WASANI 5 BORA KWA CHORUS TANZANIA 2010 - 2012








Muziki wa Hip hop hauwezi kuwa mtamu pasipo kuwa na chorus nzuri. Mwenye wimbo anaweza kuamua kuimba mwenyewe chorus ama kutafuta msaniii mwingine atakayemuimbia chorus ya kuvutia. Mchango wa msanii anayetoa melody nzuri ya chorus kamwe hauwezi kubezwa. Kuna wale ambao huvutiwa tu na chorus ya wimbo. Mara nyingi tumewahi kuzipenda nyimbo kwasababu tu ya chorus iliyoimbwa kwa ustadi mkubwa.

Tumeamua kuangalia kwa umakini kabisa pasipo upendeleo wowote kutafuta ni msanii gani aliyeshirikishwa zaidi na wasanii wa hip hop kuanzia  mwishoni mwaka juzi (2010) hadi leo na kuwaweka kwenye Top five. Katika kupata list hii tumeangalia uzuri wa chorus yenyewe na  namna wimbo ulivyohit. Kigezo cha wingi wa nyimbo alizoshirikishwa msanii hakikuwa na mchango mkubwa katika kupata wasanii bora wa chorus za hip hop mwaka 2010 – 2012.

Kuna wasanii wakubwa ambao ungehisi wanaweza kuwa kwenye list hii lakini ukweli ni kwamba nyimbo walizoshirikishwa aidha hazikuwa na impact yoyote, zilikuwa nyimbo za kawaida sana ama idadi yake haitoshi kumfanya aingie kwenye Top five. Wasanii hao ni pamoja na Ali Kiba na Diamond ambao licha ya kutokuwepo kwenye list hii wameendelea kufanya vizuri kwenye kazi walizofanya wenyewe.

Katika list hii hatukupenda kuwachanganya wasanii wa kiume na wa kike pamoja. Tutaangalia namna ya kuwaweka kwenye chart yao inayojitegemea.

Wafuatao ndio wasanii waliofanya vizuri zaidi kwa kushirikishwa kwenye chorus za wasanii wa Hip Hop nchini Tanzania mwaka 2010 –2012.

1. Belle 9




Ni ukweli uliowazi kuwa hakuna msanii wa Bongo Flava aliyeshirikishwa kwenye chorus za ngoma za hip hop na kufanya vizuri kwa mwaka 2010-2011. Kijana huyu ameendelea kudhihirisha kuwa kila anaposhirishwa kwenye ngoma, tokeo la ushirikiano huo lazima litikise mawimbI ya radio.
Kinachosikitisha tu ni kuwa Belle hajawahi kupata tuzo yoyote licha ya uwezo wake huu usio na kifani. Pamoja na kufanikiwa kwake, Belle ameendelea kuwa mnyenyekevu na kama ukipata bahati ya kukutana naye huwezi amini jinsi alivyo humble na asiyependa makuu. Hizi ni baadhi ya ngoma zilizotushawishi tumpe nafasi ya kwanza kwenye top five hii.


JINA LA MSANII ALIYEMSHIRIKISHA
JINA LA WIMBO
PRODUCER
Quick Racka
255
Marco Chali
Shetta
Nimechokwa
Pancho Latino
Jos Mtambo
Naongea na Roho
J-Ryder
Desamo
Yamebaki mazoea
Tris



2. Ben Pol


Pamoja na kutoka M-LAB mwaka juzi, Ben Pol ameendelea kufanya vizuri kwenye muziki. Mwaka huu ulikuwa mzuri kwake baada ya kuibuka na tuzo ya mwanamuziki bora wa R&B katika tuzo za Kili. Na sasa kijana huyu ameanza kujikusanyia sifa kubwa katika uimbaji wa chorus za ngoma za hip hop. Kwa speed hii aliyonayo sasa, Belle 9 anayeongoza kwenye top 5 hii anapaswa kuwa makini lasivyo atanyang’anywa taji.
Kitu kizuri kwa vijana hawa ni kwamba hivi karibuni Belle ataachia ngoma yake mpya aliyomshirikisha Ben Pol. Hatupati picha jinsi Double Bs hawa watakavyokimbiza pindi ngoma hiyo itakapotoka. Hizi ni miongoni mwa nyimbo alizoshirikishwa na kumurder chorus pasipo na huruma.


JINA LA MSANII ALIYEMSHIRIKISHA
JINA LA WIMBO
PRODUCER
Chidi Benz
Nipokee
Mesen Selekta
Darasa
Sikati tamaa
Manecky
Gosby
I got it
-
Suma Mnazaleti
Tafakari
Mesen Selekta

3. Jux




Kijana huyu kutoka kundi la Wakacha anapaswa kuweka kwenye orodha ya wasanii wa kuangaliwa sana mwaka huu. Ndiye sauti pekee wanayoitegemea Wakacha katika kupimp chorus zao. Ni msanii mwenye uwezo mkubwa katika muziki wa R&B. Uvaaji wake ambao mara nyingi humpa muonekano wa kijana wa mjini, unaendana kabisa na sauti yake tamu inayotoka pindi afunguapo mdomo wake kuimba. Kwa sababu hizo ndio maana katushawishi kumweka katika nafasi ya tatu. Hizi ni miongoni mwa ngoma alizoziremba kwa chorus tamu.


JINA LA MSANII ALIYEMSHIRIKISHA
JINA LA WIMBO
PRODUCER
Stamina
Alisema
Mesen Selekta
Cyrill
Nivumilie
Manecky
Mabeste
Sirudi tena
Pancho Latino


4. Dully Sykes




Mzaramo huyu mwenye pesa mjini kama watu wanavyomtania ameendelea kuwa king’ang’anizi bila kuonesha dalili zozote za kuchuja. Tangu enzi za Historia ya kweli na Salome enzi hizo, speed ya Dully Sykes haijabadilika zaidi ya kuongezeka kwa kasi na mambo makubwa zaidi.
Kwa sasa ni mmiliki wa studio mbili mjini. Dhahabu Records iliyomfungulia ukarasa mpya wa uprodusa na 4.12 Records, studio mpya yenye gharama kubwa kabisa. Dully bado ni miongoni mwa wasanii wanaotafutwa zaidi na wasanii wa Hip hop nchini ili awafanyie chorus. Baadhi ya ngoma alizoshirikishwa kwa mwaka 2011– 2012 ni hizi:


JINA LA MSANII ALIYEMSHIRIKISHA
JINA LA WIMBO
PRODUCER
MwanaFA
Ameen
Dully Sykes
Izzo B
Barua
Lamar
Shetta
Mdananda
Dully Sykes
Cpwaa
Action
Marco Chali


5. Steve R&B



Umaarufu wa Steve katika uimbaji wa chorus ulianza kujulikana pale aliposhirikishwa na Mr. Blue kwenye Tabasamu. Huenda kama top 5 hii ingejumuisha mwaka uliotoka wimbo huo, si jambo la kushangaza kama angekuwa ameshika nafasi ya kwanza. Lakini ukweli ni kuwa speed ya msanii huyu mwenye sauti ya pekee imeanza kupungua na ndo maana amejikuta akiwa katika nafasi ya tano. Nyimbo alizozishirikishwa kwa kipindi cha mwaka 2010– 2011 ni hizi:

  
JINA LA MSANII ALIYEMSHIRIKISHA
JINA LA WIMBO
PRODUCER
Suma Mnazaleti
Ungejua
-
Ngwea
Saizi yao
P-Funk na Q-The Don
Baby Boy
Tunapendana
Man Walter

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates