YANGA YAINGIA FAINAL KWA KUIFUNGA APR 1-0 KUKUTANA NA AZAM JULAI 28

3:11 PM
mfungaji wa goli la yanga hamis kiiza



kikosi cha yanga

said bahanuz





Iddi Azan: Bodi ya filamu imelala usingizi

2:22 PM



Mbunge wa Kinondoni Iddi Azan ameiponda bodi ya filamu nchini kuwa imelala na hivyo kushindwa kufanya kazi yake.

Akichangia hoja bungeni kwenye mjadala wa  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, amesema zipo filamu nyingi zinazoingia nchini zenye mambo machafu lakini hazichukuliwi hatua yoyote.

Amesema kuna mtindo umekuwa maarufu sana nchini wa kuingizwa kwa filamu za ngono zilizotengenezwa nje lakini makava yake yakiwa na picha za wasanii wa Tanzania.

Mbunge huyo ametaka apewe maelezo ya kutosha kutoka kwa wizara hiyo kama wasanii wa Tanzania wanaoonekana kwenye makava hiyo ndio waliocheza movie hizo.

Lisa Jensen akijitambulisha miss world

2:19 PM
Mwaka huu kwenye shindano la Miss World, Tanzania inawakilishwa na aliyekuwa mshindi wa tatu kwenye Miss Tanzania 2006 Lisa Jensen.
Shindano hilo litafanyika nchini China.
Katika video yake ya kujitambulisha iliyowekwa kwenye akaunti ya Youtube ya Miss World anasikika akisema, “I am raising three beautiful children back at home.” Ni sentesi ambayo imeanza kuleta mkanganyiko. 
“Did she say she is raising three children?” ni ujumbe ulioandikwa chini ya video hiyo na mtu aliyeiangalia.
Sentesi hiyo inaleta mkanganyiko kwakuwa haieleweki kama anaamaanisha analea watoto watatu wa kwake mwenyewe ama wadogo zake, ndugu zake, watoto yatima ama!!

Godzilla auponda mfumo wa elimu Tanzania

2:10 PM



Rapper mwenye swagga za 50 Cent, Godzilla ameukosoa mfumo wa elimu uliopo nchini ambao anadai hautengenezi wataalam. Kupitia mtandao wa Facebook, Godzilla ameandika:

Mfumo wa Elimu Tanzania inabidi ubadilishwe. Elimu ndefu sana na haiko katika kutengeneza wataalam(Experts).

Mfano mtu kasoma hadi darasa la 7 akafeli na mtu aliyesoma hadi Form6 akafeli wote wanakuwa sawa coz hawaajiliwi #so miaka yote imepotea bure.

Zamani kulikuwa hadi na la 4 la mkoloni wazee wakifika la 4 wanamaliza sa hivi aje wazee?!

Fanyeni mfumo mzuri wa Elimu ili tuwe na wasomi wengi.

Mawazo mazuri Godzilla.

Updates:IGP wa Uganda aamrisha passport ya Chameleone irudishwe haraka

2:08 PM

Mkuu wa jeshi la polisi nchini Uganda,  IGP, Kale Kayihura amewaagiza maofisa wa Tanzania kuirudisha haraka passport ya Jose Chameleone.
Kayihura ametoa amri hiyo alipokutana na Chameleon kwenye kituo cha polisi cha Muyenga mchana wa leo jijini Kampala.
Amesema maafisa wa hapa nchini wamesema passport ya msanii huyo ingewasili baadaye leo na kukabisdhiwa kwake mara moja.
Leo Jose Chameleone akiwa na mashabiki wake wameandamana kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Uganda kudai arudishiwe passport hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na Erick Shigongo kwa madai kuwa meneja wake amemtapeli dola 3500.

HIKI NDICHO ALICHOANDIKA JOSE CHAMELEONE KWENYE FB YAKE KUHUSIANA NA TUHUMA ZA ERIC SHIGONGO KUSHKILIA PASSPORT YAKE!

2:05 PM
Picture

HAYA NDIO MANENO 240 ALIYOYASEMA DIAMOND PLATNUMS KUMALIZA MJADALA NA BABA YAKE

2:03 PM

.
Baada ya stori kuandikwa kwenye magazeti kwamba Staa Diamond Platnums anadaiwa kumtelekeza baba yake na hamjali wala hataki kusikia stori zake, hii ndio kauli ya Diamond kuhusu hiyo ishu.
Amesema “kiukweli ni vitu ambavyo mimi vimenishangaza sana kwa sababu sijui chochote nakuja kukuta tu kwenye magazeti, na nisingependa nisikie swala la mzazi wangu kusema mimi ni mtoto wake sijui nini na nini kwamba mimi nafanya starehe sihusiki na yeye sio kauli nzuri kiukweli, ina maana ananijua kwamba mimi ni mwanae baada ya kuwa DIAMOND”

Kwenye line nyingine Diamond amesema “siku zote kama alijua mimi ni mtoto wake basi angenisomesha na kunipa elimu nzuri lakini siku zote nilihangaika na Mama yangu mzazi akanikuza na kunisomesha kwa shida na tabu zote mpaka leo nimekua hivi, nisingependa kumsikia mtu yeyote anaongea kwamba mimi ni mtoto wake au yeye ni nani kwa sababu siku zote hawakuonekana, wasitake kuonekana kipindi cha Maslahi mtu ndio anajifanya anahusika sana na mimi kama mtoto wake”

“Haya mambo nilianza kuyasema toka natoa single ya binaadam sikujua hata kama leo ningekuja kuwa na Prado, makazi au kuwa na haya mafanikio mengine, baba yangu ataendelea kuwa baba yangu tu ila siwezi kumpa kipaumbele kama ninachompa mama yangu kwa sababu kama angetaka hilo angenijali toka mapema” – DIAMOND.

Kwa kumalizia, Diamond ambae mpaka sasa ametumia zaidi ya milioni 69 kujenga Nyumba yake Tegeta Dar es salaam amesema “mimi nilikua napenda kusoma na nilikua nafanya vizuri kwenye masomo yangu lakini sikua na uwezo wa kifedha kuendelea kusoma, mzazi wangu alikua na pesa ina maana angenijua mimi angenisomesha leo ningekuja kuwa hata mbunge au hata waziri kwa sababu mi najua nina upeo mkubwa sana wa kielimu na vitu vingine, sasa nimesota na muziki alafu leo ndio wanajitokeza, SITAKI WANIACHE NA MAMA YANGU MZAZI
 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates