Monday, July 16, 2012 Utoaji wa Tunzo, kwa Filam Zilizoshinda katika Tamasha la ZIFF la 15 katika viwanja vya Ngomekongwe.

1:35 PM

ay, July 16, 2012

Utoaji wa Tunzo, kwa Filam Zilizoshinda katika Tamasha la ZIFF la 15 katika viwanja vya Ngomekongwe.

 
 MC  Farouk akitowa  utaratibu  wa Usiku wa Utoaji wa Tunzo za ZIFF, uliofanyika katika ukumbi wa Ngome Kongwe Usiku wa jana.    
 Wanafunzi wakisoma Utenzi wa Utoaji wa Tunzo kwa Filam Bora katika Tamasha la ZIFF la 15 

Waziri  wa Habaru Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbaruok, akitowa hutuba  katika sherehe za Ufunganji wa Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar lilofanyika katika Viwanja vya Ngome Kongwe Forodhani na kuitangaza Zanzibar Kiutalii kupitia Tamasha hilo la 15 la ZIFF.

 Mkurugenzi wa ZIFF akiwatambulisha wafanyakazi wa  Tamasha hilo wote wakiwa ni Wazanzibar waliofanikisha Maonesho ya Tamasha kwa sekta zote katika kipindi chote cha maonesho hayo.
Wafanyakazi wa Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar ZIFF, vijana wa Kizanzibar  wakiwasalimia Wananchi waliofika katika sherehe za ufungaji wa Tamasha hilo.    
Mkurugenzi wa Kampuni ya ZUKU, akitowa salamu za Kampuni yake kuweza kufanikisha Udhamini wa Tamasha hilo uliofanywa na Kampuni hiyo.  
Mtayarishaji wa Filam ya UHLANGA kutoka Afrika ya Kusini Ndaaba Ka Ngawane, akitowa shukrani kwa kupata ushindi wa Filam yake na kupata ushindi wa jumla kupitia Filam hiyo
 Mtayarishaji  wa Filam ya LUHANGA kutoka Nchini Afrika ya Kusini akiwa na Vijana wake baada ya kukabidhiwa Tunzo yake, na kuibuka mshindi wa Jumla kwa kukusanya Tunzo nyingi katika Tamasha la mwaka huu la 15, kwa ubora wa kazi yake kupitia Filam hiyo.

Mshindi wa Tunzo ya Filam ya Ruhago kutoka Nchini Rwanda Mbabazi Aime Philbert akitowa shukrani kwa ushiindi wa filam yake baada ya kukabidhiwa tunzo yake. 
 Waheshimiwa wakifuatilia vijana wakisoma Maulid ya Home wakati wa utoaji wa Tunzo za ZIFF.
 Vijana wa Mtaa wa Mtendeni wakisoma Maulid ya Home katika Usiku wa Utoaji wa Tunzo za ZIFF kwa mwaka 2012
 Watayarishaji na Wadhamini wa Tamasha la ZIFF wakipiga picha za kumbukumbu ya Tamasha la 15 wakati wa Vijana wa Maulid ya Home wakisoma katika Jukwaa la ZIFF la Ufungaji.
 
Mtayarishaji wa Filam ya ZAMORA kutoka Zanzibar Shamis Bhanji akifurahiya Tunzo yake baada ya kukabiidhiwa kwa kuwa Filam bora kwa Nchi za Afrika Mashariki.
Mwakilishi wa Kampuni ya ZANLINK akiwa na furaha baada ya kukabidhiwa Cheti cha kufadhili Tamasha hilo kwa Muda wa Miaka Kumi kutowa huduma ya Internet kwa kipindi chote  cha Tamasha.



Wasanii wa Kikundi cha 6B wakionesha umahiri wao wa kucheza  muziki wa aina yote , wakilishambulia jukwaa katika sherehe za ufungaji wa Tamasha hilo.

HAWA NI BAADHI YA MA CELEBRITY WETU BONGO WAKIWA NA WATOTO ZAO.

1:29 PM


JCB akiwa na mtoto wake wa Kiume

Chindo Man aka Mbwa akiwa na mtoto wake

Nikki Mbishi akiwa na mtoto wake wa kiume

Raque kutoka I-View Media pamoja na mkewe wakiwa na mtoto wao wa kike 

Mike T na mwanae wa kiume

Barnabas akiwa na mwanae wa kiume

Amini akiwa na mtoto wake wa kike

Gelly wa Rhymes na mtoto wake wa kike

Hapa ni Spac na JCB kutoka Kijenge ya juu Arusha wakiwa na watoto zao wakiume

Tunda Man na mtoto wake wa kike

Mwana FA na mtoto wake wa kike.

Zuku yakutana na watengeneza Filamu

1:18 PM
(Zanzibar, Julai 15, 2012). Zuku usiku wa kuamkia juzi  ilifanikiwa kuaanda warsha ya watengenezaji filamu kutoka baadhi za nchi mbali mbali, ambao wanahudhuria Tamasha la 15 ya Zanzibar International Film Festival ZIFF.
 
Kauli mbiu ya warsha hiyo ilikuwa “Kupandisha viwango vya ubora katika filamu za kiafrika”. Wadau hao walilenga kuangalia kwa undani majukumu  mbalimbali kuanzia kwa wawekezaji, watangazaji, na wazalishaji kwa lengo la kutoa ufumbuzi akinifu dhidi ya changamoto zinazoikabili sekta ya wachezaji katika Afrika.
 
Warsha iliyoendeshwa chini ya uenyekiti wa Firdoze Bulbulia, ilihudhuriwa na wasemaji mashuhuri kama Ayuko Babu ambaye ni mtaalam wa filamu za Afrika, Mahmoud Thabit Kombo, Mwenyekiti wa ZIFF,  na Hannelie Bekker kutoka Zuku.
Akitoa maoni yake kuhusu kauli mbiu mbele ya jopo hiyo , Hannelie Bekker, ambaye anasimamia vituo saba (7) vya; Zuku, alisema "Zuku itakuwa na jukumu muhimu katika kupandisha viwango vya ubora wa filamu za kiafrika kwa sababu inatoa nafasi kwa watengenezaji wa filamu na wazalishaji kuuza na kuonyesha bidhaa zao. Aidha, Zuku hasa ina nia ya kukuuza vipaji vya ndani na kutangaza kazi za wasanii wa ndani – na huo ndio jukumu msingi wa uwekezaji wetu na uhusiano na ZIFF. Tunahitaji filamu na tamthilia zenye bora na hii ina maana tuna maslahi ndio maana tunataka kuona sekta hii ikistawi.”
 
Ayuko Babu, ambaye pia alikuwepo kwenye jopo, alisisitiza haja ya watengenezaji wa filamu kujipanga na kufanya kazi pamoja ili kuboresha hali ya sekta ya  filamu. Aidha alisisitiza haja ya kusaidia na kuimarisha ZIFF.  "Zanzibar ni mahali pazuri na kila mtu anaifahamu hivyo kwa hiyo kuna umuhimu  kwa kila mtu kujua kuhusu hilo na ZIFF ina fursa ya kukua kama matamasha mengine ya kimataifa kama vile Cannes na Ouagadougou." Pia alizitaka watengenezaji wa filamu kufikiri kwa makini kuhusu mifano ya biashara yao ili kuhakikisha kwamba wanapata faida na wanahakikisha kwamba wanawapa watu hadhithi zinazoleta manufaa.
 
Mwakilishi wa wacheza filamu, Farida Nyamachumbe alizungumza kuhusu changamoto alizokabiliana nazo ndani ya sekta.
Jambo ambalo liliwavutia sana wasanii wa ndani ambao changamoto ya udhibiti, uwekezaji  na usambazaji ni sehemu yao ya kusaidia uwanda huu. Pamoja na changamoto hizo,Farida alisema anamatumaini katika ukuaji wa filamu za Bongo.
Mjadala huo ulihudhuriwa na watengenezaji wa filamu kutoka Rwanda, Afrika Kusini, Nigeria, Namibia, Kenya, Marekani, Sweden na wasanii wa filamu za Bongo.
 
Zuku ambayo ni kampuni ya TV ya kulipia ambayo inaendelea kukua kwa kasi inapatikana Tanzania, Uganda na Kenya, ina nia ya kudhamini ZiFF kwa kipindi cha miaka 10 kwa thamani ya jumla ya dola milioni moja.
Udhamini huo unatarajiwa kutoa  utulivu na msaada ambayo kwa upande utachangia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha sekta ya filamu, si tu nchini Tanzania lakini maeneo mengine ya Afrika.
 
Kingamuzi cha Zuku kinatoa wigo mpana wa uchaguzi wa burudani ka vile habari za michezo, sinema, makala na muziki. Hizi ni pamoja na chaneli tatu za  BBC World News, MTV Base, Setanta Sports, Fox Entertainment na E!. Zuku pia inatoa chanelli zingine kama Zuku AFrika, Zuku Life, Zuku Sports na Zuku Movies. Huduma hii patikana kupitia satellite mahali popote Tanzania
 

Kitila - Hali yangu {Official Video}

1:15 PM

OMMY LAX - Siwema (Official Video)

1:14 PM

Abamto - Sina Tatizo {Official Video)

1:12 PM

Diamonds - Liveshow Ziff (Zanzibar)

1:10 PM
Hivi ndivyo tulivyoingia kwenye steji katika show ya ZIFF (Zanzibar) tunawashukuru sana mashabiki kwa kutupokea vizuri. Kipande hiki cha video kimeletwa kwenu na www.thisisdiamond.com

JINSI YA KUWAPIGIA KURA BIBI BOMBA 2012

1:02 PM

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates