Jason Derulo akiperform nchini Rwanda

6:39 AM
juzi mwanamuziki wa Marekani Jason Derulo alitumbuiza kwenye uwanja wa Amahoro nchini Rwanda kwenye fainali za shindano la Primus Guma Guma SuperStar. Hizi ni baadhi ya picha za show hiyo.


Sinta na Nyoshi El Sadaat kuja na ‘The Return of JLO'

6:35 AM

Mwanadada Sinta na mwanamuziki wa kundi la Fm Academia, Nyoshi El Sadaat wanakuja na filamu iitwayo The Return of Jlo.
Filamu hiyo inayoongozwa na muongozaji maarufu wa kampuni ya Steps Entertainment, Selles Mapunda itaingia sokoni mwezi September, 2012.
Kupitia website yake, Sinta ameandika:
“Jumamosi saa nne na robo usiku ndio itakuwa habari ya mujini pale movie yangu ya the return of jlo itakapoanza vibweka vyake katika station yako ya star Tv.Ni vipande tuu,mpango mzima ni mwezi wa tisa, si ya kukosa ikiingia madukani maana I’m back like  never went. Saa ni saa nne na robo usiku.Star Tv  na Sauda mwana wa Mwilima.Glory be to God.
Sinta na Nyoshi wakiwa kwenye scene
Hata hivyo baadhi ya wasomaji wa website yake wameendelea kumkejeli kama ilivyo kawaida.
“Subiri tukusifie we mbwiga …..uzinduzi waufanyia hollyowood au kule kwenu kimara????? Kuchamba kwingi kushika mavi na usijidai baharia kumbe wajiharia, kuwa msomi kama unavyojinadi,” aliandika mmoja.
Selles Mapunda na Sintah
Mwingine alisema,”Dah kweli wewe u r not creative, bingwa wa kucopy paste sasa hivi atamwambia baby yake amnunulie nyumba iliaoneshe kwenye tv, kubwa jinga hili limama linaloshindana na watoto.”

Ben Pol alijua ‘Baadaye’ ya Ommy Dimpoz itakuja kuwa hit

6:21 AM


Mara nyingi wasanii hupata fursa ya kusikiliza nyimbo za wenzao zinapokuwa kwenye hatua ya kutayarishwa.
Ben Pol aliusikia wimbo wa Ommy Dimpoz kabla hata ya kutoka na kumwambia kuwa utakuja kuwa tishio.
‘Unakumbuka niliwahi kukuambia kuhusu 'Baadae ,ona bro ,sasa nchi yote inaimba 'Baaadaeee eeeh'...hongeraaaa!!!,” ametweet Ben Pol kumwambia Ommy Dimpoz.
“Nakumbuka broo thanxxx,” alijibu Ommy.
Baadaye ni wimbo wa pili wa Ommy Dimpoz kufanya vizuri baada ya kuhit pia na wimbo wake wa kwanza, Nai Nai aliofanya na Ali Kiba.
Katika hatua nyingine Ben Pol amekuwa msanii wa kwanza Tanzania kuzungumzia habari ya msanii maarufu wa Marekani Frank Ocean kujitangaza kuwa ni shoga.
“Frank ocean anatuweka watu kwenye wakati mgumu ,ametoa album kali huku amejitangaza kuwa yeye ni gay ,kumuacha kumsikiliza nayo ni ishu,da!” amesema.
Hata hivyo hitmaker huyo wa ‘Nikikupata’ na mshindi wa tuzo za Kili, anaamini kuwa scandal hiyo haimpunguzii uwezo wake katika muziki.
“Haishushi ,ila bado wabongo sisi hatuwaelewi mashoga (mimi mbongo pia) ,ameni-dissapoint kidizain flani ,ila he's a gud singr/writer.”
Album ya Frank Ocean, Channel Orange ilikamata nafasi ya pili kwenye chart ya Billboard 200 na nafasi ya kwanza kwenye Billboard R&B/Hip-Hop Albums chart, kwa kuuza kopi 131,000 katika wiki ya kwanza.
 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates