DOGO JANJA AFANYIWA KISOMO KABLA YA KUTOA NGOMA MPYA..

1:36 PM

dogo janja akiongea na clous tv

 Unaweza usiamini lakini huu ndiyo ukweli, Siku chache baada ya kutua Bongo na kujiunga na kampuni ya Mtanashati Entertainments ya jijini, nyota wa Bongo Fleva , Abdul Abubakar Chande ‘Dogo Janja’ mwishoni mwa wiki iliyopita alisomea kisomo maalumu cha kuomba Mwenyezi Mungu amnyooshee mambo yake pindi atakapoanza kushusha ngoma mpya.
 Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kisomo hicho kichoshudiwa na Teentz.com, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Ostaz Juma na Musoma alisema kuwa wameamua kumfanyia kisomo hicho kwa lengo la kuweka kazi zote za Dogo janja mikononi mwa Mungu kwa kuwa wana amini wao watu ambao wajafurahishwa na mpango mzima wa dogo huyo kurejea Bongo.

“Ni wazi kuwa wapo watu ambao hawajafurahishwa na kurejea kwa Dogo Janja, na kama unavyojua binadamu wana hila zao ndiyo maana tumeamua kufanya kisomo hiki ili kila kazi yake iwe kwenye mikono ya Mwenyezi Mungu” alisema Ostaz Juma na kuongeza kuwa tulichokifanya ni kwa ajili ya.....
Mungu hivyo basi watu wasidili maneno na kusema tumefanya ‘ kafara’ alimaliza Ostaz.
Katika hatua nyingine baada ya kumalizika kwa kisomo hicho jana (Jumapili) Dogo janja alifanya ‘shopingi’ ya nguvu kwenye maduka makubwa ya viwalo yaliyopo Mlimani City jijini Dar.
  
Katika shopingi hiyo Dogo janja alitumia zaidi ya shilingi Milioni 2.5 za kibongo kununua vitu mbalimbali, kama Seti 5 za viatu, Suti 4, Jeans 10, T shirt 10,miwani 5, simu aina ya BlackBerry, Laptop na vitu vingine kibao .
Huku akionekana mwenye furaha kubwa Dogo Janja aliiambia Teentz.com kuwa amefuahi kwa kiasi kikubwa kwa yale yote ambayo Ostaz Juma na kundi zima la Mtanashati kwa yote wanayomfanyia hivi sasa kwani hatakuwa na malipo mengine zaidi ya kuwafanyia kazi nzuri zenye kiwango.
“Nina furaha sana, hakika namshukuru Ostaz kwa yote anayofanya kwangu sina la kusema zaidi wasubiri ngoma za kweli zitakazokuwa kama shukurani kwao kwa sababu ndiyo kitu pekee ambacho naweza kukifanya kwao” alisema Dogo Janja.
IMEANDIKWA NA TEENZ.COM

J.I KUKINUKISHA MOMBASA

1:30 PM

BARNABAS NDANI YA DODOMA KWENYE USIKU WA SAUTI @Kilimani Club

12:40 PM

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates