KUKUSANYIKA NI HAKI YETU

12:22 PM







Kwa maana hiyo Jumuiya baada ya kushauriana na wanasheria itachukua hatua zote za kisheria za kumfikisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mahakamani kwa uvunjifu huu wa amani na ukiukwaji wa katiba unaofanywa na kikundi cha watu wachache wasioitakia mema Zanzibar na wanaotumia madaraka yao vibaya kwa maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma. Inaonesha kuwa kuna ajenda ya siri iliyokabidhiwa kikundi hicho cha watu wachache kilichoanza na Mh. Balozi Seif Ali Iddi ikafuatiwa na Mh. Mohammed Aboud (waziri katika ofisi yake) pamoja na kumuamuru Mh. Fadhil Suleiman Soraga na kumburuza katika uvunjifu huu wa amani. Sasa wameanza kujitokeza wakuu wa Mikoa kwa ajenda ya wazi kabisa ya kuvunja katiba ya Zanzibar na kuhatarisha neema ya amani iliyopo nchini.
JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU
(JUMIKI)
للجنة الدعوة الإسلامية
THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION
P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145- FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com
MKUNAZINI ZANZIBAR
Ref: JMK/OUT/VOL-12/2012
DATE: 09/05/2012
TAARIFA RASMI KWA VYOMBO VYA HABARI
TAMKO LA JUMUIYA YA UWAMSHO NA MIHADHARA
YA KIISLAMU ZANZIBAR TAREHE 09/05/2012.
DHIDI YA:
- MH: DADI FAKI DADI MKUU WA MKOA WA KASKAZINI PEMBA
- MH: TINDWA MKUU WA MKOA WA KUSINI PEMBA
- WAKUU WA JESHI LA POLISI KUSINI PEMBA (OCD NA RPC)
Kufuatia taarifa kupitia vyombo vya habari tarehe 08/05/2012 katika mkutano uliofanyika Jamuhuri Garden Wete wakati Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mheshimiwa Dadi Faki Dadi akizungumza na vikosi vya ulinzi na usalama, alipiga marufuku mihadhara inayosimamiwa na Jumuiya ya uwamsho na mihadhara ya kiislamu Zanzibar pamoja na kuzuia kutizama DVD za mihadhara kupitia masheha kufuatia tukio la Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mheshimiwa Tindwa akishirikiana na OCD na RPC wa Mkoa wa Kusini Pemba kuvunja mihadhara.
Ndugu waandishi wa habari tunapenda ifahamike kwamba Jumuiya ilifuata taratibu zote za kisheria na kufuata katiba ya Zanzibar bila ya kukiuka katika kusimamisha mihadhara hiyo.
Pili Jumuiya inasikitishwa sana kuliona jeshi la polisi likiburuzwa na wakuu wa mikoa hiyo wachache na kushiriki katika uvunjifu wa amani na ukiukwaji wa katiba. Tunashangaa sana wakati katiba ya Zanzibar imeweka wazi na kubainisha haki na uhuru wa kuabudu na kueneza dini kama ibara ya19 inavyoeleza “kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, wa imani… kazi ya kutangaza dini kufanya ibada na kueneza dini itakuwa huru… shughuli na uwendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi”. Kwa mujibu wa ibara hiyo mtu yoyote yuko huru katika suala zima la ibada na kueneza dini seuze Jumuiya iliyosajiliwa rasmi na vyombo vya dola nayo pia ina haki zote za kuitisha mihadhara makonagamano n.k anaeingilia kati shughuli za Jumuiya kuzizuiya huwa tayari amevunja katiba.
Kwa maana hiyo Jumuiya baada ya kushauriana na wanasheria itachukua hatua zote za kisheria za kumfikisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mahakamani kwa uvunjifu huu wa amani na ukiukwaji wa katiba unaofanywa na kikundi cha watu wachache wasioitakia mema Zanzibar na wanaotumia madaraka yao vibaya kwa maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.
Inaonesha kuwa kuna ajenda ya siri iliyokabidhiwa kikundi hicho cha watu wachache kilichoanza na Mh. Balozi Seif Ali Iddi ikafuatiwa na Mh. Mohammed Aboud (waziri katika ofisi yake) pamoja na kumuamuru Mh. Fadhil Suleiman Soraga na kumburuza katika uvunjifu huu wa amani. Sasa wameanza kujitokeza wakuu wa Mikoa kwa ajenda ya wazi kabisa ya kuvunja katiba ya Zanzibar na kuhatarisha neema ya amani iliyopo nchini.
Ndugu waandishi wa habari,
Jumuya inatamka wazi kuwa itaendelea kutumia uhuru wake wa kuabudu na kueneza dini kupitia mihadhara, makongamano n.k. Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar inavyoeleza pia inawataka Wazanzibar na Waislamu kwa ujumla wasiyumbishwe na watu wachache kwa taarifa zao binafsi wanazozitoa katika vyombo vya habari kwa maslahi yao binafsi na kutafuta umaarufu.
Pia Jumuiya inachukua fursa hii kuwanasihi viongozi hao kuacha kutumia madaraka vibaya na kuwakumbusha ibara ya 12 ya katiba ya Zanzibar “watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote” hivyo watawajibika kwa utumiaji wowote mbaya wa madaraka yao pia tunawakumbusha maneno ya Mh. Shein aliyoyasema katika jimbo la Koani “…endeleeni kuitunza amani ya Zanzibar aliyechoka na amani basi aondoke ahame kabisa atuachie…” TUPUMUE, huu si wakati wa kuwalazimisha watu muungano kuukubali au kuukataa watu wapewe uhuru wa KURA YA MAONI kila mtu aamue kwa uhuru wake.
Kila Mzanzibar afahamu kuwa anahaki kamili ya kuabudu, kueneza dini, uhuru wa maoni, uhuru wa kujumuika, kupata habari na taarifa pia kuzitoa na kuzieneza, hayo yote yanalindwa na katiba ya Zanzibar, KILICHOBAKIA NI WEWE MWANANCHI KUWA IMARA KUTUMIA HAKI YAKO BILA YA KUTETEREKA. Rejea ibara zifuatazo katika katiba ya Zanzibar:-
Ibara ya 18 “…kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake na kutafuta, kupokea na kutoa habari kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi”
Ibara ya 20 “…hakuna mtu atakaezuiwa kufurahia uhuru wake wa kuchanganyika au kujiunga… na kujihusisha atakavyo na watu wengine…”
Shime Wazanzibar tudumishe amani na tuilinde pia tutetee haki yetu tusirudi nyuma kwa hili.
Jumuiya kwa mnasaba huu inachukuwa fursa hii kuwatangazia Waislamu na Wazanzibari kuwa itafanya dua kisiwani Pemba pamoja na sala ya Ijumaa ya pamoja tarehe 11/05/2012 hapo Chakechake Pemba ikifuatiwa na mihadhara katika wilaya zote za Pemba Insha’allah.
Wabillahi tawfiq.
NAKALA:
MH: RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI.
MAKAMO WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR.
MAKAMO WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR.
MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR.
WAZIRI WA SHERIA KATIBA NA UTAWALA BORA.
WAKUU WA MIKOA ZANZIBAR.
KAMISHNA WA JESHI LA POLISI ZANZIBAR.
IDARA YA MUFTI ZANZIBAR.
 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates