Home » Archives for 08/28/12
KIRAKIRAMI FT BIZZO RHYMES -NAZISAKA DOOH MP3
7:14 AM
•
kirakirami |
Artst: kirakirami ft bizzo rhymes
Studio: B-records....
Producer: suma kopa
Kim Kardashian atupa nguo zake zote sababu ya Kanye West
6:51 AM
•
Kanye West anamtaka mpenzi wake Kim Kardashian avae mavazi ya heshima na ya kuvutia.
Katika kipindi cha jana cha Keeping Up With the Kardashians,
rapper na mbunifu huyo wa mavazi, 35 – ameweka deal na mpenzi wake huyo wa
miezi mitano kuwa kama atazitupa nguo zake zote atamnunulia zingine.
USIKU WA SAUTI ndani ya mikoa 4 Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Zanzibar.
6:45 AM
•
Na
mwandishi wetu:
KIONGOZI
wa zamani wa bendi ya Diamond Sound ‘Dar es Salaam Kibinda Nkoi’, Ibonga
Katumbi ‘Jesus’ mwezi ujao ataungana na baadhi ya wanamuziki wengine wa kundi
hilo katika onyesho la Usiku wa Sauti na Marafiki wa Kweli litakalofanyika
katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Zanzibar.
Akizungumza
mjini Dar es Salaam jana, mratibu wa tamasha hilo Martin Kadinda ‘Single
Button’ alisema onyesho hilo linahusisha wanamuziki wakongwe ambao wataungana
na Jesus pamoja hao wa Diamond.
“Kila
kitu kinaenda sawa aliyekuwa amealikwa kwenye onyesho ni Jesus lakini katika
onyesho hilo atatakiwa kuimba nyimbo zake kadhaa ambazo alitamba nazo akiwa
Diamond na Beta Musica kwa hali hiyo alishauri aite wenzake ili wamsindikize.
“
Kutokana na heshima walijengeana wenzake walikubali kumsindikiza, kwa hiyo
mashabiki wa Kibinda Nkoi baada ya miaka 12 wataweza kuwaona tena Ibonga
Katumbi, Richard Mangustino, Wayne Zola Ndonga na Alain Mulumba Kashama
wakisimama pamoja na kuimba tena nyimbo zao kali,” alisema Kadinda.
Kadinda
alisema lengo kubwa la onyesho hilo ni kuthamini muziki wa zamani na kufundisha
matumizi ya vyombo vya muziki.
Katika
onyesho hilo pia watakuwepo wapiga magitaa kama Elly Chinyama, Adolph Mbinga,
Marcis Mengi na mpiga drum wa mwisho kuipigia Diamond Sound Kata Nyama
Serikali.
Baadhi ya nyimbo
zitakazopigwa katika onyesho hilo ni pamoja na Neema, Mugheni, Chance, Jetou,
Bana Beta, Midabwada na Infarouge.
Kadinda alisema wanamuzki wengine watakaoshiriki kwenye onyesho hilo
wataendelea kutangazwa.
THE MAKING OF PAIN KILLER by C-SIR MADINI
6:43 AM
•
C-sir Madini
amemaliza kushot kichupa cha wimbo wake mpya ambao unatarajiwa kutoka
mwezi ujao unaoitwa PAIN KILLER. Audio ya wimbo huo imetengenezwa na Kid
bwoy wa Tetemesha Recordz, na video imetengenezwa na Adam Juma wa Next
Level, na katika video hiyo C-sir amevalishwa na Kidoti Fashion ya
Jokate. Fans kaeni tayari kwa ujio huu mpya wa C-sir Madini.
Audition ya Maisha Plus 2012 yaanza
6:40 AM
•
Awamu ya
kwanza ya zoezi la kwasaka vijana
watakaoweza kumudu mchakamchaka wa shindano la Maisha Plus, imeanza jana
(Agosti 27) huko Bagamoyo mkoani Pwani.
Leo shindano
hilo litafanya usaili katika wilaya ya Lushoto ambako zoezi hili litafanyika
katika maeneo ya mjini mwa wilaya hiyo.
Baada ya
hapo ratiba za audition zitaendelea kama ifuatavyo;
Agosti 29- Kilimanjaro/ Sanya juu
Usaili
utafanyika katika mji wa Bomang’ombe
Agosti 30- Arusha/ Ngorongoro
Usaili
utafanyika Karatu
Agosti 31 – Singida
Usaili
utafanyika Singida Mjini
Septemba 1- Iramba
Usaili
utafanyika Iramba Mjini
Septemba 2- Dodoma
Usaili
utafanyika Kondoa Mjini
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)