BELLE 9- AMERUDI

1:49 PM

P-SQUARE SPEED 1800

1:18 PM


P square toka Nigeria wanalakutuambia wa Africa baada ya kutupia picha na Drake
Baada ya kumweka Rick Ross kwenye remix ya Beautiful Onyinye na kuhitendea haki, sasa wanajaribu kuona kama wanaweza kupiga ngoma na mwana YMCMB, Drake.

Haijathibitishwa rasmi lakini picha hii iliyowekwa kwenye page yao ya Twitter inaashiria kuwa very soon watapiga ngoma na Mbabe wa Chris Brown ambaye hivi karibuni alipiga chupa Brown na kukimbilia chooni..
Photo: P square toka Nigeria wanalakutuambia wa Africa baada ya kutupia picha na Drake
Baada ya kumweka Rick Ross kwenye remix ya Beautiful Onyinye na kuhitendea haki, sasa wanajaribu kuona kama wanaweza kupiga ngoma na mwana YMCMB, Drake.

Haijathibitishwa rasmi lakini picha hii iliyowekwa kwenye page yao ya Twitter inaashiria kuwa very soon watapiga ngoma na Mbabe wa Chris Brown ambaye hivi karibuni alipiga chupa Brown na kukimbilia chooni..

MAONI >>>
By DUPA the DJ

Hate it or Love it: Diamond anapiga hela jamani!

12:50 PM




Hivi kuna wiki umeshasikia inapita bila kusikia Diamond amepiga show sehemu? Huyu jamaa anapiga show mfululizo na hatudhani kama anapata hata muda wa kupumzika.
Halafu ukisikia amepiga show sehemu weka akilini kuwa hapo kaingiza si chini ya milioni nane,ndogo sana labda milioni tano. Akitoa gharama ndogo ndogo kama za kuwalipa dancers wake n.k, zinazosalia zote zinaenda kwenye akaunti yake mwanangu!

Akaunti inatuna tu. Na nasikia kijana alivyo mchumi kama mchaga, hata buku anaweza asikupe kudadeki! Kama demu akishoboka kwake akitegemea atapewa good times,asahau tu sababu ain’t nothing like that coz the money is going straight to the bank. Juzi kanunua mkoko mpya, kitu cha Prado ambacho kimemnyofoa kama 70 Tshs Milli! Damn! So hate it or love it this dude got cash!!

Jana tu alikuwa Morogoro kwenye show ya Wajanja ya Vodacom akiwa na Fid Q, Mabeste, Shetah,Ommy Dimples na Ney wa Mitego! Nasikia wameangusha show ya kali sana pande hizo na watu walikuwa nyomi balaa, si unajua show za bure!

Kabla ya jana, yeye na dancers wake wakiwa wametupia dress code ya kufa mtu, wamepiga show ya maana sana pande za Dodoma. And the ladies? Kama unavyoweza kuimagine, walikuwa hawakatiki stejini ili tu kumshuhudia kwa karibu mchizi na wengine hawakuna  soo  kuomba japo busu tu! Dah.

Cheki baadhi ya picha za show zake wiki hii.

'Nishike japo mkono tu jamaani'
'Nichumu baasi'
Mashalaa!
'Unasema!'
Nyomii


Mfahamu Octopizzo rapper aliyezindua condom zake

12:46 PM





Kuna wale ambao sasa hivi nchini Kenya wanamuona kama rapper bora kabisa kuliko wote. Kila ngoma anayotoa inamsogeza zaidi kwenye kulimiliki taji la king wa rap wa Kenya. Kijana huyu anatishia nafasi za wakali kama Collo na Abbas kwenye hip hop ya nchini humo.
Kwa sasa amekuwa gumzo nchini Kenya kwa kuzindua condom zake ziitwazo ‘let’s do it.



Kwa wale ambao wameshazitumia wanasema zimewapa mizuka ya ajabu. Kinachofurahisha ni kuwa condom hizi zinatoa mwanga ama zinawaka gizani.


Leo kupitia Twitter amesema condom hizo zitaingia sokoni hivi karibuni, "the first stock should be here in a months time what will take time is formalitiz and ish."
Anaamini kuwa katika dunia yale leo si rahisi kumwambia kijana aachane kabisa na ngono ili kuepuka virusi vya HIV hivyo ni afadhali kama wakitumia condom. Leo (June 28) ametweet, “in the 21st century telling a teenager or a 21yr old to abstsin ni ka kudial 555 and telling zack "we not brunging yu home"

OCTOPIZZO NI NANI?

Ni msanii wa hip hop kutoka Kibera, eneo maarufu sana jijini Nairobi wanapoishi watu wa hali ya chini kabisa, akina kajamba nani (the largest slum in Africa).

Ni mhasisi wa kundi la vijana liitwalo Y.G.B. (Young, Gifted, and Black), likiwa na rapper wenye vipaji, watunzi wa mashairi, wachoraji, wasanii wa graphics na dancers.

Alizaliwa mwaka 1987, kwa jina la HENRY OCHIENG. Amesoma shule ya msingi na sekondari hapo hapo Kibera pamoja na St. Mary's Changamwe College mjini Mombasa,kabla ya kurejea Nairobi kujaribu bahati yake ya muziki.

Akiwa na Prezzo

Ni mtoto wa kwanza kwenye familia yao ya watoto wanne na pia ni baba wa mtoto mmoja wa kike aitwaye Tracy.

Akiwa na umri mdogo kabisa Octopizzo alifunzwa na maisha magumu ya Kibera lakini kuvutiwa kimuziki na wasanii kama Chino XL, Big L, KRS, Diabolic, EPMD, Copyright, CL Smooth, Immortal Technik, na Supernatural.
Ameshinda mashindano kibao ya freestyle nchini Kenya, kama G Pange Hip Hop Challenge, Hip Hop Halisi Freestyle Challenge, na Usanii Kona Hip Hop Challenge.



Octopizzo ameshapanda kwenye stage moja na wasanii wa kimataifa kama Dead Prezz (U.S.A.), Black Twang (U.K.), DJ Trouble Maker (U.S.A.), Bunt Face (U.S.A./Ethiopia), Malikah (Lebanon), Le Melanina (Colombia), Mad Maxamon (Germany), Restley Perez (Philippines), na Anne Khan (Germany). Na pia ameshaperform na wasanii wa Kenya wakiwemo Jua Cali, Nonini, P Unit, Wahu, Wyre, Jaguar, Jimmy Gait, Ukoo Flani, Point Blank, Mwafrika na Ness.
Mpaka sasa amesharekodu mixtape tatu, S.O.N. (Stragglers of Nairobi), Y.G.B. (Young Gifted and Black), na The White Shadow. Mwkaa 2008 S.O.N. ilikuwa mixtape iliyouza zaidi katika historia ya hip hop ya Kenya.



Pamoja na muziki, Octopizzo ni mwenyekiti mtendaji wa Chocolate City (Kibera) Tours na mwenyekiti na mwanzilishi wa Y.G.B. (Young, Gifted, and Black)

Pia ni muigizaji na ameshaonekana kwenye show ya MTV SHUGA msimu wa pili.

Mafanikio yake ya haraka kwenye muziki yaliwafanya baadhi ya watu kumzushia kuwa ni mwanachama wa ‘Illuminati’, chama cha siri kinachomuabudu shetani.

Lakini watu hao wameshindwa kutambua namna msanii huyo alivyotoka mbali katika harakati zake za kutafuta maisha aliyonayo leo. Kipaji chake cha uandishi wa mashairi wenye ubunifu mkubwa, ubunifu wake katika ujasiriamali na uvumilivu ndivyo vimemfikisha hapo alipo.




Kwa uwezo wake, Octopizzo ana mustakali wa nguvu kwenye hip hop ya Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla. Anawaacha na fundisho vijana wanaopenda kufanya hip hop na kufanikiwa kama yeye, kuwa wanapaswa kufikiria zaidi ya kutoa ngoma na kupeleka radio. Wana uwezo wa kufikiria miradi ya kufanya na kuisaidia jamii wanayoishi kwa kujituma kuiletelea maendeleo na kuiweka kwenye ramani kwa kuitangaza kimuziki.






Ufahamu mjengo wa P-Square – Square Ville

12:41 PM



Mitandao ya burudani nchini Nigeria inadai kuwa kupata kiwanja kwenye maeneo ya Omole (Ikeja, Lagos) nchini Nigeria ni Naira milioni 100 ambako ndiko nyumba ya P-Square waliyoipa jina la Square Ville ilipo. 

Hizo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni 900 za Tanzania.  Mingine inasema kuwa ukiiangalia nyumba yenyewe gharama yake ya haraka haraka ni zaidi ya dola milioni 2 za Marekani ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 3.1 za Tanzania, Damn!
Eneo la swimming pool
Sebule mojawapo



Awali nyumba hiyo inajengwa watu walipiga hesabu na kubaini kuwa imegharimu naira milioni 300 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 2 na kitu. Wakati huo vitu vya ndani vilikuwa havijawekwa bado.

Square Ville ina bwawa la kuogelea, sebule sita, master bed rooms kumi n azote zikiwa na furniture za nguvu na mengine ambayo si lazima kuyataja.
Dah! P-Square wako mbali sana jamani!


Akon alipowatembelea March mwaka huu (angalia hizo tuzo nyuma yao)
Welcome to Square Ville

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates