This Way imemsaidia kufika hapo.
Wakati majina yanaendelea kushuka, list ilifungwa na supper modal Gisele Bundchen ($45 million) Katy Perry ($45 million) na Judge Judy wa TV show ($45 million).

Hadi list inafungwa hakuna jina la mama Blue Ivy, mwimbaji  Beyonce Knowles Carter hata kwenye top five japo wengi walimtegemea hata katika top three. Kibongobongo tungesema hapa wanawake wenzake waburudishaji wamemficha.

NEW VIDEO: LINAH - OLIVER TWIST REMIX

1:49 PM

EXCLUSIVE: NEW VIDEO: C-SIR MADINI - PAIN KILLER (Official Video)

1:45 PM


C-sir Madini
Baada ya kuonyesha uwezo wake kupitia wimbo wake wa kwanza wa "Kifungo Huru" alioutoa mwaka jana 2011, uliofuatiwa na wimbo wake wa pili alioutoa January mwaka huu 2012 unaoitwa "Nishike Mkono", hii ndio single yake ya tatu ambayo kwa mara ya kwanza chiwileinc inakupa nafasi ya kuiona video yake mpya aliyoipa jina la "PAIN KILLER"

Wimbo huu umeandikwa na kua produced na Kid bwoy wa Tetemesha Recordz. Video imesimamiwa na Adam Juma wa Visual Lab/Next Level.

Kwa mujibu wa management ya C-sir video itaanza kuonekana katika vituo vya TV mapema wiki Ijayo, na itaanza kusikika katika vituo vya radio wiki moja baada ya kuanza kuruka katika Tv stations.

Diamond Platnumz apata management mpya, shows, mavazi, matangazo, vyote vitasimamiwa na I-VIEW MEDIA.

1:39 PM
Mkurugenzi wa I-View Media Raqey na Diamond wakisaini mkataba
Huu ni ukurasa mpya uliofunguliwa na msanii anaefanya vizuri sana hapa nyumbani na nje ya mipaka ya Tanzania Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz, baada ya kufikia uamuzi wa busara na wa kisomi wa kukabidhi madaraka ya kusimamia na kuendesha shughuli zake za muziki kwa kampuni inayoitwa I-VIEW MEDIA ya jijini Da es salaam.


Baada ya zoezi la kusign contract ya miaka miwili, sasa kampuni ya I-View Media ndio itashughulika moja kwa moja na upokeaji wa bookings na kunegotiate deals zote za msanii Diamond za ndani na nje. 

Hii ni hatua nzuri sana kwa Diamond, sababu hakuna biashara inayofanikiwa bila kuwa na miongozo mizuri ambayo inasimamiwa na watu professionals wa field husika.

Hongera sana Diamond kwa hatua hii muhimu katika career yako.
 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates