PICHA TANO ZA LOCATION YA VIDEO YA TIMBULO SAMSON & DELILA

1:05 PM
 Video yote chini ya ADAM JUMA (Next level)

Watu wenye tabia hii husababisha mapenzi kuwa magumu

1:04 PM



Mapenzi yamekuwa magumu. Ni mzigo mzito kuubeba. Yanaendelea kujeruhi wengi, bado ni mateso kwa wengine. Sasa hivi, asilimia kubwa ya watu inaamini kwamba kupata mwenzi sahihi wa maisha ni ndoto za alinacha. Ni kamari, ni bahati nasibu.
Maendeleo yamekuja na mambo leo. Kile kinachoonekana ni Uzungu, kimeathiri kwa kiasi kikubwa ustaarabu wetu. Mila na desturi zetu vimepokwa na utandawazi uliotujia. Hii inamaanisha kwamba uhusiano wa kimapenzi wa sasa, hauendani na sura ya utamaduni wetu.
Vijijini kuna unafuu japo na kwenyewe fujo zimeshaingia na mambo yameshabadilika. Mijini ndiyo matatizo yenyewe. Ulimwengu wa digitali na fursa za mitandao zinatutia wazimu. Tunataka kuiga mitindo ya maisha ya wenzetu, matokeo yake tunageuka watumwa wa mapenzi.
Hayakuletwa mapenzi ili yawaumize watu, yapo kwa ajili ya kutoa faraja ndani ya jamii. Yalivyo ni kwamba baada ya misukosuko ya kimaisha, vurugu mechi za kusaka riziki na mihangaiko mingine ya kimaisha, angalau unaweza kusahau yote unaporejea kwa mwenzi wako.
Hata hivyo, mapenzi hugeuka matatizo pale ambapo kazini umeondoka pakiwa moto, unarudi nyumbani nako pia unakuta moto. Unakosa sehemu ya kwenda kujishikiza. Faraja inaota mbawa. Hapa ndipo tafsiri ya mapenzi inapokosa mashiko. Jitazame, muangalie na mwenzako!
Japo ni ukweli usiopingika kuwa mapenzi siku zote hayapo tambarare hata kwa wenza waliostaarabika, ila katika kundi la mabrazameni na masistaduu ni mtihani. Kuna usemi kwamba glasi hugongana kabatini, nakubaliana nao lakini kwa makundi hayo ni pasua kichwa.
Mabrazameni na masistaduu ni zao la mapenzi ya Kichina, yaani uhusiano bandia. Inawezekana akiwa kwako akajilegeza kama amefika, kumbe anao wengine wengi. Hili ni janga zito kwa maisha ya sasa. Uaminifu haupo, uzinzi na usaliti vimekuwa fasheni ya kutukuzwa.
Wengine siyo masistaduu wala mabrazameni, wapo kawaida au pengine wana muonekano wa heshima mno. Hata hivyo, ukichimbua hulka zao ndiyo utachoka. Ni wakali wa kuwapanga foleni, akitoka kwa huyu anakwenda kwa yule. Mapenzi yametawaliwa na rangi ya Shetani.
Wapo wanaobadili wapenzi kwa sababu za tamaa, lipo kundi linaloamini miili yao ni mtaji wa kupata fedha, wengine shida za maisha zikasababisha uamuzi huo wa kujidhalilisha, wapo ambao ni tabia. Bila kugusa huku na huko hatosheki. Makundi yote hayo yamezingirwa na Ibilisi.
Mume wa mtu, anapewa sifa ya ‘uchapaji’ wa vidosho. Kwamba anajua kuwapanga kila kona. Nyumba za kulala wageni, anaingia kama nyumbani kwake. Yaani wanamjua, ni mteja wao hodari. Akifika, wanampeleka kwenye chumba anachokipenda.
Wapo wanaopiga simu, yaani namba za nyumba za kulala wageni zimejaa kwenye simu yake. Akijibiwa kwamba Sinza Kumekucha hakuna vyumba, anapiga Vatican, nako akikosa anajaribu Mori. Inahitaji sala na dua kuishi na mtu wa aina hiyo. Kuna mawili, kama hatakupa maradhi, omba usijue tabia yake, atakuua kwa presha..................

"PIPI" AONESHA TUMBO LAKE LENYE MIMBA

1:03 PM


Mwanamuziki wa kike nchini Tanzania PIPI

Tom Cruise ndiye muigizaji anayelipwa hela nyingi duniani

12:54 PM

Licha ya kuwa kwenye mchakato wa kupewa taraka na mke wake Kate Holmes, muigizaji wa Mission Impossible  Tom Cruise ametajwa kuwa muigizaji anayeingiza fedha nyingi zaidi duniani.
Kwa mujibu wa jarida la Forbes, Cruise ameingiza kiasi cha dola milioni 75 kati ya May 2011 hadi May 2012.
Amewapiku waigizaji wenzie Leonardo DiCaprio na Adam Sandler ambao wamekamata nafasi ya pili katika orodha ya waigizaji 100 wanaolipwa pesa nyingi zaidi.

Adam Sandler
Leonardo DiCaprio  
Cruise mwenye miaka 50 amefanikiwa kuingiza fedha nyingi kwa kufanya vizuri kwa filamu yake ya  “Mission Impossible – Ghost Protocol” iliyotengeneza dola milioni 700 kwenye majumba ya sinema.


DiCaprio na Sandler wamekamata nafasi ya pili kwa kuingiza dola milioni 37 kila mmoja.

Mcheza mieleka wa zamani Dwayne ‘The Rock’ Johnson amekamata nafasi ya nne kwa kuingiza dola milioni 36 baada ya miongoni mwa filamu alizoigiza Fast Five kuingiza dola milioni 626 za box office.

The Rock


Ben Stiller
Sacha Baron Cohen 
Mchekeshaji Ben Stiller amekamata nafasi ya tano kwa kuingiza dola milioni 33 huku Sacha Baron Cohen akifuatia kwa kuingiza dola milioni 30.
Wengine waliopo kwenye top ten ni Johnny Depp, 7, Will Smith, 8, Mark Wahlberg, na Taylor Lautner, 10.




Jonny Deep

Will Smith
Mark Wahlberg
Taylor Lautner

Wachezaji wanaounda timu ya kikapu ya US kwenye Olimpiki 2012

12:53 PM
Lebron James  
Kobe Bryant
Carmelo Anthony
Tyson Chandler
Deron Williams
Chris Paul
Kevin Love
Kevin Durant
Russell Westbrook

MwanaFA akerwa na makampuni ya simu kugeuza nyimbo kuwa matangazo

12:51 PM
mwana fa

Rapper Hamis Mwinjuma aka MwanaFA ameelezea kukerwa na mtindo uliopo sasa wa makampuni ya simu kugeuza nyimbo za wasanii kuwa matangazo na kuelezea kuwa ni ufinyu wa ubunifu.
“Ndugu makampuni ya simu,mashindano ya kubadili nyimbo za bongo fleva kuwa matangazo yenu yametosha sasa!fanyeni kubuni kitu kipya,ahsanteni!” ametweet leo.
MwanaFA siye pekee aliyechukizwa na kitendo hicho kilichokithiri kwa makampuni ya simu nchini.
Mtangazaji na mbunifu wa vipindi na masuala mbalimbali wa Clouds Fm Cindy naye pia ameonesha kusikitishwa na tabia hiyo.
"Salaam kwa kampuni zetu za simu, matangazo bila kutumia nyimbo na wasanii wa muziki yanawezekana kwa kuajiri ubunifu 'kidogo tu' katika utunzi wenu wa matangazo na njia za mawasiliano kwa jamii!!ni hayo tu,” aliandika kupitia Facebook.
“Inachosha kila mara kusikia nyimbo zetu zote nzuri zimebadilishwa kuwa na ujumbe wa tangazo... Mbaya zaidi ni kuona kampuni zinavyoigana kana kwamba hiyo ndio namna pekee ya kutangaza bidhaa/huduma zao...inanionyesha pia ufinyu wa ubunifu wao katika utoaji wa huduma zao!!!”
Aliongeza,If only zingekuwa ni original production and not the renditions of popular songs/artists performances...then that would be a step towards creativity in all this. Atleast get a vocalist, write an original music (creatively) n produce AN ORIGINAL musical ad with FRESH melodies...but NOT get a popular (over played) song, change lyrics (lazily uncreative) and produce a rendition of the original!! Can u imagine the original being on high rotation (played every now n then) plus the renditioned advert on probably every half an hour...dont know about any of u but I know that radio/Tv would lose my listenership.”
Cindy hakuishia hapo ambapo aliendelea kwa kusema, “Mental and emotional appeal goes way further than just a popular melody...it’s the msg thats left behind after the melody stops n another commercial comes in before a chain of other programming activities. Small research...go ask ten ppl who listened to the radio in the morning n ask them the msg they got from any of the copy music adverts... I did n I know what I gushin about!!!”
Miongoni mwa nyimbo za wasanii wa Bongo Flava zilizotumiwa kufanya matangazo ya simu ni pamoja na Hakunaga wa Sumalee, Nimpende Nani wa Diamond, Mgambo wa Juma Nature (Vodacom), Bongo Flava wa Dully Sykes (Tigo), Dushelele wa Ali Kiba na Ndege Mtini wa Ferooz (Airtel).

Facebook yaongeza icon ya mashoga kwenye timeline

12:48 PM


Baada ya mmoja wa waanzilishi wa Facebook Chris Hughes ‘kuolewa na mpenzi wake wa siku nyingi  Sean Eldridge huko New York City, Marekani, jumamosi iliyopita, mtandao huo maarufu wa kijamii umeamua kuanzisha alama ya kuonesha status kwa wapenzi wa jinsia moja.
Chris Hughes (Kushoto) na Sean Eldridge walipofunga ndoa jumamosi
Kwa kawaida wakati watu wanapobadilisha status kutoka single, engaged ama it’s complicated na kwenda 'married' kulikuwa na kiicon cha mwanaume akiwa na mwanamke kwenye timeline, lakini sasa hivi kuna alama imeongezeka ya mwanamke akiwa na mwanamke ama mwanaume akiwa na mwanaume.
Facebook banaaaaa!

Wema Sepetu ni mjamzito?

12:47 PM



So Wema Sepetu strikes again? This time sio kuhusu wedding dress tena na mipango ya harusi kama alivyosema last time. Sasa hivi kaja na jipya. We must admit that she is very good at teasing her followers on Twitter with controversial statements and unfortunately we all fall in her deliberate traps!
Okay weekend iliyopita kaja na jipya. “Am not in a good kabisa! hichi nachokihisi ndo chenyewe ama? Hehehhehhe,” alitweet.
Tafsiri ya haraka haraka kama ndo umekuta na sentensi hiyo mbele ni nini? Ofcourse, sisi pia tunafikiria hivyo hivyo unavyofikiria sasa, kwamba anahisi ni mjamzimto, what else?
Kama kawaida followers wake wakaingia kwenye mtego na maswali yakaanza, “Wema kipi tena?,” That’s what she wanted to hear right? “Shijuwiiiiiiii,” alijibu na kuchokoza maswali mengine yalioanza kumkera tena! “Hiyo ya Diamond au?,” akaulizwa na mtu mwingine, (Prank gone wrong Wema?). Hata hivyo alijikaza na kujibu, “Umetumwa?”
Baada ya kusikia Diamond kaingizwa kwenye mazungumzo akaamua kukaa kimya kama panya aonapo paka, na mada ikabadilika.
Katika hatua nyingine picha za hivi karibuni za Wema zinazomwonesha akiwa mweupe zaidi ya mwanzo, zimekuwa topic kwenye mitandao ya kijamii. Wengi wameoneshwa kutofurahishwa na mabadiliko hayo makubwa ya ngozi yake ambayo wanadai yametokana na mkorogo.
“Wema wa zamani alikuwa mzuri sana natural colour, kwa sasa hivi umekuwa una rangi mbaya ya ngozi.Naweza kusema inakaribia kufanana na ya Michael Jackson,” aliandika msichana mmoja aitwaye Mariam.
Msichana mwingine aitwaye Pauline alimtetea kwa kusema: “Hakuna aliyekamilika chini ya jua na siku zote embe tamu na lililoiva ndio linalotupiwa mawe.Kiukweli Wema ni mzuri ndio maana anafuatwafuatwa mara magazeti mara raia, hebu muacheni jamani mnamsema kwa mabaya tu ina maana huyo Wema hana jema hata moja?”
She looks beautiful though, doesn’t she?

Sam Saintfeit wa Ubelgiji kuwa kocha mpya wa Yanga

12:43 PM
Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ethiopia mbelgiji Tom Saintfiet ana asilimia zaidi ya 90 ya kuwa kocha mpya wa Yanga.
Kocha huyo pia alikuwa ameomba kuifundisha timu ya taifa ya Kenya, lakini huenda akaja Yanga kwakuwa amepewa dau kubwa zaidi.
“He applied for the Kenya National Team job, but it would seem Yanga have offered him big bucks,” aliandika kocha mwenye leseni ya level B kutoka UEFA, Tom Legg.
Tom Saintfiet aliyezaliwa tarehe 29 March 1973 alianza kuwa kocha akiwa na miaka 24 na kumfanya kuwa manager mwenye umri mdogo zaidi kwenye soka la Ubelgiji.
 
Kiongozi wa usajili wa Yanga, Seif Ahmed alithibitisha kuwa kocha toka Ubelgiji, Tom Saintfiet ni miongoni mwa wawili wenye nafasi kubwa kutua Jangwani.
Timu alizozifundisha
1997-2001 -    Lower Belgian Divisions
2000       -     F.C. Satelitte Abidjan
2002-2003 -   B71 Sandur
2002-2003  -  Stormvogels Telstar
2003-2004 -   Al-Gharafa Sports Club
2004       -     Qatar U-17
2005-2006 -  BV Cloppenburg
2006-2007 -   FC Emmen (Technical Director)
2008       -     RoPS
2008-2010 -   Namibia
2010       -     Zimbabwe
2010-2011 -   Shabab Al-Ordon
2011       -      Ethiopia

Picha kumi zinazochekesha zaidi Facebook 2011-2012

12:40 PM
Katika pitapita zako Facebook bila shaka ulishakutana na picha hizi kumi. Ni picha maarufu sana kwenye  mtandao huo wa kijamii na mara nyingi bado zinaendelea kuonekana kutokana na watu kuzishare.


Picha zenyewe ndo hizi.



1. Jamaa aliyeamua kupunguza 'upwilu' kwa kufanya mapenzi na mbuzi! What a shame!
2.Afande Sele alipoamua kubaki na kiboxer tu
3.Maustaadh hawa walipoamua kung'oana jino kibabylon
4. Asiyefanya kazi na asile
5. Hii ndo hali halisi
6. Kibonde the birthday bway!
7. Loser to pay, winner to stay ndo mpango
8.Nichumu mwaaaaaa!
9. Radio inapomeza kanda
10. Vp! Msosi bado tu?
 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates