Video: Mdogo wake Barack Obama bado choka mbaya

1:27 PM

Mdogo wake na rais wa Barack Obama wa Marekani, George Obama bado ameendelea kuishi maisha magumu kwenye nyumba ya matope (slum) nchini Kenya.
“Nadhani ana familia yake mwenyewe,” alisema George Obama katika mahojiano na mwandishi Dinesh D’Souza.
“Mimi ni member wa familia yake lakini nina umri mkubwa, hivyo najisaidia mwenyewe,” mdogo wake na Obama alisema kwenye clip hiyo ya dakika nne iliyopo kwenye website ya Hollywood Reporter (www.hollywoodreporter.com).
D’Souza, mwandishi wa kitabu cha mwaka 2011 kilichouza sana “The Roots of Obama’s Rage,” alisema alimtafuta mdogo wake na Obama baada kumuona kwenye habari iliyomwonesha akiishi kwenye kijibanda jijini Nairobi.
Alipoulizwa na mwandishi huyo iwapo kaka yake ameshindwa kumsaidia George Obama alijibu: “Ana mambo mengine ya kushughulikia.”

“He’s taking care of the world, so he’s taking care of me.”

Chanzo cha kifo cha mama yao P-Square chabainika

1:24 PM
Sababu ya kifo cha Josephine Okoye,mama wa nyota wa muziki wa R & B nchini Nigeria wa kundi la Psquare, Peter na Paul imejulikana.
Maelezo ya msemaji wa Psquare yamesema mama yao alifariki saa chache baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo nchini India.
Mrs.Okoye alipelekwa nchini India kwaajili ya kufanyiwa operation baada ya kukaa katika hospitali ya St.Nicholas  ya nchini Nigeria kwa muda, ambayo ni miongoni mwa hospitali ghali nchini humo.
Wakati huo huo, watu maarufu wamekuwa wakimimika kwenye nyumba ya kifahari ya P-Square iitwayo Square Ville, kuungana na ndugu na jamaa kwenye msiba huo.
Pamoja na watoto wanne aliokuwa nao, Mrs Okoye ameacha mjukuu mmoja kutoka kwa Peter Okoye aliyezaa na Lola Omotayo.

Taylor Swift ndiye msanii (under 30) anayelipwa zaidi, anafuatiwa na Justin Bieber, Rihanna

1:22 PM
Wanamuziki wa Pop wa kike wakiongozwa na Taylor Swift, Rihanna na Lady Gaga wametawala orodha mpya ya jarida la Forbes la maceleb wanaolipwa pesa nyingi zaidi wakiwa na umri wa chini ya miaka 30.
Swift, 22, amempiga fimbo Justin Bieber katika nafasi ya kwanza kwa kuingiza kiasi cha dola milioni 57 kwa mwaka hadi kufikia mwezi May mwaka huu (May 2011 – May 2012).
 
Mrembo huyo hulipwa dola milioni moja kwa kila concert anayopiga.




Bieber, 18, amekamata nafasi ya pili kwa kuingiza dola milioni 55 alizozipata kwa kuuza nyimbo, concerts na matangazo ya bidhaa kama lotion za Proactiv.



Rihanna, 24, amemzidi mshindi wa kwanza wa mwaka jana Lady Gaga katika nafasi ya tatu kwa kuingiza dola milioni 53.
Mwanamuziki huyo wa Barbados ameingiza hela hizo kutokana na albam yake ya “Talk That Talk”, tour yenye show 85 aliyofanya na matangazo kama ya  Vita Coco coconut water na Nivea lotion.



Gaga, 26 amekatama nafasi ya nne kwa kuingiza  dola milioni 52 chini sana ya dola milioni 90 alizoingiza kabla ya hapo.



Katy Perry, 27, na Adele, 24, wamekamata nafasi ya tano na sita kwa kuingiza milioni 45 kwa Perry na dola milioni 35 kwa Adele.

Adele
Muigizaji wa kike Twilight” Kristen Stewart, rapper Lil Wayne na waigizaji wa kiume wa “Twilight”  Taylor Lautner na Robert Pattison wamekamilisha list kwa kuingiza kati ya dola milioni 26.5  na milioni 34.5.


Kristen Stewart
Robert Pattison
Taylor Lautner 
Sababu ya wasichana kuongoza ni kutokana na wao kupata mikataba ya kufanya matangazo katika maeneo ya urembo, afya na fashion.

Justin Bieber anataka David Beckham awe kocha wa timu yake

1:21 PM


Justin Bieber anataka kuanzisha timu ya soka huko Los Angeles na anataka mchezaji wa kulipwa wa Uingereza David Beckham awe kocha wa timu hiyo.
Bieber mwenye miaka 18- anataka kufuata nyayo za Robbie Williams na Vinnie Jones kwa kuanzisha timu za soka.
Timu ya Robbie inaitwa LA Vale na wakati Vinnie ana timu mbili,Hollywood United na Hollywood Allstars.
Justin alisema: "Nimekuwa nikicheza soka sana katika miaka miwili ama mitatu mpaka sasa. Nimekuwa nikifurahia sana.
Aliendelea kuliambia gazeti la Daily: "Mtu mmoja tu ambaye tunataka awe kocha wa timu, naye ni David Beckham.


David Beckham
"Sio kwamba tutakuwa tukicheza mechi kila wiki. Kiukweli tutakuwa tukicheza game tatu ama nne kwenye msimu.”
"Ntamuomba David mimi mwenyewe naamini atakubali.
Justin aliongeza kuwa mpenzi wake Selena Gomez na mke wa David, Victoria Beckham nao pia wanaweza kuhusishwa kwenye project hiyo.
"Nitawaomba  Selena na Victoria kama watapenda kuwa  cheerleaders wetu! 
But hey, that might be pushing it,” alisema.

(Official video) BEN PAUL - MANENO

1:11 PM

AFANDE SELE ATOA TAMKO KUTOKANA NA FUJO ILIYOTOKEA ZANZIBAR MUSIC AWARDS

1:07 PM
 Mfalme sele ameamua kufunguka baada ya kukaa kimnya sana tangu siku ya tukio la zanzibar music awards ambalo walishindwa kupafom yeye na swahihiba yake 20percety na kusababisha fujo iliyo dumu kwa takribani nusu saa bwawani hotel na baadae kuhamia kituo cha police malindi.
Leo kwenye ukurasa wake wa FACEBOOK amefunguka  kama ifuatavyo tembea nayo....!!!!!
Salaam Ndugu zangu wote mashabiki na wadau wa muziki wetu!!
Tamko langu kuhusiana na lugha zilizotolewa na Twent Percent kuhusiana na show yetu ya Zanzibar Music Award.
"Tulialikwa kwenye ZANZIBAR MUSIC AWARD, na kabla ya kazi makubaliano yote ya kazi kwa mujibu wa mkataba yalifuatwa, makubaliano hayo yalihusisha sisi kujigharamia gharama zote za nauli na Malazi (accomodation).
Tulifika Zanzibar salama, tulipokua Zanzibar twenty alitaka agharamiwe huduma zote ambazo ni nje ya mkataba wetu, nikamuomba na kumsihi sana Ndugu yangu aheshimu mkataba, asitafute matatizo kwani tayari mpaka wakati huu tuna kesi na Halmashauri ya Manispaa ya Moro ambayo kimsingi sikuhusika (nilishatolea ufafanuzi siku za nyuma).
Lakini yeye alipingana na mimi, akanibishia na kunisukuma Mbele ya.......... wageni na wenyeji wetu, wakiwemo Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seiph Ali Idi, Waziri Seiph Khatibu.
Walikuwepo waadishi wa habari wa siku Nyingi Akiwemo Abubakari Liongo (idhaa ya kiswahili radio Ujerumani), Mkurugenzi wa ZENJI FM ndugu Tua Saidi Tua.
Mimi Selemani Abdallah Juma Msindi sihusiki kwa namna yoyote, na tabia zisizo za kuridhisha zinazoonyeshwa na Ndugu yangu Twenty Percent, ambae nimekua nae nyumbani kwangu hata kabla ya Tuzo zake Tano (Kili Music Award) ambazo kazi hizo zote hizo kaandikia nyumbani kwangu siwezi kuwa na tatizo nae ni ndugu yangu kiimani na kikazi, hata kazi yangu niliyofanya nae kabla siku za nyuma "MBELE YAKO NYUMA YANGU" .. Kuna mstari Nilisema " ..Kuandika Rhyme kwenda Gym kimtindo kuonyesha Ugum, bado unatakiwa uwe na nidhamu ya kweli, sio ya kumzuga Mwalimu, utajihukumu".
Nimekua nikisisitiza nidhamu kwa Ndugu zangu woote toka enzi za Ghetto BoyZ, Watupori na Mabwasha'Kingdom, ambao wengine hawafanyi sanaa, ila nipo nao kwenye Familia yetu kubwa hapa Tanzania. Nimesikitishwa na kitendo hicho. Siku zote nimekua mwenye kuhitaji suluhu kwa namna ya Amani.
Verry sorry kwa wote ambao mumefadhaika kwa hilo. Tuendelee kuwa pamoja na msisite kutoa ushauri wenu, maoni ili Game letu lisonge. MUNGU ATUBARIKI.
Asanteni sana.
Selemani Juma Abdallah Mutabhazi Msindi.
a.k.a Afande Sele (King of Rhymes)

WENGI HAWAMUELEWI ROMA MKATOLIKI

1:03 PM


HAHAHAHAHA UPEO WENU MDOGO SANA NARUDIA TENA UPEO WENU MDOGO MNO...NILIWAHI MWAMBIA DULLA WA PLANET BONGO KUWA AFTER TUZO MAISHA HUBADILIKA NA HATA UKIANDIKA KITU FLANI UTAAMBIWA KISA TUZO HAHAHAHA NDO HAYA SASA..WAKATI KUMBE B4 TUZO NILISHAWAHI ANDIKA STATUS HII HII(wanaonifatilia watakumbuka)NA KOMENTI NYINGI KAMA SIO ZOTE ZILINISAPOTI HAHAHAHAHA safi sana hii nimeipenda great challenge...NGOJA NIWAMBIENI KI2 HAKUNA SHABIKI MZURI KAMA HUYO NILIYEMTAJA HAPO...UNAJUA KUWA INDUSTRY YA FILAMU IMEKUZWA SANA NA MABEKI TATU?WAOO NDO MAJUMBANI HUPENDA KUTAZAMA BONGO MUVI NA KUSIKIZA MIZIKI YA KIBONGO YENYE TACHI KAMA BEST NASO, ROMA,AFANDE SELE,20 PASENTI, NA WENGINEO WENYE MLENGO HUO KAMA VINAPANDA BEI YA BLAD KEY(chunguza ndo uongee wana msipaniki tuu) NI NGUMU SANA KUKUTA BEKI 3 ANAMUELEWA KWIK RAKA, WAKACHA,(basi hapo pia mtasema nimewaDIS hahahahaha dah)...SO HAO NDO MASHABIKI WE2 NA HUYO BEST NASO NI MFANO TU WA KUWAKILISHA WASANII KAMA YY!! TAZAMA SHOW ZA BURE KAMA TIGO,EATEL NA VODA ZA VIWANJANI..UNADHANI WANAOJAA NI KINA NANI? MABEKI3,WATU WA BODA BODA,MAHAUS BOYZ,YANI WATU FLANI HIVI AMBAO HAWAWEZI KWENDA BILICANAZ AU MAISHA CLUB(chunguza)SIO WOTE BUT MAJORITY NAZUNGUMZIA!!!NA NDOMANA WASANII WA AINA HIZI ZA BEST NASO LAZIMA TUPATE SANA SHANGWE NA KUPOKELEWA POA KOZ NDO CHAKA LE2!!! sasa roma unipeleke kempisk kupiga show...hahahahahaha..nilishafanya show kunduchi na dj choka nakumbuka pale wet n wld...walijaa wahindi sana basi nilikuwa natazamwa tu hadi aibu!! bt nilikuwa muelewa kuwa lile sio chaka langu!!!ila yupo msanii ambae walimuelewa hao wahindi...bt msanii huyo huyo aliepokelewa na wahindi...nipeleke nae mbagala dar live sasa ndo utajua roma ni chaka lake au aje!!?SO HAO NDO WANYONGE TUNAOWAWAKILISHA KAMA MAANA YA KIDOLE CHA MWISHO!! PITIA PITIA WALINZI WOOOTE WANAOLINDA NYT AAAF KAGUA SIMU ZAO UTAKUTA NGOMA ZA WASANII GANI? SASA JE NIKISEMA ROMA ANAPENDWA SANA NA WALINZI NI MATUSI(aaaah tusizinguane hapa na uelewa wenu hafifu hamjui loloteeee kama ipo ipo tu!! aaaf hawa marafiki wanao sisitizaga roma ni add roma ni add plz ndo hawa hawa wanaletaga uduzanzi kwa uelewa wao mdogo!!...NA BLOCK TU SASA NIMEPANIKI DIZAINI!!) MWENYE SIKIO NA AMESIKIA NA ASIEJUA MAANA HAAMBIWI MAANA...SORRY NAISHIA HAPA

ROCK TF FORTEEN - NGUVU ZA KIUME

12:35 PM
Audio ni mkono toka mandev records zanzibar chini producer bujju video amesimamiwa na Canaone

HAMSHA POPO WANGARISHA VIDEO YA JOBFIRE

12:27 PM
jobfire

jobfire na hammer Q wakiwa location

jobfire
wadada wa nne wanao kimbiza dsm kwasasa kupitia unenguaji na u video modl wanao julikana km hamsha popo a.k.a watoto wa kariakoo wamehusika kwenye video ya msanii jobfire mkali a.k.a sauti za matukio akiongea na chiwile inc jobfire ameshukuru ushirikiano alio pata toka kwa akina dada hao " nimefurahishwa na kazi nadhani wadau watahamini mnacho sema video itapokua tayari"  alifunguka jobfire ambae yupo dsm kukamilisha video ya ngoma yake ya mchiriku inayo kwenda kwa jina la akiwa na Hammer Q
 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates