RAHMA JUMANNE NA NDOTO YA KUA MWANAMITINDO WA KIMATAIFA

2:14 PM






TWITE ATUA YANGA, MAMIA WAMLAKI,

1:53 PM
Twite baada ya kutua Uwanja wa ndege akiwa na viongozi wa Yanga

BEKI mpya wa Yanga, Mbuyu Twite ametua Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere na kulakiwa na mamia ya wapenzi wa klabu hiyo, kabla ya kupakiwa kwenye gari kuelekea makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.

Hakuna kiongozi yeyote wa Simba wala askari polisi aliyemsogelea kama ambavyo kulikuwa kuna tishio kwamba akitua tu beki huyo wa kimataifa wa Rwanda, mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) watamkamata kwa tuhuma za kuwatapeli dola za Kimarekani 30,000.
Inadaiwa, kabla ya kusaini Yanga, Twite aliyekuwa akichezea APR ya Rwanda alisaini Simba na kuchukua dola 30,000.
Hata hivyo, baadaye mchezaji huyo alighairi na kuamua kwenda Yanga na kurudisha fedha za Simba kupitia viongozi wa APR na St Eloi Lupopo ya DRC, ambazo zilikuwa zinammiliki kwa pamoja mchezaji huyo.
Lakini viongozi wa Simba waligoma kupokea fedha hizo ingawa viongozi wa APR na Lupopo walifika hadi ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutaka kuzikabidhi fedha hizo, ili Simba wakazichukulie hapo.
Twite aliianza kuichezea Yanga wiki iliyopita ilipokuwa Kigali, Rwanda kwa ziara ya wiki moja lakini alishindwa kurejea na wenzake Jumatatu kwa kile kilichoelezwa anakamilisha kuhama kwake rasmi na kuja kuanza maisha mapya Dar es Salaam,
Lakini upande wa pili, Simba SC waliamini beki huyo amekwepa kukamatwa kufuatia kuvuja kwa habari za mpango wa kumtegea akitua nchini wamkamate.
Ametua na amekwenda Jangwani, maana yake jaribio la kumkamata akitua limefeli na sasa tusubiri kama Simba watamuwekea mtego mwingine.

Twite akizungumza na Waandishi huku amevaa jezi namba 4 yenye jina Rage






Mjumbe wa Bodi ya Udhamini ya Yanga, Francis Kifukwe kushoto akiwa Uwanja wa Ndege na kigogo wa Usajili, Seif Ahmad 'Magari

FACES ZA MISS MWANZA HIZI HAPA!! SHINDANO KUFANYIKA IJUMAA HII, NDANI YA YATCH CLUB MWANZA!!

1:42 PM





NEW TRACK: Zero ft Mr Blue - Sikuelewi

1:38 PM

Ijumaa hii usikose Uzinduzi wa Santuri 5 kwa pamoja ndani ya NEW MSASANI CLUB

1:35 PM

NEW TRACK: KAGOMAZ & SARKOZY - MULOKO

1:33 PM

WILL START WITH THE IDEA OF TITLE MULOKO,
IT COMES FROM THE WORD LOCAL.
ADAM JUMA ( C.E.O OF VISUAL LAB / NEXT LEVEL )
ONE OF THE BEST DIRECTOR IN AFRICA
CAME ALONG WITH THE IDEA AND WE THOUGHT IT WOULD BE
BETTER IF WE DO IT IN AFRICAN WAY.
THE SONG TALKS ABOUT A LOCAL GIRL.

WE DID THE SONG UNDER


ARTIST : KAGOMAZ & SARKOZYSONG :
MULOKO
PRODUCTION : CHILLI INC 
PRODUCER : TOTI


TOGETHER LETS PROMOTE AFRICAN MUSIC TO ANOTHER LEVEL .
ONE LOVE .

GARDER G HABASH ATUA TIMES FM

1:23 PM
 Aliyekuwa mtangazaji wa Clouds FM katika kipindi cha Jahazi, Garder G Habash aka Captein anatarajia kuanza kutangaza tena Jumatatu ijayo kupitia kituo cha radio c
ha Times FM 100.5 cha Dar es Salaam.

Kipindi chake kiitwacho Maskani kitakuw

a kikiruka kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 10 jioni hadi saa 1 usiku.

Gadner akiongea machache baada ya kutambulishwa Times FM
Kuna tetesi za mtaani ambazo hazijathibitishwa rasmi zinazosema kuwa mtangazaji huyo atakuwa akilipwa shilingi milioni 5 kwa mwezi.

Kama tetesi hizo zitakuwa na ukweli, Gadner atakuwa mtangazaji wa radio anayelipwa pesa nyingi zaidi nchini.

Kipindi chake kinatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na kipindi chake cha zamani, Jahazi cha Clouds FM ambacho kwa sasa huendeshwa na Arnord Kayanda, Wasiwasi Mwabulambo na Ephraim Kibonde.

Hata hivyo Clouds FM watakuwa na advantage katika mikoa mingine ambayo Times FM haisikiki.

Kwa upande wa Dar es Salaam, Maskani ina nafasi kubwa ya kuchukua wasikilizaji wengi wa Jahazi hasa wanaosikiliza radio wakiwa majumbani.

Times FM wana disadvantage ya frequency walinayo ya 100.5 ambayo gari nyingi haizifikii na hii ni kwasababu kuna wasikilizaji wengi jijini Dar es Salaam wanaosikiliza radio kwenye magari.




Picha ya pamoja ya baadhi ya watangazaji wa Times FM. Kutoka kushoto ni: Gadner, Schola, Natasha, Ndimbo, Dida na Joet.




 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates